Zion Train
JF-Expert Member
- Jun 5, 2008
- 501
- 78
nami nakupongeza dkt Riwa, hakika we ni msaada mkubwa sana kwenye jukwaa letu hili.
Dr Riwa pamoja na pongezi toka kwa ndg yetu kauk najumuika naye kukupongeza kwa kutokuwa mchoyo wa tiba. Vile vile nina shida kubwa ya fungus kwenye vidole vya miguu, nimejitahidi kutumia dawa nyingi na lotion pia lakini sipati nafuu ya kudumu. Hivi sasa naumwa miguu siwezi hata kuvaa viatu vidole vimevimba na vinatoa maji kwenye joints, naomba msaada wako Dr!!!!!!!!!! Naishi Arusha.

Naunga mkono hoja! nakumbuka enzi zile kabla ujio wa Dr Riwa kulikuwa na madaktari wafuatao :- figganigga, aspirin, Uporoto, husninyo, wiselady, Lizzy ,Dena Amsi, n.k Dah! ilikuwa balaa! ilikuwa ukisema umefanya kijipu cha ufizi tu wanakuambia ukapime ukimwi, Halaf nakumbuka siku moja jamaa alikuja kusema anawashwa sana na mgongo madaktari wetu wakamuambia ana tubakulosis. Khaaa!

ubarikiwe Dr Riwa.
si afadhali walikuwa hawa-prescribe klorokwini manake ungewakomesha wagonjwa,lol

heheh Dah! mimi ni daktari wa rufaa! hata huyu Dr Riwa akichemka basi nitakujulisheni, lakini mpaka sasa kijana anafanya vizuri sana! hongera Dr Riwa, halaf mimi nikimwaga CV langu hapa nazani kesho wagonjwa wote watatoroka muhimbili wajiunge JF. PAW na Cookie watasibitisha hii
hehehe! ww ushashindwa kazi banaa. siku hizi mambo yote miseto! kwanza ulikuwa mchungu kama unakomeshea aisee! wagonjwa wengine tunaugua vichaa hapa, shaurilo!

huku ninakoishi kichaa si marazi kichaa ni moja katika hobbies mashuhuri.
Dr. Riwa pamoja na pongezi zote hapo juu kutoka kwa mabrodaaaaaaaaz and sistaaaaaaaaaz napenda kuongezea kwa kukushukuru kwa mchango wako mkuu doctor..pia si vibaya kama itawezekana kukupa ka verse kidogo hii ndio zawadi yangu kwako dr...
iyoo ayoo ooh yoyo iyoo ayooo x2 Dr. Riwa iyoo ayooo oyoyo iyoo ayooo x2 Dr. Riwa. this is my dedication to you usikilize huu wimbo ukiwa na moja baridiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sana...
thanks have a nice day...dr.
Wandugu,
Nashukuru sana...tena sana kwa kuona na kuthamini mchango wangu hapa JF sana katika jukwaa hili la JF Doctor. Ahsanteni pia kwa dua, Husninyo ahsante 'free style'! Najitahidi kila pale ninapoweza kuchangia na/au kushea nanyi elimu hii ya utabibu na afya nikiamini kuwa kuna matatizo mengi ambayo hata wengine hawawezi kuongea na daktari wake, lakini anayamwaga hapa na tunajadili. Najua jukwaa hili lina madaktari wengine, manesi na wadau wengine mbali mbali wa afya ambao wana michango mizuuri tu, nami mara kwa mara najifunza kwao na kwa wachangiaji wengine pia! kwa kifupi ni jukwaa nilipendalo...
Nilifanya kazi kama daktari kwa miaka kadhaa Muhimbili, nikapata matatizo na mwajiri wangu (Wizara ya Afya), nikawa frustrated sana na kupractice clinical medicine, nikahamia kwenye utafiti wa masuala mbali mbali ya afya. Nimejikita zaidi kwenye 'afya ya jamii' kwa sasa, sitibu tena...hivyo sina hospitali ninayofanya kazi kwa sasa.
Lakini mara zote unapohitajika ushauri/ufafanuzi ambao upo ndani ya uwezo wangu, au issue ambayo naweza soma zaidi ili kuweza kushea nanyi nijuacho, basi karibuni kwa kuanzisha thread hapa jukwaani...au hata kwa PM...ni furaha yangu pale ninapoweza kusaidia.