Dr.Riwa anastahili pongezi sana katika hili jukwaa

nathamini sana mchango wako... madactri wengine wamekimbia hili jukwaa na umebaki peke yako, MZIZIMKAVU, NJIWA na wengine ... rudini humu wana JF bado wanawahitaji.

kuna tiba flani nilipata toka katika thread ya mzizimkavu ilinisaidia sana aisee..

long live JF doctor
Asante sana mimi pia nimefurahi ikiwa ushauri wangu umekusaidia ubarikiwe
 
Mungu akakuzidishie nguvu kwa kutumia kipawa chako kutoa msaada hapa J.F Dr. Riwa
 
Dr Riwa pamoja na pongezi toka kwa ndg yetu kauk najumuika naye kukupongeza kwa kutokuwa mchoyo wa tiba. Vile vile nina shida kubwa ya fungus kwenye vidole vya miguu, nimejitahidi kutumia dawa nyingi na lotion pia lakini sipati nafuu ya kudumu. Hivi sasa naumwa miguu siwezi hata kuvaa viatu vidole vimevimba na vinatoa maji kwenye joints, naomba msaada wako Dr!!!!!!!!!! Naishi Arusha.

Kwanza nakushauri roweka miguu yako kwenye Potatium permanganet (Ipo ya maji au ukipata ya cristals chukuwa chembe chache na uweke kenye maji) dakika kumi kila siku inafaa. Baada ya hapo ningekushauri uache miguu ikauke kwa upepo usijifute kwa taulo au kitaambaa chechote. Kuna dawa inaitwa BIFONAZOLE (solution ama cream) ukiipata itasaidia.
Ikimwona Dk atakuandikia systemic antifungal (kama fluconazole) kukusaidia baada ya kutumia ile dawa ya kupaka
 
Habari ya kazi Daktari, hongera kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutushirikisha na kutusaidia kupita taaluma ulinayo.

Kwa leo ningependa kupata msaada wako juu ya tatizo ambalo nimekuwa nalo kwa muda mrefu sasa,huwa nina maumivu makali sana ya mgongo ambayo nimejaribu kuyatibu mara kwa mara bila mafanikio. Huwa napata maumivu ya mara kwa mara kama vile ni crack kwenye uti wa mgongo. Je,hili linaweza kuwa ni tatizo gani?
 
Back
Top Bottom