Dr Mwakyembe na kashfa ya misaada Kyela

Dr Mwakyembe na kashfa ya misaada Kyela

Of course, hakuna taabu, bali unapaswa kuwashukuru waliokusupport huo msaada na sio kujifanya wewe umetoa kwa fedha zako wakati umechangiwa, hii ndio hoja inayojadiliwa hapa na si vinginevyo!
Jamaa yangu amba.nkya unanishangaza yaani Mwakyembe jana tu kaeleza TRC itapata vichwa 25, mabehewa ya Abiria pamoja na ya mizigo zaidi ya 100 wewe unataka awataje na wafadhili watakaotoa misaada hiyo au mikopo?
Sasa wewe unazungumzia jimbo la Kyela unasahau huyu jamaa yuko Nchi nzima mpaka na Reli ya Ubungo na Bandari au mnahasira anavyowabana na kuwatimua huko Bandarini maana mlijipanga ndugu watupu mpaka mkasahau kwenu Hai, hivi ni kwanini usiwaulize hao Wabunge wengine mbona hatuwasikii majimboni kwao?
Hapa sijaona Mantiki ya kumfananisha mbunge yoyote na Waziri kama Mwakyembe au Magufuli na ninakuhakikishia ni vichaa tu watakaomnyima kura asirudi Bungeni na kuwa Waziri kwa kipindi cha 2015 - 2020
 
Last edited by a moderator:
Unaona, amesema ITAPATA na si kuwa NITATOA Vichwa 25 na ........

Mwakyembe nimeshasema mara nyingi kuwa uwezo wake mkubwa sana ila anashangaza pale anapoanza usanii ambao hatakiwi kabisa kuufanya. Kudanganya kwake hajaanza leo. Wakati wa uchaguzi alimuahidi mzee mmoja gari na mzee karibu afe kwa kumpigania. Uchaguzi ulipoisha akawa ameshamsahau mzee wa watu hata anaitwaje. Mzee akaishia kufukuzwa kazi na kuuguwa na wala pesa za matibabu akawa hana..... hukumu hapahapa duniani.

Kuna daraja alitaka kulidandia kuwa ni yeye alijenga, hapo akawa amemtibua Gen. Mwamunyange maana ni JWTZ ndiyo walilijenga. Sikumbuki vizuri ile sakata iliishia wapi ila wana Kyela kama Mkulima wanaweza kuja hapa kutufafanulia.

Tatizo wengi wenu ni vipofu sana wa Mwakyembe. Hamtaki kusikia chochote kuhusu yeye hata kama ni kweli. Kama wote tungeliungana na kumbana huyu jamaa na achape kazi bila usanii, hapo ndiyo mngelisema hata Dr. Slaa ni cha mtoto. Ila ndiyo hivyo tena, ataishia kuwa Mbunge na sanasana Waziri maana akija jaribu kunyenyia kichwa juu zaidi, ndipo watu wanaomfahamu wataanika maovu yake waziwazi ambayo mtakosa hata la kusema.

Mwakyembe chapa kazi bana na achana na USANII. You can do better and you know it.
Jamaa yangu amba.nkya unanishangaza yaani Mwakyembe jana tu kaeleza TRC itapata vichwa 25, mabehewa ya Abiria pamoja na ya mizigo zaidi ya 100 wewe unataka awataje na wafadhili watakaotoa misaada hiyo au mikopo?
Sasa wewe unazungumzia jimbo la Kyela unasahau huyu jamaa yuko Nchi nzima mpaka na Reli ya Ubungo na Bandari au mnahasira anavyowabana na kuwatimua huko Bandarini maana mlijipanga ndugu watupu mpaka mkasahau kwenu Hai, hivi ni kwanini usiwaulize hao Wabunge wengine mbona hatuwasikii majimboni kwao?
Hapa sijaona Mantiki ya kumfananisha mbunge yoyote na Waziri kama Mwakyembe au Magufuli na ninakuhakikishia ni vichaa tu watakaomnyima kura asirudi Bungeni na kuwa Waziri kwa kipindi cha 2015 - 2020
 
Last edited by a moderator:
issue sio majungu wala chuki bali kinachotakiwa ni kujitoa kwake mwenyewe na sio kupitia mgongo wa wengine na hilo ndilo wanachama wake wanahoji pia

Kwani wewe kilichokuuma ninini. Ligwani anawavurug wkai kake kuko shwari. Amba.nkya, acha kutumika kama toilt paper ati!
 
