VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Muda wako umewadia. Muda wako wa kusema ukweli zaidi. Lowassa amekuchokoza leo mjini Dodoma. Amedai kuwa yeye hakuhusika na Richmond. Sakata la Richmond, I mean. Amedai kuwa sakata hilo lilitungwa na kulenga Uwaziri Mkuu wake tu.Hakukuwa na zaidi. Kwa maana nyingine, Dr. Mwakyembe na Kamati yako teule ya Bunge mlitunga kashfa ya Richmond. Yaani,Dr.Harrison Mwakyembe na Kamati yake ni wazushi na waongo!
Dr. Mwakyembe, umepata nafasi adhimu na adimu isiyo na msimu. Nafasi ya kusema hata yale ambayo hukusema Bungeni Dodoma ulipokuwa ukiwasilisha Ripoti ya Kamati yako. Ukweli juu ya sakata la Richmond. Kama Lowassa ameruhusiwa na chama na Serikali kusemea kashfa hiyo, wewe na iliyokuwa Kamati yako hamzuiwi. Mkinyamaza,mtasadifu ukweli wa jina la waongo na wazushi mlilopewa leo hii Dodoma.
Ukiwa nguli wa tasnia ya Sheria, Dr. Mwakyembe panga hoja zako nawe uzungumze na watanzania. Kama huna pesa ya kukodi ukumbi,waite waandishi hata nyumbani kwako. Watakuja na kukusikiliza. Muda wa kulinda heshima yako huu.Kama Lowassa kamwaga mboga, wewe Dr. Mwakyembe mwaga ugali.
Liwalo na liwe!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)