Dr Shein a role model president we never had!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Shein a role model president we never had!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Aug 23, 2011.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dr shein ni rais wa zanzibar ambaye wengi wetu tulikuwa tunamfahamu kama mzee wa mikasi. Nimekuwa namfuatilia kwa karibu utendaji wake tangu ashike madaraka. Sasa hivi wamefikia miezi sita tangu serikali anayoiongoza ashike hatamu na kwa utendaji wake na performance ni wa kuigwa. Nimefanya tathmini haya yafuatayo:-

  Aliposhika madaraka motto ya uongozi wake ni Zanzibar yenye maendeleo na kujitegemea.

  Vitu alivyovifanya hadi sasa tangu awe kiongozi wa nchi:-

  a. Ameweza kutengeneza motto ya serikali ni kuhakikisha wizara za zanzibar zinakuwa na mipango sahihi na kutekelezeka.

  b. Amepunguza matumizi ya viongozi wa juu wa serikali pamoja na safari zisizo na muhimu na kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa chini kwa zaidi ya asilimia 100.

  c. Zanzibar ina current account surplus na imekuwa inaongezeka kila mwezi kuonyesha kukuwa kwa exports kuliko imports in the country.

  d. GDP ya zanzibar inakuwa kwa kasi na ndio inachangia kwa kukua kwa sekta ya uzalishaji (production and trade) Tanzania.

  e. Hospitali kuu ya mnazi mmoja inafanyiwa ukarabati mkubwa jambo ambalo hospitali hii ilitelekezwa kitambo.

  f. Ameweza kuwakamata wafanyabiashara wakuu wa madawa ya kulevya zanzibar na wako mbio kufikishwa mahakamani.

  g. Airport kuu ya unguja inaanza kujengwa kufikia hadhi ya kimataifa (jambo lilikuwa hekaya za kufikirika zamani) na wameanza mchakato wa kuanza kujenga airport kubwa pemba.

  h. Zanzibar wako mbioni kuanzisha shirika lao la ndege.

  i. Amepandisha bei ya karafuu kutoka shillingi 3,000 hadi Tshs 20,000 (na hivyo kutatua tatizo la umaskini kwa upande mwengine kwani ni zao la karafuu ni uti wa mgongo wa zanzibar na serikali ililitupa mgongo na matokeo Kenya wametajirika na wengine wameamua kuacha kulima karafuu na kufanya biashara na vijana wengine kuwa hawana kazi) baada ya kupanda bei vijana wengi wameamua kurudi shamba kuanza kulima tena karafuu.

  Hayo ni machache ninayo fahamu ila binafsi nampa pongezi Dr Shein wewe ni kiongozi makini na tunasikia mwadilifu mmungu akupe nguvu uendelee na umakini huo huo uwasaidie wazanzibar kwa walikuwa maskini mno!!! Tunatamani uje kutuongoza na sie Tanganyika kwani tumekosa mwelekeo kwa sasa!!!!
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  ..he comes across as more of a Technocrat than a politician.

  ..hata mimi nimekuwa impressed na hatua alizochukua kuhusu suala la bei ya karafuu.

  ..tuombe MUNGU asijekubadilika mbele ya safari kama alivyotokea kwa Ben Mkapa.
   
 3. REBEL

  REBEL Senior Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  yuko fresh mimi niko zanzibar na unayosema ni ukweli.na kikubwa ana akili nyingi kuliko ****** wenu.
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh! Kazi nzuri Dr Shein kama ndiyo hali halisi ya Zanzibar unastahili pongezi. Inawezekana ni matunda ya kufanya kazi na mtu kama Mkapa, sasa la kuangalia akiweza kuhifadhi pesa nyingi asije geuka kama Mkapa
   
 5. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Sina roli wala modo Magamba... Nipishe nisepe!
   
 6. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 940
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Zanzibar wamejitahidi sana jana nilisikia waziri wao mmoja alikuwa na ndoto ya kugombea urais anasema ndoto yake imepotea baada Mh Shein kufanya mambo ya uakika..
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,028
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Saluti kwake,sio kama huyu wa kwetu maneno meeengi kazi hakuna kazi kukeneka tu agrrrrrrrrr.
   
 8. e

  ebrah JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mbona alipokuwa makam huku bara akikuwa kimya? pia nadhan ubora wa kazi unategemea na kiwango cha elim, kwani jamaa yupo juu, sikama huyu anayepwa kwa uzuri wa sura na kusingizia ni hshima!
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mmesahau Mwinyi alipokuwa Zanzibar? je alipopewa nchi nzima . .... msinikumbushe mzee rukhsa.
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hebu subiri kidogo mpendwa,

  imekuwaje kwa muda huo mfupi awe kapata mafanikio hayo na hasa ukizingatia kuwa bajeti yake ya kwanza ndiyo hii ya june/july 2011. nadhani mipango mingi ya hiyo ilianzia kwa karume.

  in view of the aforesaid, bado navuta pumzi kumtathmini zaidi atakapotekeleza bajeti yake mwenyewe angalau kwa mwaka mmoja, kisha nitajua kama ni walewale tuliowazoea au huyu ni tofauti kidogo

  ubarikiwe!
   
