Dr. Shein amteua Joel Thomas kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi

Ni mwanzo mzuri lakini asisubiri makanisa ya chomwe ndo ajue kuna Wakristo, au ndo malipo ya kuchoma Bibilia na Nyumba za Ibada?
 
Kwanza anamerit au nikwasababu ni Joshua?Nadhani ateue mtu kwa merit sio mambo za ugodfather
 

Wadau, kuonyesha wazanzibar ni wamoja na hawana matatizo ya kidin, shein amemteua "Mkristo" kuingia barazani. hii itaondoa propaganda zinazoenezwa na wasioitakia mema znz


Na Juma Mohammed,
MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein,amemteua Marina Joel Thomas kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee,kwa vyombo vya habari imesema uteuzi huo umeanza Juni 17 mwaka huu.
Rais amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Katiba ya Zanzibar inampa uwezo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuteuwa watu kumi kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Walioteuliwa kupitia nafasi hizo na nyadhifa zao za sasa kwenye mabano ni Balozi Seif Ali Idd(Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Mohammed Aboud Mohammed(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais) Omar Yussuf Mzee(Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo).
Wengine ni Zainab Omar( Waziri wa Ustawi wa Jamii,Maendeleo Vijana Wanawake na Watoto), Ali Mzee Ali, Sira Mwamboya (Naibu Waziri wa Afya) Juma Duni Haji (Waziri wa Afya), Fatma Abdulhabib Ferej(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais) Ramadhan Abdallah Shabaan( Waziri wa Ardhi, Maji na Maendeleo ya Makaazi) na Marina Joel Thomas.


sosi: Rais wa Zanzibar Dk. Shein amteuwa Marina Joel Thomas | Mzalendo.net
Mkuu nilipoona title nikashangaa maana nilihisi ni Joe Thomas mzee wa R&b kutoka pande za Obama
 
Oh what a fancy name Joel Thomas.
Oh what's in a name?
Everything or nothing at all!
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Marina Joel Thomas kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.


Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee kwa vyombo vya habari imesema uteuzi huo umeanza Juni 17 mwaka huu.

Rais amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Katiba ya Zanzibar inampa uwezo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuteuwa watu 10 kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar......
Source: Mwananchi 18/06/2012
 
Ni Upuuzi mtupu. Huyo ameteuliwa kama yeye na si kama mwakilishi wa Wakristo. Acha ujinga hapa! Anawakilisha kundi gani la Kikristo? RC, KKKT au kundi lipi?
 
Aliyeteuliwa jina lake ni Marina Joel Thomas, hajasema kama ni Muislam au Mkristo wala hakuna sehemu yoyote kwenye hii source imeandika mambo ya ukristo. Hii heading yako cjui umeitolea masaburini au wapi
 
Aliyeteuliwa jina lake ni Marina Joel Thomas, hajasema kama ni Muislam au Mkristo wala hakuna sehemu yoyote kwenye hii source imeandika mambo ya ukristo. Hii heading yako cjui umeitolea masaburini au wapi

Ulipaswa kuuliza kupata ukweli na siyo kutoa povu na kulalama kwa mwanaume aliyebanwa nyeti zake!
 
Labda tungeulizana kuwa vigezo vya kupata hao kumi maana naona Rais aweza kumchagua hata Mkewe kuwa Mbunge au Mwakilishi .Katiba mpya iondoe upuuzi huu,wawakilishi wawakilishe wapiga kura,na rais kama alipiga kura basi naye anawakilishwa tayari.
 
Ataapishwa kwa kitabu kipi cha kiimani au atakuja na cha kwake?

inamaanisha uko kuna kitabu cha dini moja tu?, ndio maana ndio maana napendekeza vitabu vya dini viwekwe kado na kutumia katiba. kwani havisaidii kuwafanya watende haki. wazi watupu, wala rushwa wakubwa na ni warafi wa mali za taifa.
 
Kwani wakristo waliomba mwakilishi?kwani waliitaji au waisilamu wanajipendekeza baada ya kanisa kuchomwa.Wakristo hawaitaji mwakilishi wao wanauwezo wa kujiendesha wenyewe kwa kutumia raslimali zao wenyewe.
 
Chonde chonde jamani mtu kuitwa marina haina maana ni mkiristo. Tusibaguane kwa majina na dini

Nashangaa tumesharule out as if tunauhakika na kile tunachojadili. Yuko Profesa Issa Omari (emerita) alikuwa UDSM school of Education kwa Miongo kadhaa na ni mmoja kati ya maprof walioitendea nchi hii haki....ukiona tu jina hutasita kuconclude kuwa ni muislamu isipokuwa kwa sisi tunaomfahamu ndo tunajua kuwa ni Mkristo.......Pili to me it is not an issue kwasababu wakristo wa zanzibar hawajawahi kuwa na madai ya kupa muwakilishi na wala Shein hajasema anateua muwakilishi wa wakristo Zanzibar.... sifagilii utendaji unaoangalia dini za watu....Teua kulingana na Merit basi.....
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom