Utitiri wa viwanda vya bati Tanzania na paa za nyumba zenye bati mijini kuwa na kutu ni Udhaifu mkubwa uliopo TBS

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,038
1,154
Miji mingi Tanzania inakabiliwa na kupoteza ubora,nyumba nyingi zinaonekana kuchakaa hususani paa za nyumba nyingi kuonekana kuwa na kutu. Yawezekana ni bati kutokuwa na bati nyingi kukosa ubora licha ya hapa nchini Kuna taasisi ya umma inayoshughulika na ubora wa bidhaa.

Utitiri wa viwanda vya bati umeleta changamoto lukuki Kwa TBS kiasi Cha kushindwa kutambua uwezo wa bati kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa. Kiuhalisia mwanzo wa kufuatilia ubora wa bidhaa Kwa TBS huwa mwanzoni tu,ukishapata cheti Cha ubora, TBS huwa hawana muda wa kufuatilia,hapo ndipo viwanda huanza kuchakachua.

Tatizo lingine TBS wameshindwa kudhibiti ubora wa rangi kwenye mabati,bati zimekuwa zikipauka mapema tangu kupauliwa, siku hiz bati hupauka kuanzia mwezi mmoja Hadi sita tangu kupauliwa.

TBS inatakiwa kujitathimini, wengi wamejaa wafanyakazi wenye uwezo mdogo,connection zinaiharibu hii nchi.
 
Nasikia watu wananunua zao mashine za kukunja mgongo wa bati then wanaanza zao kuzalisha tu kirahisi. Kuna mdau alinipa hiyo story kijiweni , akinishauri na mm nikanunue mashine za kukunja mabati huko china
 
Mabati ya kipimo (gauge) cha 32 ambayo tunaambiwa ni kwa ajili ya uzio na mabanda hayapati kutu hata kama ni miaka 10 wakati yale ya kilimo cha 30, 28, 26 yanapata kutu muda mfupi baada ya kuezekwa.

Yanaweza hata kupata kutu yakiwa yamehifadhiwa ndani.
 
Mabati ya kipimo (gauge) cha 32 ambayo tunaambiwa ni kwa ajili ya uzio na mabanda hayapati kutu hata kama ni miaka 10 wakati yale ya kilimo cha 30, 28, 26 yanapata kutu muda mfupi baada ya kuezekwa.

Yanaweza hata kupata kutu yakiwa yamehifadhiwa ndani.
Ukiona bati linapata kutu muda mfupi baada ya kupaua jua hayo ni reject.nakumbuka mwaka juzi nilinunua bati toka mahali fulani nikapaua.
Baadabya wiki toka nipaue mvua ikanyesha ikaondoka na rangi za bati !
Niliwatokea warudishe pesa yangu au nawaharibia mazima sihitaji tena bati zao.

Kwa hali na hasira nilizo enda nazo jamaa aliiva mwekunduu anaomba radhi mara mia mia.

Mwisho nilirudishiwa pesa yangu na fidia.

Nikaenda zangu ALAF penye bati za uhakika.
aka "ALIEZEKEA BABU HADI MJUKUU ANAISHI BILA KUVUJIWA"
 
Tatizo lipo kwa watu wa srk ndomana Kuna lundo la Viwanda Vinavyozalisha Bidhaa Fake, na pia Hawa watu wa srk wanapata 10% na Kila wakienda kufanya ukaguzi wanachukua Posho.
Swala la Bati Kibongo Bongo Mabati watu Wengi tunateseka kwa kuuziwa Mabati yasio na Ubora. Kwa Lundo la Viwanda.
 
Back
Top Bottom