Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda

Wewe ni tatizo na huhitajiki uwanjani na kauzi kako ka unakumbuka,unakumbuka,unakumbuka,sema watu wakuelewe,ama wewe ni tunda wa zile shule zetu zilizoanzishwa na kaka ENL kwa nguvu nyingi sana....aibu kwelkweli..Umechosha mkuu?
 
Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.


Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda

Hii ni kazi ya wataalaum walioko UWT.. nadhani ndiyo hawa walioshiriki kutilia sumu mwakyembe...
Hii ni kazi ya mtu aliebobea kupinduapindua maneno ili kuudanganya umma......!

Lakini jamani....mmesomeshwa ili kuisadia nchi, siyo kuja kuhongwa ovyo na mafisadi na kuwatumiki kuua adui zao!!! malaaniwe!
 
Naungana na wote ambao wanaona ni vema ungetueleza hayo unayokumbuka wewe. Kwenye bord hapo, unaona kweli umeonyesha kitu wewe domokaya? Siku zote yule ambaye anafanya utafiti au anatafuta kitu baada ya kukipata huwaeleza wenzake na sio kuwaambia na wao watafute. Kama hukua na haja ya kusema hayo unayokumbuka ni vema ungekaa kimya kuliko kutupotezea muda bure. Ungeendelea kukumbuka na hao wenzako. Sasa umetuonyesha nini?
 
Nimefanya hivyo makusudi, watanzania tunajifanya tunapenda kusahau sana, wenye kumbukumbu na wenye hamu na ari ya kutaka uchambuzi wa kweli na si kufanya ushabiki watatafuta na kufahamu na katika kutafuta huko kutawafanya wamjue zaidi Dr Mwakyembe na kuwajua zaidi wanasiasa wengine wanafiki ambao hawana lengo lolote la kuwasaidia watanzania bali kuwatumia. Ukiwa makini utataka kujua zaidi kuliko kusubiri kuambiwa. Mangapi umeshaambiwa mengi na umeyasahau hapo hapo bila kuyafanyia kazi? Ukitafuta utakumbuka na utataka kujua zaidi.

bado hujatoa maelezo aliyoyataka Nyabhingi....Mwakyembe alitamka maneno yapi? just tell us..... kama umeamua kuanzisha uzi huu then you should explain
 
watu bwana.. hujaona kabisa dr mwankyembe alichoifanyia tz.. tena naamini angeendelea kuwa mwalimu asinge fanya chochote kikubwa zaido ua kuifanyi akazi tu CCM kama huyo ndugu yenu Mkandara/Mukandara(rekebisha mwnyw).. yani we unawafagilia sana hao waalimu wenu wanaowafelisha na kuwalala wanafunzi ili wafaulu????

tafuta huyo mwanasiasa unaemfikiria ambae angesoma ile report kama mwankyembe... MNATAKA MFANYIWE NINI???????
Baada ya kusoma ripoti what next?
 
Hivi mvi nae huwa naingia humu JF na kutuma posts?
Sababu katika malalamiko yake huwa anapenda sana ku refer taaluma ya Dr.. Mwakyembe. Kipindi cha kuachia madaraka, aliwahi semakuwa Dr. ni mwalimu wa sheria pale mlimani na anafahamu na kufundisha kuhusu natural justice na hapa napo naona ma-mvi umerudia tena kuwa ametukana taaluma yake.
Vipi inakuwasha sana elimu yake nini? Mbona afya ya mvi inayozorota kwa kasi sasa hivi huiongelei?
 
Tanzania News Agency (SHIHATA)Journalist19781980
Information Services DivisionJounalist19771977
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position FromTo
Chama Cha Mapinduzi - CCMMember - National Executive Committee (NEC)20062010
Chama Cha Mapinduzi - CCMYouth Commander - Dar es Salaam20042009
Chama Cha Mapinduzi - CCMLaw Advisor20012005
 
Wewe std seven? Najua ni ticha kihiyo wa udsm haueleweki kabisa. Ebu rudia uone umeaddress nini kwenye post yako. Sisi regardless what as long as Dr. bado anaumwa priority ni kumuombea uzima mambo mengine na kama kuna jambo subiri apone um-face.
Kwni kuwa std seven ni dhambi? Ndio mimi ni std seven nina haki na maoni yangu na naweza kuwa na kumbukumbu nzuri kuliko wewe ukitilia maanani nilisoma enzi hizo ambao ufaulu ulikuwa kwa qouta system, sitashangaa ukiniuliza quota system ni nini
 
bado hujatoa maelezo aliyoyataka Nyabhingi....Mwakyembe alitamka maneno yapi? just tell us..... kama umeamua kuanzisha uzi huu then you should explain
I should explain?! Wow kweli nimefurahi kuona watu wanaojiita wana upeo mzuri kuandika mawazo yenye vituko na kuonesha ushabiki badala ya kujadili hoja. Juma Mwapachu katika kitabu chake kimoja amewahi kuandika kuwa watanzania wale wtu tunaodhani na kufikiri ni Think Tanks wa nchi hii nao ni vilaza wakubwa kwani utakuta mtu kapaki magari manne ndani ya ua wale yenye thamani zaidi ya milioni mia moja yeye anatumia gari la tano wakati kumbe angeanzisha kiwanda kidogo angaajiri watu na angekuwa anaingiza pesa nyingi huku akisaidia tatizo la ajira nchini. Sishangai mawazo ya mnaojiita wasomi wa nchi hii
 
hivi dr. Mwakyembe ni threat kwa El or Jk? Na kwa nn iwe dr tu siyo kamati nzima ya dowans au wengine hawajui mengine ni dr pekee anajua? Mi ninavyojua kamati nzima ndiyo iliamua kuficha baadhi ya mambo kuikoa serikali.
 
Naungana na wote ambao wanaona ni vema ungetueleza hayo unayokumbuka wewe. Kwenye bord hapo, unaona kweli umeonyesha kitu wewe domokaya? Siku zote yule ambaye anafanya utafiti au anatafuta kitu baada ya kukipata huwaeleza wenzake na sio kuwaambia na wao watafute. Kama hukua na haja ya kusema hayo unayokumbuka ni vema ungekaa kimya kuliko kutupotezea muda bure. Ungeendelea kukumbuka na hao wenzako. Sasa umetuonyesha nini?
Siku zote! Wewe ni msomi kwelikweli na una kanuni ambayo haibadiliki kuhusu utafiti. Nimeipenda hiyo lakini mara hii ya kwangu ambayo si ya kisomi haipo katika siku zote. Natamani ningekuwa najua elimu ya utafiti kama wewe labda nisingefanya makos a haya ya kuibua hamu ya kukukmbuka aliyoyafanya Dr Mwakyembe wakati akitafuta ubunge wa Afrika Mashariki
 
Domokaya ana point muhimu sana ila labda tu kaileta kwa style ambayo inagusa sana hisia za binadamu.

Wazungu ni watu ambao akisema hakupendi, basi hakupendi kweli na hafichi na akisema anakupenda basi anakupenda hasa. Kuna Waafrika na mataifa mengine duniani, baadhi ya watu wake wanakuwa pia na tabia hii. Hata hapa kwetu JF, Mzee FMes ni mtu ambaye kama anakufahamu, atakwenda na wewe motoni na ukimuudhi atakupa maneno moja kwa moja bila kuuma.

Wengine huwa wanamchukia kwa hilo na wengine wanampenda. Wengi tunakumbuka ugomvi wa Malecela family na Sophia Simba ulivyoishia kutoleana maneno makali na siri kali za kifamilia.

Mwakyembe upande mmoja kama binadamu, anatia huruma sana ukimuona jinsi alivyo sasa. Mie mwanzo nilijua ni zile danganya zake za kawaida na haumwi kihivyo. Nilipomuona na ile kofia, niliishiwa nguvu na ndipo u-Tomasi wangu ukaisha na kuamini kweli jamaa anaumwa na anaumwa haswa hadi anatia huruma.

Ila maneno ya Domokaya kwa upande mwingine yana ukweli. Ukisoma maneno ya Jenifa hapa chini, anagusia kwa mbaali hayo maneno. Watanzania tuache uvivu wa kusoma na kuwa na kumbukumbu fupi. Tafuteni maneno ya Mwakyembe wakati wa Mkapa na mjiulize kwa nini Wazenji hasa Pemba hawampendi Mkapa na Mwakyembe. Mkiyapata basi mtajua nini Domokaya anaongelea.

Mie binafsi, upande mmoja nakubaliana na Domokaya ila upande mwingine namhurumia Mwakyembe. Mixed feeling.
greatsinkers wa jf hawajui ile tume ya mwakiembe kuhusu mauaji ya pemba ilisema nini.

asante ya ccm ikawa kumpa kura nyingi ubunge afrikamashariki.

shule za kata ni ukimwi wa taifa. sisi tuliosoma shule zenye mshiko tunajua mambo bana.
 
hivi dr. Mwakyembe ni threat kwa El or Jk? Na kwa nn iwe dr tu siyo kamati nzima ya dowans au wengine hawajui mengine ni dr pekee anajua? Mi ninavyojua kamati nzima ndiyo iliamua kuficha baadhi ya mambo kuikoa serikali.
Kamati nzima iliamua kuwaficha mafisadi wenzao. Dr nae akiwa mmojawapo. Kanuni ambayo haiko wazi ndani ya CCM ni hii kama unaujua ukweli na unataka kuishi ni bora uuseme ingawa maisha yako yatakuwa ya taabu, walau utaendelea kuishi. Ukiujua ukweli ndani ya chama halafu ukasema iko siku utausema au unataka kuusema baadae " Costra Nostra" inafanya vitu vyake, unanyamazishwa! Dr hakulijua hilo? Hakuliona kwa Kolimba, Malima na Amina?

Kama Dr aliikoa serikali basi hakuwa upande wa wananchi na kamwe hawezi kuwa labda aambiwe amebakiza mwezi kuishi ndipo hapo ataona hana cha kupoteza lakini bila hivyo roho ya ufisadi aliyonayo itaendelea kuwaka na atahitaji mali zaidi na umaarufu zaidi
 
I should explain?! Wow kweli nimefurahi kuona watu wanaojiita wana upeo mzuri kuandika mawazo yenye vituko na kuonesha ushabiki badala ya kujadili hoja. Juma Mwapachu katika kitabu chake kimoja amewahi kuandika kuwa watanzania wale wtu tunaodhani na kufikiri ni Think Tanks wa nchi hii nao ni vilaza wakubwa kwani utakuta mtu kapaki magari manne ndani ya ua wale yenye thamani zaidi ya milioni mia moja yeye anatumia gari la tano wakati kumbe angeanzisha kiwanda kidogo angaajiri watu na angekuwa anaingiza pesa nyingi huku akisaidia tatizo la ajira nchini. Sishangai mawazo ya mnaojiita wasomi wa nchi hii

ushabiki katika post yangu uko wapi??? :embarassed2: mimi sikufunzwa kukashifu kama ulichokifanya kwenye red ila nimefunzwa kureason.
You have to explain kwa kuwa title ya thread yako imetaka Mwakyembe asihurumiwe....so you have to explain more ili tuone sababu za kutomwonea Mwakyembe huruma
 
Mkuu leo umenifumbua macho,hii ndio raha ya JF,halafu anatokea mbunge mmoja mwenye matatizo ya akili anasema JF ifungiwe,pumbavu zao.Mkuu sitamtetea wala kumuonea huruma huyu mtu tena,kwa hakika auaye kwa upange na yeye atauwawa kwa upanga..well said mkuu!!
 
