Dr. Mwakyembe aliwahi kuwa TBS?

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,006
3,669
Samahani wakuu, Jee Dr. Mwakyembe aliwahi kuwa TBS? au nimechanganya majina.

Naomba mnielimishe.
 
MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,143
707
Ni watu tofauti- huenda ni ndugu wa ukoo!

Yule wa TBS alikaa pale kama miaka 25 wakati Harison alikuwa Mwalimu wa Sheria UD
 
MMASAI

Member
Feb 9, 2008
28
0
Aliyekuwa TBS chief ambaye ame retire anaitwa Daimon Mwakyembe na huyu jamaa mtetea haki anaitwa Harrison Mwakyembe
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,006
3,669
Ahsanteni wote mliochangia kunijibu, nimeelimika nashkuru.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,531
9,646
Samahani wakuu, Jee Dr. Mwakyembe aliwahi kuwa TBS? au nimechanganya majina.

Naomba mnielimishe.

Ni watu tofauti, ila nahisi ni ndugu.
Daimon Mwakyembe wa TBS kitaaluma ni Mkemia, wakati huyu Harrison Mwakyembe Mbunge ni Mwanasheria.
 
Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
8,065
1,712
Aidha ni ndugu wa Damu, Ukoo wao umepanuka toka Kyela hadi Zanzibar na kuishia Bukoba.
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
630
Ni watu tofauti, ila nahisi ni ndugu.
Daimon Mwakyembe wa TBS kitaaluma ni Mkemia, wakati huyu Harrison Mwakyembe Mbunge ni Mwanasheria.

Wote wanatoka Kyela lakini sio ndugu. Ni majina tu yanafanana.
 
G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
13
Daimon na Harrison ninavyowafahamu ni mtu na mdogo wake meaning Daimoni ni mkubwa na Harrison ni mdogo wote wakiwa wanatokea Mbeya,wilaya ya kyela kijiji cha Ikolo.
 
RR

JF-Expert Member
Mar 17, 2007
6,934
1,953
Wote wanatoka Kyela lakini sio ndugu. Ni majina tu yanafanana.

Daimon na Harrison ninavyowafahamu ni mtu na mdogo wake meaning Daimoni ni mkubwa na Harrison ni mdogo wote wakiwa wanatokea Mbeya,wilaya ya kyela kijiji cha Ikolo.

Waungwana Mtanzania na G.Mwakasege ni yupi kati yenu ni sahihi? Kuna mwanaJF mwingine mwenye data zaidi?
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,006
3,669
Sabau kubwa ya kuuliza swali hilo, ilikuwa ni kutaka kujuwa kama ni mtu huyo huyo au la, baada ya kupata majibu kutoka kwa wachangiaji tofauti, nimeridhika na nimeona kuwa hawa ni ndugu, iwe wa tumbo moja, au wa ukoo, au wa kutoka kijiji kimoja, kwa kifupi, kwa njia moja au nyengine wanahusiana.

Kilicho nisababisha niulize hivyo ni kuwa, niliwahi kusikiya kuwa Dr. Mwakyembe (wa TBS) anahusika na ufisadi wa kumpa mfanya-biashara mmoja wa Dubai, UAE biashara ya kukaguwa magari yanayotarajiwa kuletwa Tanzania, kwa misingi ya utatanishi, nikimaanisha yana ka-harufu harufu cha ufisadi.

Kwa kuwa si yeye, sina haja ya kumlaumu kwa kosa la nduguye. Ni hilo tu. Nashukuru kwa wote waliochangia majibu.
 
MaMkwe

JF-Expert Member
Sep 5, 2007
284
21
Aliyekuwa TBS chief ambaye ame retire anaitwa Daimon Mwakyembe na huyu jamaa mtetea haki anaitwa Harrison Mwakyembe

Sidhani kama ni mtetea haki na shujaa kama wengi wanavyodai. Yeye alitumwa kazi na Bunge na ameifanya, ametimiza wajibu wake. Anayestahili sifa ya kutetea haki ni Zitto Kabwe na Silaa walojitoa kafara kuibua masuala ya ufisadi bungeni.
 
green29

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
311
40
Waungwana Mtanzania na G.Mwakasege ni yupi kati yenu ni sahihi? Kuna mwanaJF mwingine mwenye data zaidi?
Hilo chata la MWAKASEGE linanifanya niamini hoja yake. But caution, huko vijijini tukitembelea ndugu zetu (hasa babu na bibi) utakuta kila mwanakijiji mnaekutana nae unatambulishwa ni ndugu yetu! Logic niliyoipata kwa Mwakasege ni kuwa hawa jamaa ni ndug sababu wanatoka kijiji kimoja. Ila kwa hawa Mwakyembes naona mpaka majina yanafanana.

Solution: DNA Test

ndaga fijo
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom