Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by domokaya, Feb 22, 2012.

 1. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,292
  Trophy Points: 280
  Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

  Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

  Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.


  Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

  Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

  Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

  Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

  Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

  Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda
   
 2. data

  data JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,799
  Likes Received: 6,579
  Trophy Points: 280
  Episode... 7,000,000
   
 3. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono, 80%, ila umesahau kuwa ana share kubwa sana katika kampuni fulani ya kufua umeme. Natumai itakuwa fundisho kwa wengine.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  mbona husemi hizo kebehi alizosema,hayo maneno machafu dhidi ya wananchi,..eti unayakumbuka maneno yote halafu huandiki hata neno moja,..hakuna point yoyote mpya uliyoandika hapo...tuambie alikebehi kwa maneno gani,.sio ili mradi kila mtu aandike kitu kuhusu mwakyembe...
   
 5. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  lowassa naye kabla jua halijazama atavuna alichokipanda!!!na mtakifaidi pamoja!
   
 6. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  watu bwana.. hujaona kabisa dr mwankyembe alichoifanyia tz.. tena naamini angeendelea kuwa mwalimu asinge fanya chochote kikubwa zaido ua kuifanyi akazi tu CCM kama huyo ndugu yenu Mkandara/Mukandara(rekebisha mwnyw).. yani we unawafagilia sana hao waalimu wenu wanaowafelisha na kuwalala wanafunzi ili wafaulu????

  tafuta huyo mwanasiasa unaemfikiria ambae angesoma ile report kama mwankyembe... MNATAKA MFANYIWE NINI???????
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  La maana kwa sasa ni kumuombea apone, wala si kumnenea maneno ya kifedhuli...Hata wakongwe wanasema Adui muombee Njaa, wala si KIFO au kuugua maradhi!
   
 8. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We utakuwa mjukuu wa BABU wa loliondo, au mtoto wa yahya husseni
   
 9. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,292
  Trophy Points: 280
  Nimefanya hivyo makusudi, watanzania tunajifanya tunapenda kusahau sana, wenye kumbukumbu na wenye hamu na ari ya kutaka uchambuzi wa kweli na si kufanya ushabiki watatafuta na kufahamu na katika kutafuta huko kutawafanya wamjue zaidi Dr Mwakyembe na kuwajua zaidi wanasiasa wengine wanafiki ambao hawana lengo lolote la kuwasaidia watanzania bali kuwatumia. Ukiwa makini utataka kujua zaidi kuliko kusubiri kuambiwa. Mangapi umeshaambiwa mengi na umeyasahau hapo hapo bila kuyafanyia kazi? Ukitafuta utakumbuka na utataka kujua zaidi.
   
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Mleta Thready hii unaonekana kama wewe ni mzushi tu! Nimeona neno NINAKUMBUKA umelirudia neno hili zaidi ya mara 5! sasa unakumbuka nini? mbona husemi hayo unayoyakumbuka ndugu?
   
 11. Sibonike

  Sibonike JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 10,294
  Likes Received: 5,016
  Trophy Points: 280
  Ajabu sana utakuwa umetumwa na mafisadi tu. Kuna hela nyingi zilitengwa kuwasafisha mafisadi kama bwama Manyama yeye kazi yake ni kumkosoa Sita, Mwakyembe na wengine na kumpamba mwenye mvi mwizi wa kutupwa. Anajjita mwalimu wa watu!
   
 12. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Umeandika yeye alizoea kuwapa sumu wengine,ni kina nani hao walopewa sumu?
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mtasema meeengi je njia mliyo tumia kumnyamazisha ni sahihi?
   
 14. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,292
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa letu ni kutokutaka kuona hata mtu mwingine anapotuonesha. Hatuwezi kufika kamwe, tukiendelea kushabikia watu wanaotufanya sisi wajinga, watu ambao wanaposhindwa ndipo wanakumbuka kuwa kuna wananchi. Lakini hao si wabaya kama wale ambayo wanajaribu kuharibu majadiliano yenye lengo la kutafuta jawabu kwa kupindisha hoja na kusema mambo ya hovyo hovyo na mepesi katika koja nzito na zenye kutaka tafakuri
   
 15. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  mmh, sawa sawa kabisa. Mwakyembe anakula alichokipanda!
   
 16. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Afadhali umenisaidia mkuu,thread ndeefu nimefuatilia mwanzo mpaka mwisho ni lawama tu dhidi ya Mwakyembe lakini sijaona mifano halisi ya matamshi na kebehi hizo alizotoa mwakyembe
   
 17. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Mwakyembe ni mnafiki sana yeye na rafiki yake sita, hivi kwanini alituficha baadhi ya mambo kwenye ile ripoti ya richmond . Ilikuwa ni kwa faida ya nani ? Aende kupata huruma kwa hao hao aliowaficha kwenye ripoti. Anavuna alichokipanda .

  Rosti-hamu huyo anafunga akaunti zake ana mwachia manyoya .
   
 18. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,292
  Trophy Points: 280
  Njia iliyotumika kumnyamazisha iwe sahihi au isiwe sahihi imetokana na mfumo ndani ya chamachetu na utaratibu ndani ya mtandao ambao yeye na wenzake waliubariki kabla ya kujua siku moja wangeasi baada ya kunyimwa uwaziri, mkuu, uspika na uwaziri katika kundi lililokosa kulipwa fadhila ndani ya mtandao. Angalau kuhasimiana kwao kumewafanya warudi kwa wananchi ingawa hiyo si dhamira yao na hili ndilo tatizo, hawana dhamira ya dhati hawa ila tu wanatufanya kimbilio wanapoona wanataka kunyongwa kama wao walivyowanyonga wenzao. Hawana jipya, hakuna haja ya kuwahurumia wala kuwategemea kutatua matatizo yetu.
   
 19. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,292
  Trophy Points: 280
  Aliyoyasema yapo, yaliandikwa kwenye magazeti na yalijibiwa na watu makini, kama wewe hukuwepo angalau basi upate nafasi ya kufanya utafiti, lakini kama moyo wako utaridhika kwa kusema mleta thread hii ni mzushi haya sitakuwa na la kukusaidia
   
 20. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  1. alitoa kebehi kwa taaluma yake..
  2. akagandamiza wananchi..
  3. mmoja wa watengenezaji wa mifumo michafu na ya kinyama..

  kwenye red mbona imekuwa tofauti..? so kosa kubwa la Dr. Mwakyembe ni kuingia kwenye chama na kujaribu kupambana (kwa mujibu wa andishi lako) dhidi ya hao mafisadi..? kwa hiyo kwako ww wale wote wanaonekana kutaka kupigania wanyonge wanastahili hili alilolipata Dr na hao wengine uliowataja..? ingekuwa vzuri kama ungejiweka wazi..

   
Loading...