Hongera sana Dr Shein.
Anataka tusahau makanisa yaliyo chomwa eeeeh!
Mkuu nilipoona title nikashangaa maana nilihisi ni Joe Thomas mzee wa R&b kutoka pande za Obama
Wadau, kuonyesha wazanzibar ni wamoja na hawana matatizo ya kidin, shein amemteua "Mkristo" kuingia barazani. hii itaondoa propaganda zinazoenezwa na wasioitakia mema znz
Na Juma Mohammed,
MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein,amemteua Marina Joel Thomas kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee,kwa vyombo vya habari imesema uteuzi huo umeanza Juni 17 mwaka huu.
Rais amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Katiba ya Zanzibar inampa uwezo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuteuwa watu kumi kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Walioteuliwa kupitia nafasi hizo na nyadhifa zao za sasa kwenye mabano ni Balozi Seif Ali Idd(Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Mohammed Aboud Mohammed(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais) Omar Yussuf Mzee(Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo).
Wengine ni Zainab Omar( Waziri wa Ustawi wa Jamii,Maendeleo Vijana Wanawake na Watoto), Ali Mzee Ali, Sira Mwamboya (Naibu Waziri wa Afya) Juma Duni Haji (Waziri wa Afya), Fatma Abdulhabib Ferej(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais) Ramadhan Abdallah Shabaan( Waziri wa Ardhi, Maji na Maendeleo ya Makaazi) na Marina Joel Thomas.
sosi: Rais wa Zanzibar Dk. Shein amteuwa Marina Joel Thomas | Mzalendo.net
mkuu ni meHivi mteuliwa ni Me au Ke? Jina lake la kwanza siliewi elewi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Marina Joel Thomas kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee kwa vyombo vya habari imesema uteuzi huo umeanza Juni 17 mwaka huu. Rais amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Katiba ya Zanzibar inampa uwezo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuteuwa watu 10 kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar...... |
Aliyeteuliwa jina lake ni Marina Joel Thomas, hajasema kama ni Muislam au Mkristo wala hakuna sehemu yoyote kwenye hii source imeandika mambo ya ukristo. Hii heading yako cjui umeitolea masaburini au wapi
Ataapishwa kwa kitabu kipi cha kiimani au atakuja na cha kwake?
Chonde chonde jamani mtu kuitwa marina haina maana ni mkiristo. Tusibaguane kwa majina na dini