Dr. Ramadhan Dau aunguruma darajani Kigamboni

Sehemu tatu muhimu za hotuba yake

1) Shukran kwa kupewa Fursa
Hakupangwa kuongea nae hakujipanga kuongea lakini Rais katambua mchango wake kampa fursa.ya kuja kuzungumza

2) Kaeleza kwa kifupi Wazo la ujenzi liliwajia 2002 baada ya kumkaribisha Mzee Mkapa akawapa changamoto hiyo

3) Anawapa changamoto kama wanataka kumfunika basi washindane kwa mambo mzuri mazuri badala ya vimajungu majungu.
Anshukuru anaondoka zake! Sijui siku hizi but by the time 1992 nina access records alikuwa ndio kijana mwenye record ya kumaliza Phd akiwa na umri mdogo zaid wa miaka 30 hapa Tanzania.
 
Wastara haumbuki, wa mbili havai moja
Who the Almighty elevates, no one can pull down.

Dr Dau is a true son of Tanzania, kwa uongozi wake kalifanyia Taifa makubwa, si mradi wa daraja peke yake bali miradi kibao!
 
UKWELI NCHI BADO INAMUHITAJI DAU,HASA HASA KWENYE KERO KAMA ZA UMEME NA BIMA
 
2016%2B-%2B1

2016%2B-%2B1

‘’Wastara haumbuki,
Wa mbili havai moja…’’

Haya ni baadhi ya maneno kwenye nyimbo niliyokuwa nikiisikia katika gramaphone nyumbani kwetu wakati nikiwa na umri mdogo sana. Mama yangu akipenda kuuimba mwimbo huu kila afanyapo kazi iwe kupika au kufua. Kuna beti za mwisho nazikumbuka na nikizpenda sana. Zilikuwa na maneno haya:

''Kwetu Congo natumaini,
Kwetu Kongo natumaini.''

Beti hizo nilizipenda kwa kuwa akifurahi alikuwa akiniadhimisha kwa kuniambia kuwa mimi nimetoka Congo.

Wakati huo Bi. Hawa biti Maftah mwanamke wa Kimanyema akimuimbia Nyerere mwimbo
maarufu katika mikutano ya TANU Mnazi Mmoja: ''Hongera mwanangu hongera...''

Wakati ule Dar es Salaam ilikuwa ndogo na jamii ya Kimanyema mjini ilikuwa na hadhi ya kipekee.

Kuanzia wanawake wao hadi wanaume.

Kubwa ni yale maumbo makubwa ukimouna mwanamke wa Kimanyema kapanda ana futi
sita na mwanamme halikadhalika.

Basi nilikuwa nizkizisikia beti hizo mama akiziimba nikawa nasisimkwa na mwili.

Nilipopata umri na kila nilipokutana na shida za dunia khasa katika mambo ya hasad na mengine kazini na kwengineko, vikwazo na nini... mama yangu akinambia: ''Wa mbili havai moja.''

Maana yake ni kuwa ikiwa Allah kakuandikia kupata ndivyo itakavyokuwa hivyo hivyo hata zije fitna kiasi gani.

Ndipo hapo inaingia, ''Wastara haumbuki.''
Yaani hutoweza kumfedhehesha aliyenyanyuliwa.

Fuatilia ukurasa huu...

Al-akh Dr Dau kamaliza kila kitu katika speech yake fupi iliyojaa hekima na busara. Wenye kuelewa wameelewa wasioelewa wakale viwembe. Wazee wa fitna sijui wamelala wapi sasa hivi
 
Franco Zetta,
Maalim wangu Sheikh Haruna ndiye aliyenisomesha ilm na
adabu za kufanya mjadala.

Akisisitiza sana heshima na lugha ya kupendeza.
Mimi siwezi kujibu kejeli itakuwa hapana tija.

Dr. Dau alipoanza kazi Bandarini aliwashangaza
sana madereva waliokuwa wakimuendesha.

Mchana akipelekwa nyumbani kula basi humkaribisha
dereva wake wakakaa meza moja na kula pamoja.

Hawa madereva walikuwa hawajaona kitu kama hicho.

Ikawa ni gumzo kwao na kila mmoja wao alikuwa anaomba
apangiwe kazi kwa Dr. Dau.

Rejea tena nikupe nyingine.
Kwa kukusaidia tu mawazo maana mimi wala siji shughulishi kusoma huu ushairi ulio mtungia mpendwa wako, kwanini usinge andika kitabu kabisa ili huo utunzi wako uwafikie watu wengi zaidi na wewe ukapewa ujira wenye tija na huyo mfadhili wako.
 
Franco ZettaIkiwa husomi ungekaa kimya usingenijibu nami ningekaa kimya.
Mohamed Said si mwandishi mtu anaeweza kumpuuza.

Hili ningependa ulijue.
Dr. Dau alinionyesha Thesis yake ya Ph D.

Ameanza na Bismillah Rahman Rahim...
Kuandika maisha ya mtu inataka utoe muda upite.

Hata kama nikiandika maisha yake sitamtoza chochote.
Hakika Dau ni mtu karim na amewafanyia ihsani wengi
si mimi peke yangu.

Rudi tena nikupe habari za Dr. Dau.
 
U
hahahaha!! hii picha hii kuna watu wanatamani wavunje simu zao wakiingalia ...

cc Ritz FaizaFoxy

13051531_1129481750426638_1956601341495157194_n.jpg
Acha Ubweha! Unafikiri hiyo picha ni tume au mahakama? Yaani Tanzania nyumbu hawaishi! Angalia kipindi cha kampeni 2010 Kikwete alikuwa anapiga picha na kina nani na akasema hawa ni watu safi nipeni nikafanye nao kazi ila baadae angalia walikuja kutwa ni watu wa aina gani! Acha kuwa na akili za kimbayuwayu
 
Franco ZettaIkiwa husomi ungekaa kimya usingenijibu nami ningekaa kimya.
Mohamed Said si mwandishi mtu anaeweza kumpuuza.

Hili nimgependa ulijue.
Dr. Dau alinionyesha Thesis yake ya Ph D.

Ameanza na Bismillah Rahman Rahim...
Kuandika maisha ya mtu inataka utoe muda upite.

Hata kama nikiandika maisha yake sitamtoza chochote.
Hakika Dau ni mtu karim na amewafanyiwa ihsani wengi
si mimi peke yangu.

Rudi tena nikupe habari za Dr. Dau.

Mzee wangu Mohamed Said Mbona sijaona hata sehemu kidogo kwenye kalamu zako kumzungumzia Prof Assad au yeye hajapata kukaaa mitaa ya kariakoo?
 
Sehemu tatu muhimu za hotuba yake

1) Shukran kwa kupewa Fursa
Hakupangwa kuongea nae hakujipanga kuongea lakini Rais katambua mchango wake kampa fursa.ya kuja kuzungumza

2) Kaeleza kwa kifupi Wazo la ujenzi liliwajia 2002 baada ya kumkaribisha Mzee Mkapa akawapa changamoto hiyo

3) Anawapa changamoto kama wanataka kumfunika basi washindane kwa mambo mzuri mazuri badala ya vimajungu majungu.
Anshukuru anaondoka zake! Sijui siku hizi but by the time 1992 nina access records alikuwa ndio kijana mwenye record ya kumaliza Phd akiwa na umri mdogo zaid wa miaka 30 hapa Tanzania.

Mkuu hebu tuwekee hiyo Cv yake ambayo unasema kamaliza PhD 1992 na hiyo Degree ya kwanza kamaliza mwaka gani?...Humu Jukwaani kuna watu wapo radhi kuongea uongo hili kuwa ukweli aisee
 
Una maana ktk watu mashuhuri, Waislamu, huyu ndo kafanya la maana kuliko wote hadi ufikie kutukana wasio wa dini yako? Dau hajatumia pesa yake au hajatafuta pesa nje na michango ya wanachama ambao ni wa-TZ kwa uanachama wao.

Kuna mtu kauliza, hali ingekuwaje kama daraja hili lingejengwa na taasisi ya kiislamu? Nadhani munaiondolea heshima dini na kuonyesha kwamba haina watu wenye kufanya mambo ya maana zaidi ya Dau. Naamini Uislamu uko juu kuliko uzembe unaoandikwa hapa.