Mtu mwenye akili,akikupa mawazo ya kipumbavu ,na wewe una akili,usipoyakataa anakudharau -jk.nyerere-mtoa hoja jipime katika nukuu hii,naamini wewe ni maskini wa mawazo,utaishia kuhesabu idadi ya waleta misaada kyela hadi uote mvi,ganga njaa vizuri,style zingine siyo.
 
Inawezekana pia sababu ya ugonjwa kama ulivyosema, vipi wapinzani nguvu yao ikoje hapo?

Nguvu ya upinzani inazidi kuimarika kila uchao, mbaya zaidi hadi vijijini ngome ya ccm zimevunjwa, hawana pa kutokea, wanasoma upepo
 
Kwani Mbunge anatoaga hela zake binafsi kwa maendeleo ya jimbo?
Nijuavyo ni ushawishi wa mbunge/diwani kwa wafadhili na kwa serikali pia
Ama kweli ukiwa kiongozi kwenye nchi maskini kama TZ ni lawama tupu.
 
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, kuna tetesi kwambaDr Mwakyembe Mbunge wa Kyela amejikuta anapata kashfa na aibu kubwa jimbonikwake Kyela baada ya kutoa na kuahidi misaada mbalimbali wilayani humo; ikiwani njia ya kujibu mapigo kwa Asasi na makamanda wa CHADEMA waliotoa misaada wilayani hapa.
Inasemekana kashfa na aibu ya kufungua mwaka 2013, imempatawaziri huyo baada ya kujifanya ametoa msaada wa magodoro 40 na mashuka 60kwenye hospitali ya wilaya ya Kyela, kumbe ni msaada uliotolewa na Kampuni yaBioland. Aidha, Dr Mwakyembe ameahidi kutoa madawati 180 kupitia mgongo wa benkiya NBC, tawi la Kyela, hata hivyo kuna taarifa kuwa benki hiyo imemkatalia yeyekuwa ndiye ametoa madawati hayo kwa kigezo kuwa benki haiendeshi shughuli zakekisiasa na itakabidhi msaada wa madawati hayo muda wowote itakapoona inafaa. Yote hayo alikuwa anajaribukujibu mapigo ya Asasi ya SCSA au Pambana Saidia Jamii iliyotoa madawati 100kwenye shule ya msingi Ikombe.
Kama haitoshi, Dr Mwakyembe akiwa kwenye mkutano wa hadharakata ya Ngonga karibu na nyumbani kwake aliahidi kutoa mifuko 100 ya sarujiakijibu mapigo ya Diwani wa CHADEMA, kamanda Tamali aliyetoa mifuko 20 kwenyekata hiyo. Ahadi hiyo imeibua hasira kubwa kwa wanakyela kutokana na ukweli kwamba mbunge huyo haonekani jimbonikwake na ahadi nyingi alizotoa jimboni hapa hakuna iliyotimizwa, ndio maana wanakyelahawana imani naye tena.
Kutokana na hali hiyo, kikao cha ndani cha dharura cha CCMwakiwemo wazee kiliitishwa wilayani hapa ambacho kilikuwa mahsusi kumuonya mbungekuhusu mambo hayo aliyofanya kwani ni kuwadanganya wananchi ikizingatiwa kuwaahadi nyingi alizotoa jimboni hapa hajatekeleza.
Upepo na hali ya siasa kwa mbunge huyo si shwali wilayanikyela kama lilivyokuwa 2010, tofauti na watu wengi wanavyodhani kupitia vyombovya habari akionekana mchapakazi kitaifa lakini jimboni kwake wamemchokakwasababu amelitelekeza jimbo lake.

Nawasilisha................

Source: Mdau kutoka Kyela.

Acha umbumbumbu, kazi ya Mbunge si kushindana na asasi kutoa misaada kwa wananchi bali kusimamia maendeleo ya wananchi kupitia fedha zao za kodi, Kwa hiyo wewe ulitaka asitoe msaada kwasababu asasi zingine zimetoa? NB: Mbunge anapotoa msaada hata kama umetolewa na bank au taasisi nyingine yoyote sio mbaya kwani yeye hupokea misaada hiyo kama mwakilishi tu na baadae hukabidhi wananchi walengwa.
 
Uchawi sio Lazima uende Porini ukate miti na kuvaa kaniki jeusi na kutamka maneno yasio eleweka, Lazima Mtoa Mada atambue Kuwa nafasi ya Mbunge ni kuwashawishi watu mbalimbali ili waweze kutoa misaada ya kuweza kusaidia Jimbo lake, Acha uchawi wa maneno ya kisiasa, mimi naona una agenda nyingine ya kumchafua huyu ndugu.

Kwa nini usielezee kazi kubwa anaifanya ya kuisafisha TPA na Kwa kipindi kifupi Pato limeongezeka kwa zaidi ya asilimia 100. Tuache uchawi wa maneno, naomba kuwasilisha
 
Hata kama Wanakyela hawatamchagua, lakini kama Taifa atachaguliwa. Hope katiba mpya itaamua Waziri asiwe mbunge ili kuleta ufanisi, na atandelea kutumikia taifa!
 
Acha umbumbumbu, kazi ya Mbunge si kushindana na asasi kutoa misaada kwa wananchi bali kusimamia maendeleo ya wananchi kupitia fedha zao za kodi, Kwa hiyo wewe ulitaka asitoe msaada kwasababu asasi zingine zimetoa? NB: Mbunge anapotoa msaada hata kama umetolewa na bank au taasisi nyingine yoyote sio mbaya kwani yeye hupokea misaada hiyo kama mwakilishi tu na baadae hukabidhi wananchi walengwa.
wewe ndio mbumbumbu maana umekurupuka bila kufuatiliamaelezo ya kutosha yaliotolewa kwenye thread hii, tunachojadili hapa ni kwamba pamoja na mbunge kuwa naushawishi kwa wadau mbalimbali kuchangia shughuli za maendeleo ni lazima piaappreciate wadau waliochangia, kwa mfano; alitakiwa aseme 'naishukuru kampuniya Bioland na NBC kwa kuchangia misaada nilioitoa' na si yeye pekee kuwa ametoamchango husika as if katumia mfuko wa jimbo, nadhani umeelewasasa.

Hata kama Wanakyela hawatamchagua, lakini kama Taifa atachaguliwa. Hope katiba mpya itaamua Waziri asiwe mbunge ili kuleta ufanisi, na atandelea kutumikia taifa!
Upo sahihi afanye kazi za kitaifa, lakini itategemeakatiba mpya kuwa tayari 2015…. Ouote from Erythrocyte "Ukweli ni kwamba Dr Mwakyembe pamojana uchapakazi wake huku kwenye uwaziri , Jimboni utendaji kazi wake ni hafifumno , Tuwe wakweli , uhamasishaji wa maendeleo ni kama hakuna kabisa , Ni kwelikabisa kwamba Dr ana maadui wengi lakini hiyo isiwe kinga ya watu kushindwakuhoji utendaji wake jimboni , kiukweli kilichombeba Mwakyembe Kyela ni ileRipoti ya RICHMOND tu vinginevyo hakuna kitu , ule uhamasishaji wa kibunge kwawananchi kujiletea maendeleo ni kama hakuna kabisa , Huo ndiyo ukweli hata kamahatupendi kuusikia ,na tetesi za chini ya carpet zinasema amekorofishana nawapambe wake wa siku zote, akina Richard Kirumbo & co ( wazee wa bia ) ,kwa hiyo hata zile propaganda za kupofusha wanakyela ili wasione mapungufu yaDr a.k.a INGAMBAKO hazipo tena ! Shortly ni kwamba pamoja na mazuri yote yaMwakyembe, lakini kyela imemshinda ! Sasa tatizo sijui ni ugonjwa au uwaziri ?Yetu macho"
 
Uchawi sio Lazima uende Porini ukate miti na kuvaa kaniki jeusi na kutamka maneno yasio eleweka, Lazima Mtoa Mada atambue Kuwa nafasi ya Mbunge ni kuwashawishi watu mbalimbali ili waweze kutoa misaada ya kuweza kusaidia Jimbo lake, Acha uchawi wa maneno ya kisiasa, mimi naona una agenda nyingine ya kumchafua huyu ndugu.

Kwa nini usielezee kazi kubwa anaifanya ya kuisafisha TPA na Kwa kipindi kifupi Pato limeongezeka kwa zaidi ya asilimia 100. Tuache uchawi wa maneno, naomba kuwasilisha[/QUOTE
utendaji na ufanisi wake kama waziri havihusiani na thread hii, rudia kusoma thread ndipo urudi kuchangia hapa
 
Jamani huyu mtu yupo sawa kwa uwezo wa uelewa wake. Tusipoteza muda kujadili trivial things
 
mwezi umepita niliandika stories za dadangu juu ya siasa kyela na mwakiembe.

wenzenu wanajiandaa mwakiembe agombee ubungo au kawe.

kyela eti kila siku mnaomba pesa na hamfanyi kazi. wakinga na wachaga wanatawala biashara zote mjini. pia mnapenda kuchagua machifu.
 
issue sio majungu wala chuki bali kinachotakiwa ni kujitoa kwake mwenyewe na sio kupitia mgongo wa wengine na hilo ndilo wanachama wake wanahoji pia

...Cry me a river....get life ..hivi mnafikiri hizi lia lia zitawasaidia chochote ? Kila siku mnavyojaribu kumchafua ndivyo anavyozidi kutakata kwa mambo yake kikazi na wa TZ wa sasa sio wajinga kama nyie... !! Huyo mwenyewe aliyeongoza kampeni ya kumlisha sumu sasa kaufyata....

Tunaangalia anafanya nini kwa wananchi wake, na taifa sio hizi kelele za kila siku za maandazi na vitumbua....gademuh..!!
 
Uchawi sio Lazima uende Porini ukate miti na kuvaa kaniki jeusi na kutamka maneno yasio eleweka, Lazima Mtoa Mada atambue Kuwa nafasi ya Mbunge ni kuwashawishi watu mbalimbali ili waweze kutoa misaada ya kuweza kusaidia Jimbo lake, Acha uchawi wa maneno ya kisiasa, mimi naona una agenda nyingine ya kumchafua huyu ndugu.

Kwa nini usielezee kazi kubwa anaifanya ya kuisafisha TPA na Kwa kipindi kifupi Pato limeongezeka kwa zaidi ya asilimia 100. Tuache uchawi wa maneno, naomba kuwasilisha[/QUOTE
utendaji na ufanisi wake kama waziri havihusiani na thread hii, rudia kusoma thread ndipo urudi kuchangia hapa

hv huyu mchaga wa tpa nkya toka asimamishwe bandarin kwa kukosa vigezo ameona njia pekee ni kumchafa m2mishi kwa siasa za matope mimi ni upinzan ila kwa hili utaifa kwanza viva mwakyembe
 
Pigeni tu kelele ndugu zangu ila sie wanakyela ndio tunajua, mwakyembe nae anajua na kaanza kuaga rasmi apa kyela hana chake,.. Wembe uliotumika kumnyorea mwakipesile ndo kuo umeandaliwa na kunolewa vizuri kumnyoa mwakyembe,. Hutaki kunywa sumu
 
