FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
Kauli ya kuwa Mwakyembe amevuna alichopanda ...inahitaji tafakuri ..kuweza kumuelewa mleta hoja.........,kwa wale wanaojuwa sheria za kijasusi .."...wanajuwa there is always a price to pay when you agree to be used ...".....
Ukiangalia historia ya mwakyembe ..siku zote amejitambulisha ...kama mzalendo na hatuna shaka juu ya hilo...hata mtakumbuka alipokuwa mjumbe wa bodi ya NBC alipata kujitoa kupinga mambo yaliyokuwa yanafanyika kinyume.....
Kosa kubwa alilofanya Mwakyembe kwenye sakata la tume yake ...ni kukubali kutumika na kikwete kwa kujuwa au kutokujuwa.....,mkikumbuka kwenye ripoti yake aliyosema hili pia alilitaja.."baadhi ya mambo kwenye ripoti yangu sintayasoma yote " ......kimsingi aliichuja ripoti yake ili kuepuka kumu implicate rais na amiri jeshi mkuu..........hili kwa upande mwingine lilikuwa jambo jema kwa usalama wa nchi...lakini kitendo cha kwenda hewani kuwa kuna mambo ameyaficha ..kinaweza kuwa lilitafsiriwa na Jk na wenzake ...kuwa mbeleni mwakyembe angeweza kuwajeuka na kuwafanyia blackmail.........
Kitu cha kwanza rais kufanya kilikuwa kumuweka Mwakyembe karibu naye ili asije akamgeuka......[kumbukeni uhusiano wa mwakyembe na serikali kabla ya ile tume haukuwa mzuri sana.alikuwa mpinzani mkubwa]........
Tume ya mwakyembe ilimfanya akawa na maadui wa aina mbili ...
ADUI wa kwanza kundi la Lowassa..ambao wanaamini kuwa Mwakyembe tume yake ilitumika kumuuwa Lowassa kisiasa.....
ADUI Wa pili akawa ni Kikwete mwenyewe ambaye pamoja na kumchekea kote na kumuingiza mwakyembe na makamu wake engineer manyanya stella serikalini....hajapata kuamini kuwa mwakyembe angekaa na siri yote hii kwa muda gani....na ilikuwa lazima amfanyie monitoring..........lakini mnajuwa ..what deserve a hostile ....."agent"...!...
Sasa katika makundi mawilli adui wa mwakyembe ..moja adui wa wazi[lowassa]....mmoja adui wa kijino pembe"kikwete"....Tunabaki na swali la yupi aliyekuwa na access ya kumdhuru mwakyembe ..kupitia...taulo na sabuni ndani ya ofisi yake....................na kwa walio uona waraka wajiulize waliotumwa kufanya hivyo ni kina nani na wako wapi....?..kama kweli wapo
Tulikua tunarusha mawe ya kweli kama haya enzi hizo. Ila kwa sasa ukirusha uchambuzi kama huu basi utaanza kuambiwa we ni fisadi au umenunuliwa! Watoto wamejaa sana humu! Hawana hata uchungu na nchi na magazeti yanatumika kufikiria badala ya wao kutumia bongo zao kufikiri