Wakristu wamejenga KCMC. Wamejenga Bugando tena miaka ileee! Hizi zikiwa pesa zao siyo hata michango ya waislamu.
Watu kama wewe sijui unadhani daraja hili ni investment ya kiislamu? Shiiit!
Nionyeshe tusi mwenye post yangu niliyotukana.
 
2016%2B-%2B1

2016%2B-%2B1

‘’Wastara haumbuki,
Wa mbili havai moja…’’

Haya ni baadhi ya maneno kwenye nyimbo niliyokuwa nikiisikia katika gramaphone nyumbani kwetu wakati nikiwa na umri mdogo sana. Mama yangu akipenda kuuimba mwimbo huu kila afanyapo kazi iwe kupika au kufua. Kuna beti za mwisho nazikumbuka na nikizpenda sana. Zilikuwa na maneno haya:

''Kwetu Congo natumaini,
Kwetu Kongo natumaini.''

Beti hizo nilizipenda kwa kuwa akifurahi alikuwa akiniadhimisha kwa kuniambia kuwa mimi nimetoka Congo.

Wakati huo Bi. Hawa biti Maftah mwanamke wa Kimanyema akimuimbia Nyerere mwimbo
maarufu katika mikutano ya TANU Mnazi Mmoja: ''Hongera mwanangu hongera...''

Wakati ule Dar es Salaam ilikuwa ndogo na jamii ya Kimanyema mjini ilikuwa na hadhi ya kipekee.

Kuanzia wanawake wao hadi wanaume.

Kubwa ni yale maumbo makubwa ukimouna mwanamke wa Kimanyema kapanda ana futi
sita na mwanamme halikadhalika.

Basi nilikuwa nizkizisikia beti hizo mama akiziimba nikawa nasisimkwa na mwili.

Nilipopata umri na kila nilipokutana na shida za dunia khasa katika mambo ya hasad na mengine kazini na kwengineko, vikwazo na nini... mama yangu akinambia: ''Wa mbili havai moja.''

Maana yake ni kuwa ikiwa Allah kakuandikia kupata ndivyo itakavyokuwa hivyo hivyo hata zije fitna kiasi gani.

Ndipo hapo inaingia, ''Wastara haumbuki.''
Yaani hutoweza kumfedhehesha aliyenyanyuliwa.

Fuatilia ukurasa huu...

Kwa nyimbo hizo,mshua ameisoma namba mwanzo mwisho.
 
Mkuu hebu tuwekee hiyo Cv yake ambayo unasema kamaliza PhD 1992 na hiyo Degree ya kwanza kamaliza mwaka gani?...Humu Jukwaani kuna watu wapo radhi kuongea uongo hili kuwa ukweli aisee

Nikuwekee kwa Lipi? Kwa wema upi? itabadilisha kipi kwako na kwa Dau?
Nikupe tu hints,
Division one Olevel na Advance Aghakhan Secondary School ( Mnaosema katajirikia NSSF mjue huyu hajawahi kuwa Maskini tangu anazaliwa)
University of Dar es salaam (Hons 1st Class)
Phd (Newzealand)

Kuna special record kwny hiyo hiyo Degree ya kwanza UDSM aliiweka kwa kusoma kipindi kifupi zaid kwa kumaliza units zote na kubaki anasubiri ku graduate na wenzie! Kishawahi kuwa Lecturer akiwa Mkurugenzi Masoko Bandarini (1995-2001) kutokana na record yake pale.
Uhuishaji na mikakati ya kimasoko iliyoipaisha Bandari wakati wa Mkapa mpaka kuanza kujiendesha kisasa ndio vilivomfanya apewe NSSF. Kila alipotoka changamoto inayobaki ni namna ya kufikia viwango vyake ndio sababu kuna vita inaendelea ya kumchafua!
 
Mohammed Said una mambo mengi sana ya sisi kujifunza juu ya hulka binafsi za Alhaj Dr Dau. Hawa makaaaaaafir wasikutie hasira ukashindwa kutupa ya zaidi. Nimejisikia faraja sanaaaaaa kwa namna ambavyo kasoma hiyo aya na ile bismillah aliyoitamka pale mwanzo. Hii ndiodini ya haqi. Allah akbar
Msongonoma,
Dr. Dau
tumekaa pamoja na kusafiri pamoja ndani na nje ya nchi.
Nimejifunza mengi kutoka kwake.

