Dr. Shein Alia Mgawanyiko uliopo Zanzibar

Dr. Shein Alia Mgawanyiko uliopo Zanzibar

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
By Salma Said, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz


Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alitumia maadhimisho ya ibada ya Eid el Hajj kuwataka Wazanzibari kuwa wamoja huku mgawanyiko mkubwa baina ya Unguja na Pemba ukiendelea kujidhihirisha.

Akihutubia waumini wa dini ya Kiislamu jana katika Baraza la Eid el Hajj lililofanyika Mkoani, Pemba Dk Shein alisema hali ya mgawanyiko inayooekana hivi sasa haileti taswira nzuri kwa nchi. Dk Shein alihutubia Baraza la Eid ambalo halikuhudhuriwa na viongozi wa CUF kwa madai hawakualikwa.

Rais Shein alisema katika siku za hivi karibuni vitendo vya kutengana vimekuwa vikionekana waziwazi huku wengine wakichomeana nyumba na kuharibiana mazao jambo ambalo linatishia hali ya uvunjifu wa amani nchini.

“Hali ya kuwepo kwa mizozo na mivutano kwa baadhi ya mashehe na waumini inayotokana na misimamo yao, nayo inaweza kusababisha mifarakano katika jamii,” alisema.



Kauli ya CUF

Akitoa salamu za Eid kwa waumini baada ya kuswali katika Msikiti wa Kiembesamaki, Unguja, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad aliwataka wananchi kuwa na subira na kutovunjika moyo kwani hakuna jambo lisilo kuwa na mwisho wake.

Pia, alitoa pole kwa ndugu na jamaa kutokana na msiba janga la tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 16 na majeruhi 250.

Kuhusu sababu za kutohudhuria Baraza la Eid lililofanyika Mkoani, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Umma wa CUF, Salim Bimany alisema hakuna mwaliko uliofikishwa katika ofisi ya chama hicho kwa ajili ya sala hiyo.


 
Akamtafute yule jamaa mkali akamlszimishe maalim kwenda kuswali nae baraza la Eid...
 
Eti Mgawanyiko Unguja na Pemba- nani asiyejua Mgawanyiko ni kati ya wana CCM na wana CUF baada ya dhulma za Jecha. Dkt tuheshimiane.
 
haya mambo yaache yaende hivi hivi.
mwisho wa siku maji yatajitenga na mafuta.
kinachopandwa uzuri kinatiwa mbolea na maji na soon kitachipua na kuwa mche na mbaya zaid kitakuwa mti mkubwa wenye miziz mikal inayofumua hata majengo makuabwa na lami njian
 
Walipokuwa wanatamba wiki chache tu zilizopita hawakujua kuwa unabii wa ubaguzi ulikuwa unakamilika,leo wanatafuta mchawi.

Vitabu vya dini vipo,vinaeleza hekima za mfalme Suleman,viongozi wa sasa wa ngazi zote hawana hekima,wawe wa dini au serikari,tena inaniuma watu mnapoishi kwa kugawana,hakuna dhambi mbaya kama ya ubaguzi.

Jiulize swali aliyegomea mkono na atakaeziwia matibabu nani hatari zaidi,kama mtu alikataza mkono si sababu ya wewe kumnyima matibabu,mpe afya hill akiludi akiwa na afya njema ataishi na kutafakari na kuuleta mkono wake,je akifa utaupata wapi mkono wake,asante Dr.Shein kwa hekima yako na makosa kwa mwanadamu ni sehemu ya maisha.
Hapa ulijaribu kutengana na ubaguzi,maneno ya kibabe hayata wafanya WAUNGUJA na WAPEMBA kuwa wamoja zaidi ya kuongeza sumu ya chuki,waswahili wanasema kwenye msafara wa mamba ata kenge wamo.

Nini maana yangu muono wa Dr.Shein ni tofauti na waliomzunguka au wakaribu yake,kama asingetumia busara binafi angeomba ushauri kwa mzee wa kaya afanyeje juu ya mpolwaji si ajabu angesema mwache afe,je kifuatacho baada ya kufa ni mgogoro mkubwa kwani wafuasi wake wangesikia mpolwaji alinyimwa tiba wakati ni haki yake kikatiba,kwani aliwai kuwa kiongozi mkuu nani ya kaya.Asante Dr.kwa kulijua hili.

Chuki ya WAPEMBA na WAUNGUJA inaletwa na kauri zetu,so kila wakati unapopata nafasi ya kuutubia wewe ni vijembe tu vinasaidia nini,kama unasema hakuna kitakacho badilishwa na atakaeziwia leta fyoko atakiona,je ukiongea maneno ya busara utakuwa umebadiri Nini na msimamo wako ukiwa uleule wa kulijua amanita na ni wajibu wako.

Kwa nini niliwaingiza viongozi wa dini wanayaona lakini hawachukui hatua kuyakemea,uwezi ukiwa na muumini am bar hand amanita alafu wewe ukajiona unawajibika,uku tuna ubiri dunia ni ustawi wa mwanadamu huku kuna watu wanaukanyaga utawala (katiba)hapa Sheh, Padre,Mchungaji na Askofu wanafanya nini.

Uchaguzi umekwisha na hautafanyika lakini tunapaswa kutibu majeraa,la sivyo jeraa hili litakuwa la vizazi na vizazi,mwalimu alisema tukitoka kwenye ubara na visiwani tutaamia upemba na uunguja.

Kwa mtazamo wangu viongozi wa siasa jambo hili hawataliweza kamwe kwani roho zao zinavuja damu ya tamaa ya uroho wa madaraka isipokuwa viongozi wa Dini iwapo tu wataondoa woga na maslahi yao binafsi.

Tusije tukafika tukazalisha watu watakao sema liwalo na liwe,wanakuwaga wa chache sana ila madhara yake ni makubwa,viongozi wetu wakae chini rapunzel wigo wa chuki visiwani ni mkubwa kwa kweli,jambo ambalo ni baya baya sana.
 
Eti Mgawanyiko Unguja na Pemba- nani asiyejua Mgawanyiko ni kati ya wana CCM na wana CUF baada ya dhulma za Jecha. Dkt tuheshimiane.
Dhulma za Jecha????!!!! Jamani mnamwonea mzee wa watu bureeee... He is just a 'poodle'
 
jamani na wale mashekh wa uwamshoooo vp! mbona bado wako ndani hawatoki
 
Back
Top Bottom