 11. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  zanzibar washukuru sana mungu kupatiwa Dr. Shein, jamaa anaweza na watasonga mbele sana, huku kwetu alikuwa anabanwa idea zake zilikuwa wala hazishughulikiwi, bara nako wako wengi tu ambao wakipewa tutaona mabadiliko ya kweli.
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,540
  Likes Received: 12,816
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli well done watu km hawa inabudi waendelee kuongoza hata km muda hauruhusu,coz huyu anaanza vyema af anayekuja anafanya kinyesi so mambo hayaendi,inaumiza hiyoo,inabakia kana shein angekuwepo,!!!!!!!!!
   
 13. W

  We know next JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bravo Dr. wa Ukweli!
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mimi alinishtua tu pale alipojibu kwa jeuri wale waliokuwa wanapinga kuuzwa kwa jumba moja la kale huko Zanzibar na kusema ni jumba la serikali na serikali ina haki kuuza vilivyo vyake. Amesahau kuwa serikali ni watu na ni watu walioiweka serikali mamlakani kwa hiyo wana haki ya kulalamika na kukosoa. Nilishtuka nikasema kumbe wote ni magamba tu!
   
 15. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  <br />

  Peter principal at work - In a hierachy every employee tends to rise to his or her level of incompetence in otherwords an employees tend to be promoted until they reach a position at which they cannot work competently. Sihaba ,hali halisi inaashiria we have more than our fair share of incompetents.
   
 16. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Binafsi namuona Shein kama an angel kwa Zanzibar.Ni mvumilivu,makini na asiye na makuu.Ubora wa uongozi wake unachangiwa kiasi kikubwa na uchamungu wake.May God bless him overtime till an inevitable destiny ''death''.
   
 17. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Namtakia kila la heri
   
 18. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwa machache ninayofuatilia juu ta ZNZ, naungana nawe mkono. Na naona hata walikuwa waasi kwa maslahi ya Taifa sasa wanaungama na kumuunga mkono. Jana nimeangalia kipindi cha dk 45 cha ITV. Mgeni alikuwa Mohamed Aboud. Sikuamini kumsikia kwa kinywa chake, muonekano wa sura yake akimkubali Dr. Shein. Na alipoulizwa kama bado ana ndoto ya kumpinga au kugombea urais, akajibu alilolitaka ni uongozi mzuri unaowajali wananchi. Dr. Shein ametibu kiu yake na ya wa-ZNZ hivyo ameiondoa ndoto yake na wala hafikirii tena Urais bali anamuunga mkono na kumwombea Mwenyezi mungu ampe wepesi katika kutimiza kazi za Taifa.

  Leo jioni, mida ya saa kumi na moja vyombo vya Dola Unguja wamekamata container mbili zilizoingia ZNZ kwa boti kama mizigo ya Dagaa kutoka Mwanza, ikipita kuelekea "On transit" Malaysia. Baada ya kuzistukia na kuzikagua, wamebaini kuwa hayo maguni ya dagaa ndani ya container yalikuwa yamejaa Pembe za Ndovu. Unaweza kung'amua nani yuko makini kati ya Dola ya Bara na ile ya Visiwani. Hili pia linaongeza matumaini kwa Serikali iliyoko madarakani.
   
 19. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Hata Mkapa ana mabaya yake ila sote tunakubali amefufua kwa kiwango kikubwa uchumi wa nchi. Mkapa alipoweka doa ni pale alipoanza kujihusisha kibiashara pamoja na ufisadi wa Mchuchuma, Kiwira, EPA, Mashirika ya umma na fujo za mwembechai, Pemba. Dr shein ameanza vizuri kama alivyoanza Mkapa kama Miss Judith alivyonena tutaona huko mbeleni ila kwahiki kipindi kifupi huyu anafaa kuwa kiongozi kwani nyota njema huonekana asubuhi na sio jioni.
   
 20. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kiukweli huyu jamaa ni makini sana na nadhani pia utendaji wa serikali yake umekolezwa na baraza bora la mawaziri na wasaidizi wake aliloliunda..!! Bara huku kuogopana kutatumaliza...!! Hata maamuzi MYEPESI hatuwezi kufanya cku hz...!! Hii ni hatari na mwisho wake ni balaa...!! God bless
   
Loading...