Kubwa ni ''humility.''
Kanifunza mengi sana.
 
Najiuliza tu; ingekuwaje endapo mh. JPM hasingemuita na kumpa nafasi ya kuongea?
 
Nikuwekee kwa Lipi? Kwa wema upi? itabadilisha kipi kwako na kwa Dau?
Nikupe tu hints,
Division one Olevel na Advance Aghakhan Secondary School ( Mnaosema katajirikia NSSF mjue huyu hajawahi kuwa Maskini tangu anazaliwa)
University of Dar es salaam (Hons 1st Class)
Phd (Newzealand)

Kuna special record kwny hiyo hiyo Degree ya kwanza UDSM aliiweka kwa kusoma kipindi kifupi zaid kwa kumaliza units zote na kubaki anasubiri ku graduate na wenzie! Kishawahi kuwa Lecturer akiwa Mkurugenzi Masoko Bandarini kutokana na record yake pale.
Uhuishaji na mikakati ya kimasoko iliyoipaisha Bandari wakati wa Mkapa mpaka kuanza kujiendesha kisasa ndio vilivomfanya apewe NSSF. Kila alipotoka changamoto inayobaki ni namna ya kufikia viwango vyake ndio sababu kuna vita inaendelea ya kumchafua!
Pohamba,
Mimi nimefanya kazi na Dr. Dau mie nikiwa ofisa mdogo katika idara yake.
Siku moja wakubwa wenzake wakawa wanamsema kuwa kaja kunufaika
bandarini.

Mimi sikuweza kustahamili.

Nikawaambia kuwa kwa ''standard,'' za hapa kwetu Dar es Salaam Dr. Dau
katoka ukoo unaojiweza sana kiasi hata darasa la kwanza kasoma Aga Khan
sio Kinondoni Primary School kama Mohamed Said au Makurumula na Mzimuni.

Nikawaeleza kuwa Dr. Dau anasoma anaendesha gari yake mwenyewe kapewa
na baba yake.

Mohamed Said kapanda sana gari hii.

Nikaendela kuwaeleza kuwa na baba yake ana majumba kadhaa hapa mjini.

Nikawamalizia kwa kuwaambia kuwa wasidhani kuwa suti Dr. Dau kaja kuvaa
hapa Bandarini.

Dr. Dau akivaa suti na tai toka utoto wake.
Ndiyo ile unavyomuona yuko ''dandy.''

Jamaa walibaki kinywa wazi.
 
Hahahahahahaha....kweli kichwani hakuna kitu wewe tatizo mnapenda kupata data kwenye vijiwe vya kahawa...pole sana

Wewe unapata kwny vilabu cha pombe!
Hajasoma vyuo wala shule za kuokoteza. Unaweza kwenda ku prove. UDSM na Aghakhan Schools zipo na ni maarufu unaweza kwenda kujiridhisha.
Facts huwa hazibadiliki hata zikataliwe na watu wote. We unadhani elimu ya mtu inapigiwa kura ya maoni kuwa wengi wakikataa unakuwa hujasoma?
Mabwana zako washamzushia kashfa zote ushamsikia mtu anagusia ukakasi kwenye elimu au weledi wake?
 
Mchunguzi,
Nakuomba kwa hisani yako hebu soma hii labda utaelewa
nini nilichokusudia:
Mohamed Said: Nyerere Alipounguruma Umoja wa Mataifa, New York 1955
Nashukuru kuniongoza kwenye thrd nyingine, lakini hakika ya jinsi tulivyokuelewa ktk hili la Dau, hebu angalia wanachosema wachangiaji. Kwa wengine Dau ni sifa kwa Waislamu wote Haiwezekani wote tukosee kukuelewa lengo lako.

Ni bahati mbaya sana kwamba, watu wanajisikia vizuri kumuona Dau kama muislamu badala ya mtanzania. Hata daraja sasa ni matunda ya uislamu wake.
 
Back
Top Bottom