babykailama
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 251
- 243
Je ni kweli na ni halali kuwa pale Mh. Lugola, Mbunge na Askari wa Akiba alipotofautiana na Waziri kwa kutaka posho ya chakula (lishe) iwe sawa kwa Maskari wote, Mh. Dr. Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani) akamjibu kwa kulieleza Bunge kuwa huo ni utovu wa nidhamu?
Fikra zangu:
Hata kama ingekuwa ni katika kutii amri, Je Nchimbi (Waziri) ndiye wa kumpa amri Lugola (Mbunge)? Mimi nafikiri ni karibu zaidi na kinyume chake yaani Bunge ndilo linaelekeza na kiuidhibiti Serikali!
Hata context ingekuwa ni jeshini; dhana ya kulazimisha Askari yeyote kutotofautiana kabisa kwa jambo lolote na Mkuu wake ni ya kukandamiza ubunifu na wakati mwingine haki?
Kinachozungumzwa Jeshini ni utii wa Sheria, Taratibu na Amri halali na si kuminya na kuzuia mawazo tofauti (diversity in thoughts)-chemchem ya maendeleo katika jamii yeyote.
Aidha pia sikubaliani na mtu anayeweza kuhalalisha jambo kama hili kuwa Waziri alikuwa anatania; maana Mbunge alikuwa hatanii bali alikuwa akisubiri jibu la swali makini linalotaka uwepo wa haki katika namna ya kuwa treat makamanda wetu wote. Tena, Katibu wa Bunge hatujasikia akituelekeza kipindi cha kuwasilisha utani Bungeni.
Dr. Nchimbi pata somo kwamba, diversity & differentiations cannot be construed as disharmony and impudence