- Huyu ni mmoja wa watumishi wa umma ambao nilitokea kumwamini sana. Nilimwamini mno kwani hana harufu ya ufisadi, ni mwadilifu na mtu mwenye maadili ya hali ya juu. Tangu nimjue nikiwa mwanafunzi pale chuo kikuu cha Dar es salaam.
- Dr. Philip Mpango anafahamu fika kwamba chama chetu CCM kimelikoroga kule Zanzibar na hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Wamarekani kupitia MCC ni stahiki kabisa. Ningeshangaa sana Wamarekani Wangetupa hela zao au wangekaa kimya baada ya ile Sinema ya Jecha na Shein kule Zanzibar.
- Mwalimu wangu mpango, mara ya mwisho tulikutana pale tume ya mipango na wachumi wengi waandamizi. Ulionyesha uzalendo wako, lakini muda mfupi baada ya hapo uliekea Marekani kupitisha bakuli. Leo nashangaa unaimba wimbo wa CCM kwamba Tanzania haihitaji Misaada. Wewe kweli ni wa kusema kwamba Tangu December mwaka jana, Tanzania ilishajiandaa kutokuwategemea wamarekani? Nijiaminishe kwamba haya maneno ulilazimishwa kuyatamka na siyo yako. Kwani unajua fika kwamba Tanzania ina umasikini wa ajabu. Watakaoumia ni masikini, siyo nyinyi watawala.
- Nashindwa kuelewa kama kweli ulishajitayarisha kwa nini ulienda kupitisha Bakuli Marekani September mwaka Jana? Ningekuwa wewe ningekaa kimya au ningejiuzulu badala ya kujidhalilisha na taaluma ya uchumi.
- Mwalimu, hali halisi siyo shwari. Nzi wangu kwenye vyumba vya kidiplomasia vimenitonya, nami nakuonya ingawa hizi habari tayari zishakufikia, Natumai umeshajitayarisha vya kutosha baada ya wamarekani kukupapasa. Nadhani ungejitayarisha vizuri zaidi, kwa hili pigo zito linalokuja. Umoja wa bara la Ulaya yaani (EU) na Uingereza nao wanakuja na bakora lao sijui utawaambia nini watanzania. Habari ndio hiyo ila umenisikitisha jinsi watu wanavyobadilika ghafla wanapoingia kwenye siasa