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, kuna tetesi kwambaDr Mwakyembe Mbunge wa Kyela amejikuta anapata kashfa na aibu kubwa jimbonikwake Kyela baada ya kutoa na kuahidi misaada mbalimbali wilayani humo; ikiwani njia ya kujibu mapigo kwa Asasi na makamanda wa CHADEMA waliotoa misaada wilayani hapa.
Inasemekana kashfa na aibu ya kufungua mwaka 2013, imempatawaziri huyo baada ya kujifanya ametoa msaada wa magodoro 40 na mashuka 60kwenye hospitali ya wilaya ya Kyela, kumbe ni msaada uliotolewa na Kampuni yaBioland. Aidha, Dr Mwakyembe ameahidi kutoa madawati 180 kupitia mgongo wa benkiya NBC, tawi la Kyela, hata hivyo kuna taarifa kuwa benki hiyo imemkatalia yeyekuwa ndiye ametoa madawati hayo kwa kigezo kuwa benki haiendeshi shughuli zakekisiasa na itakabidhi msaada wa madawati hayo muda wowote itakapoona inafaa. Yote hayo alikuwa anajaribukujibu mapigo ya Asasi ya SCSA au Pambana Saidia Jamii iliyotoa madawati 100kwenye shule ya msingi Ikombe.
Kama haitoshi, Dr Mwakyembe akiwa kwenye mkutano wa hadharakata ya Ngonga karibu na nyumbani kwake aliahidi kutoa mifuko 100 ya sarujiakijibu mapigo ya Diwani wa CHADEMA, kamanda Tamali aliyetoa mifuko 20 kwenyekata hiyo. Ahadi hiyo imeibua hasira kubwa kwa wanakyela kutokana na ukweli kwamba mbunge huyo haonekani jimbonikwake na ahadi nyingi alizotoa jimboni hapa hakuna iliyotimizwa, ndio maana wanakyelahawana imani naye tena.
Kutokana na hali hiyo, kikao cha ndani cha dharura cha CCMwakiwemo wazee kiliitishwa wilayani hapa ambacho kilikuwa mahsusi kumuonya mbungekuhusu mambo hayo aliyofanya kwani ni kuwadanganya wananchi ikizingatiwa kuwaahadi nyingi alizotoa jimboni hapa hajatekeleza.
Upepo na hali ya siasa kwa mbunge huyo si shwali wilayanikyela kama lilivyokuwa 2010, tofauti na watu wengi wanavyodhani kupitia vyombovya habari akionekana mchapakazi kitaifa lakini jimboni kwake wamemchokakwasababu amelitelekeza jimbo lake.

Nawasilisha................

Source: Mdau kutoka Kyela.

WATANZANIA tukiendelea na majungu haya hatutafika mbali kimaendeleo.
Magodoro aliyotoa Dk.Mwakyembe katika hospitali ya wilaya ya Kyela amenunua Dar es Salaam mtaa wa Msimbazi. Madawati 180 ya msaada ambayo bado yanaendelea kutengenezwa mjini Kyela ni saada kutoka Benki ya NMB baada ya mbunge huyo kuwaomba na siyo benki ya NBC kama mtoa habari alivyoeleza. Lakini chanzo cha majungu haya yote ni watu wawili 1- Burton Mwakasitu, huyu ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya kata ya Itunge. Mwakasitu anachuki binafsi na Dk.Mwakyembe kwasababu wakati wa mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM wilaya ya Kyela alikuwa upande wa kundi linaloongozwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya mstaafu John Mwakipesile. Katika uchaguzi huo Mwakipesile alikuwa na wagombea kadhaa walioogombea uenyekiti wa CCM wilaya akiwemo Bw.Makete ambaye alishindwa nafasi hiyo iliyochukuliwa na Diwani wa Kata ya Ipinda Dk.Hunter Mwakifuna ambaye yupo upande wa Dk.Mwakyembe. mtu mwingine anayeeneza majungu haya ni Emmanuel Kiketelo Mwamlinge, huyu alikuwa Katubu wa mbunge Dk.Mwakyembe lakini aliondolewa nafasi hiyo tangu mwaka juzi kutokana na kashfa ya kupewa rushwa ya Sh.milioni 100 na kampuni moja (jina tunalihifadhi) ili iweze kujenga daraja la mto Lusungo wilayani Kyela.
Dk.Mwakyembe baada ya kuelezwa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kuhusu tabia chafu ya katibu wake, alichukua hatua ya kumsimamisha kazi Mwamlinge ambaye naye kwa kuwa hakufurahia maamuzi yaliyochukuliwa na boss wake amekuwa akieneza mambo kadhaa kumchafua Dk.Mwakyembe. Mwamlinge ambaye sasa amejiunga kundi la Mwakipesile hivi sasa kundi hilo lipo katika mchakato wa kuandaa mtu atakayegombea ubunge jimbo la Kyela 2015. Lakini kundi hilo ili kuweza kufanikiwa wameanza na spidi ya kumchafua Dk.Mwakyembe harakati ambazo zinafahamika na vyombo vya usalama.
 
kweli ukweli cku zote ndo utakuweka huru..funguka mdau
 
Back
Top Bottom