Hii ni kazi ya wataalaum walioko UWT.. nadhani ndiyo hawa walioshiriki kutilia sumu mwakyembe...
Hii ni kazi ya mtu aliebobea kupinduapindua maneno ili kuudanganya umma......!

Lakini jamani....mmesomeshwa ili kuisadia nchi, siyo kuja kuhongwa ovyo na mafisadi na kuwatumiki kuua adui zao!!! malaaniwe!

Siku hizi kila mtu aneyemkosoa wanaojiita 'makamanda wa ufisadi' anakuwa amehongwa na mafisadi. "Makamanda wa mafisadi" hata wakitaka wakuu wa wilaya wawe katika mamlaka ya kuamua kuhusu katiba ukimkosoa wewe fisadi. Nawauliza tena je mnajua kitu gani kiliwafanya hawa makamanda hadi wakaamua kujifanya kuwa makamanda. Je unajua ishu ya Jeetu Patel kutoa pesa kwa moja wa makamanda wa ufisadi na baadae hizo pesa kuchukuliwa na huyo kamanda na mume wake wakabaki hawana kitu? Walimjua laiyechukua pesa ndo maana mpaka leo wana bifu nae.Hawawezi ku deal nae moja kwa moja sasa wanatumia wananchi wanyonge kukidhi haja zao. Wote ni mafisadi tu, hilo ndilo walilo nalo mioyoni mwao, hawana lolote la kuleta mabadiliko.
 
Siku hizi kila mtu aneyemkosoa wanaojiita 'makamanda wa ufisadi' anakuwa amehongwa na mafisadi. "Makamanda wa mafisadi" hata wakitaka wakuu wa wilaya wawe katika mamlaka ya kuamua kuhusu katiba ukimkosoa wewe fisadi. Nawauliza tena je mnajua kitu gani kiliwafanya hawa makamanda hadi wakaamua kujifanya kuwa makamanda. Je unajua ishu ya Jeetu Patel kutoa pesa kwa moja wa makamanda wa ufisadi na baadae hizo pesa kuchukuliwa na huyo kamanda na mume wake wakabaki hawana kitu? Walimjua laiyechukua pesa ndo maana mpaka leo wana bifu nae.Hawawezi ku deal nae moja kwa moja sasa wanatumia wananchi wanyonge kukidhi haja zao. Wote ni mafisadi tu, hilo ndilo walilo nalo mioyoni mwao, hawana lolote la kuleta mabadiliko.
nadhani ndio maana wakiambiwa waende upinzani wanakaa kimya.kweli ccm=chama cha maslahi.
 
ushabiki katika post yangu uko wapi??? :embarassed2: mimi sikufunzwa kukashifu kama ulichokifanya kwenye red ila nimefunzwa kureason.
You have to explain kwa kuwa title ya thread yako imetaka Mwakyembe asihurumiwe....so you have to explain more ili tuone sababu za kutomwonea Mwakyembe huruma
Nimetaka Dr asihurumiwe kwa sababu yeye ni mshiriki wa moja kwa moja katika kufanya hayo waliyomfanyia. Alishirikiana nao, alikula nao sasa alipotaka kwenda kinyume walimshughulikia kama yeye alivyoshiriki kuwashughulikia wengine. Ameshiriki katika mengi, mengi yakiwa kuwafanya watanzania waishi maisha magumu. Je ni watanzania wangapi wanaoumwa zaidi ya Dr, jE hao wamepelekwa Appolo na kurudi? Dr ana thamani gani zaidi ya watanzania hao? Je kuna mtanzania bora zaidi ya mwingine? Je wewe unaiona Tanzania hii inastahili uwa hapa ilipo pamoja na utajiri uliopo? Hivi Prof Shivji angeamua kuungana na mafisadi hawa Tanzania leo ingepat mtetezi wapi? Huyu Dr hakuwa pamoja na Prof Shivji. Hivi Shivji na huyu Mwakyembe katika mizania yako ni nani mtetezi bora wa wananchi kiliko mwingine? Tafadhali ndugu yangu pambanua!
 
Njia iliyotumika kumnyamazisha iwe sahihi au isiwe sahihi imetokana na mfumo ndani ya chamachetu na utaratibu ndani ya mtandao ambao yeye na wenzake waliubariki kabla ya kujua siku moja wangeasi baada ya kunyimwa uwaziri, mkuu, uspika na uwaziri katika kundi lililokosa kulipwa fadhila ndani ya mtandao. Angalau kuhasimiana kwao kumewafanya warudi kwa wananchi ingawa hiyo si dhamira yao na hili ndilo tatizo, hawana dhamira ya dhati hawa ila tu wanatufanya kimbilio wanapoona wanataka kunyongwa kama wao walivyowanyonga wenzao. Hawana jipya, hakuna haja ya kuwahurumia wala kuwategemea kutatua matatizo yetu.
Nimekusoma vizuri mkuu, angalau sasa hivi nahisi kunakitu kinaingia akilini. Siwezi kushangaa wala kusita kusema kwamba Mwakyembe nae pia alikuwa ni sehemu ya hao wabaya wake, na ndio maana katika ripoti ya Richmond alificha mambo fulani (kama inavyosemekana) ili kuwakinga. Inawezekana kuna jambo ambalo lilikuja kumgonganisha Mwakyembe na hao wenzake, jambo ambalo yeye, Dr, anashindwa kuliweka wazi, na ndio kinacho m-gharimu sasa Mwakyembe, kwa maana kwa kufanya hivyo atakua ameuthibitishia uma kwamba kumbe hata yeye pia yumo ndani ya mtandao wa mafisadi, na ndio maana Mwakyembe na hata mzee Sitta wanaonyesha kuwa na uhakika, na ushahidi juu ya mpango wa kuwekewa sumu kwa Mwakyembe.
 
Domokaya,

Amedhubutu kusema kile ambacho wengi wanaogopa kusema kutokana na hali Dr. Mwakyembe kwa sasa. Mimi namwone huruma Dr. Mwakyembe kutokana na matatizo yake afya na nazidi kumwombea apate nafuu haraka; HOWEVER, namlaumu kutokana na kitendo chake cha kujiingiza kwenye mtego wa mafisadi. Kwa wale waliosikiliza ile hotuba aliyoitoa kwa niaba yake ya tume kuna kipindi alisema," kuna mengi hatuwezi kuyasema kutokana na kulinda usalama wa nchi." Badala ya kusema hivyo tuu nikajua ya kuwa yeye na hao mafisadi anaowalaumu tofauti yao ni MAJINA tuu.

Tume ya Mwakyembe ilipoteza sifa baada ya maeno hayo kwani kwa wale ambao tunaosoma katikati ya mistari tuliona ya kuwa hatetei maslahi ya nchi bali ya mafisadi. Kitu kingine ambacho kilionyesha dhahiri ya kuwa huyu bwana ni oppurtunistic ni pale alipotetea posho anayolipwa na mashirika waliyokuwa wakiyakagua na wakati huo huo wakilipwa na tume ya Bunge. Kusema ukweli jambo hilo alihitaji mtu kuwa mwanasheria kuona ni jinsi gani mgogoro wa kimaslahi "conflict of interest" ulivyo wazi wazi.

Ni muhimu kwa sisi watanzania kuacha tabia ya kinafiki na kuzungumza ukweli. Namwonea huruma kama Mwanadamu, lakini najua ya kuwa Dr. Mwakyembe alijua ya CCM ni ya mafisadi na mafisadi siku zote wanaamini ya kuwa the ends justify the means. Nadhani ili liwe fundisho kwa wale wote wanaotaka kuukumbatia mfumo huu wa kifisadi.
 
Back
Top Bottom