Dr. Mwakyembe: Marufuku TV na Radio kusoma habari za magazetini kwa ujumla wake

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
Waziri Mwakyembe apiga marufuku redio, televisheni kusoma habari nzima magazetini, badala yake kusoma vichwa vya habari tu.

Amevizuia kuanzia kesho vyombo vya habari (Tv na Redio) kusoma habari nzima kwenye magazeti, ili magazeti yapate soko.

======

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi.

Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana sawa.

Chanzo: Mwananchi
 
Waziri wa Habari Sanaa na Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amezuia kuanzia kesho vyombo vya habari vya Tv na Redio kusoma habari za kwenye magazeti kwa ujumla wake, na kuwataka kusoma vichwa vya habari pekee kulinda soko la magazeti.
 
Kwa sheria ipi anayoitumia kukataza hayo. This is ultra vires his powers! Mwakyembe should know that powers exercised by him are limited by the constituting or vesting instrument, and any act outside those limitations is ultra vires and may be challenged in the courts of law.
 
Waziri wa Habari Sanaa na Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amezuia kuanzia kesho vyombo vya habari vya Tv na Redio kusoma habari za kwenye magazeti kwa ujumla wake, na kuwataka kusoma vichwa vya habari pekee kulinda soko la magazeti.
Makonda alipiga marufuku movies za nje, ili kulinda Soko la Bongo movies.
Agghhhhh.......
Hii nchi bhana, yaani kila mwenye mamlaka akilala na kuamka, anafanya maamuzi yake tu
 
Habari wanaJF,

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe leo amepiga marufuku vituo vya Redio na Runinga nchini kusoma habari nzima magazetini, vyatakiwa kusoma vichwa vya habari tu.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo ili kulinda soko la magazeti nchini.
 
Back
Top Bottom