Dr. Mwakyembe akwama uwanja wa ndege baada ya Fastjet kuahirisha safari

mambo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
2,374
2,000
Tanzania ya Viwanda ninayoitaka ndio hii sasa.Kuna siku siku nilikuwa nasafiri ndege moja na Abdallah Posi ... tulikwama pia mpaka kesho yake tehe tehe ni kawaida....
 

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,905
2,000
Si chadema wanasema watu hawana hela ya kusafiri na ndege??

Je waliorundikana hapo ni akina nani??


Ndio maana Magufuli amenunua ndege mbili na kuagiza zingine mbili ili kukabiliana na changamoto hii.

Magufuli ana akili sana na anaona mbali
 

MSIMISEKI SENIOR

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
459
250
Ingekuwa ATCL yangeporomoshwa matusi hapa. Nakumbuka kuna mdau alileta uzi hapa akilalamika ATCL kuwakarisha KIA zaidi ya saa 2 eti wanasubiri bodi ya NSSF. Comments zilikuwa za matusi. Lakini hii iliyotokea sababu siyo ATCL inaonekana siyo issue
 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,706
2,000
image.jpeg
Kuna tatizo la "delay" kwa ndege za Fastjet toka jana asubuhi.Ndege ya fastjet ya jana asubuhi iliyokuwa inapaswa kuondoka kwa Flight # FN121 5H-FJD ilipata "bird strike" wakati wa "take off",kiasi kilichozusha taraharuki na abiria kupatwa na mshituko mkubwa.Kupatwa kwa "Bird strike" kulisababisha uharibifu ktk injini ya ndege na hivyo ndege kurudi na kuhairisha safari ya asubuhi ya kwenda Mbeya.

Hivyo wale abiria waliopaswa kuondoka kwenda Mbeya hawakuweza kuondoka asubuhi,na wale waliopaswa kuja Dsm toka Mbeya na FN122 wamebaki Mbeya.Hivyo abiria waliopo sasa hapo Songwe ni wale wa asubuhi na wale wa mchana huu ambao walitakiwa kuja na Fastjet Flight no FN124 inayofika Dsm jioni.

Na kwa sbb Fastjet wana ndege mbili tu kwa sasa,hawawezi kuzipeleka Mbeya jioni hii zote mbili,halafu wafute safari za Mwanza na KIA kwa jioni hii.Hili ndio tatizo linalofanya mkundikano wa abiria hapo Songwe.

Bahati mbaya Fastjet inayopaswa kwenda Mbeya haiwezi kubeba abiria wote kwa pamoja,yaani wale wa Asubuhi na wale wa jioni.
Kwa mantiki hiyo,kuna mlundikano wa abiria wa Fastjet kwa Dsm na Mbeya kwa kiasi kikubwa.

Daktari wa sheria kama Mwakyembe alitakiwa apitie hata website tu ya Fastjet,wali-update tatizo hili la "delay" ya ndege zao toka jana jioni.Halafu hivi hawajui kuwa Fastjet ni "Low Cost Airline?".Unataka upelekwe Hotelini na upewe na chakula wakati umetaka vya "dezo" kwa kukata tiketi ya Mbeya kwa ndege laki moja na nusu??

Tatizo ni "bird strike",ni nje ya uwezo wa Fastjet,hapo Mwakyembe kama waziri wa zamani wa Uchukuzi anatakiwa kujiuliza,je aliboresha kitengo cha "Bird Hazards" pale JNIA ili kiwezs kukabiliana na ndege wanyama nyakati hizi za mvua?Maana anaweza kuwa wanawalaumu Fastjet,kumbe deep inside;yeye ndio wakulaumiwa...Afrika bana!!kila siku jambo jipya la ajabu linazaliwa.

Note:Suala la "bird strike" katika msimu huu wa mvua ni kubwa sana,sbb ndege wanyama hujaa uwanjani kwa wingi kufuata wadudu wanaozagaa kutokana na mvua kama vile kumbikumbi.Bird Strike ni ile hali ya Ndege mnyama kumezwa ndani ya injini ya ndege,hasa zile aina ya "jet engine",ikitokea suala hili,ndege haiwezi kuendelea na safari tena..na ikiwa serious wakati mwingine hata moto huwaka ktk injini.Hizi ni habari toka kwa chanzo changu hapo JNIA.
 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,706
2,000
Si chadema wanasema watu hawana hela ya kusafiri na ndege??

Je waliorundikana hapo ni akina nani??


Ndio maana Magufuli amenunua ndege mbili na kuagiza zingine mbili ili kukabiliana na changamoto hii.

Magufuli ana akili sana na anaona mbali
Huu ndio mwisho wako wa kujenga hoja?
 

Arie power

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
2,553
2,000
Alikuwa anaenda wapi , kwanini hakupanda ndege yetu pendwa bombardier, acha akwame kayataka mwenyewe hao fastjet siku hizi wamezidiwa.
 

Fundisi Muhapa

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
4,423
2,000
Si chadema wanasema watu hawana hela ya kusafiri na ndege??

Je waliorundikana hapo ni akina nani??


Ndio maana Magufuli amenunua ndege mbili na kuagiza zingine mbili ili kukabiliana na changamoto hii.

Magufuli ana akili sana na anaona mbali
Madawati na madawa ndo angekua anaona mbali
 

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,081
2,000
Nimefikiria amekwama kwenye tope kumbe ni mambo ya safari !!!!!

Afu hii habari ya Kisengenyaji sana na umbea juu.
 

Fundisi Muhapa

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
4,423
2,000
Ingekuwa ATCL yangeporomoshwa matusi hapa. Nakumbuka kuna mdau alileta uzi hapa akilalamika ATCL kuwakarisha KIA zaidi ya saa 2 eti wanasubiri bodi ya NSSF. Comments zilikuwa za matusi. Lakini hii iliyotokea sababu siyo ATCL inaonekana siyo issue
Kwasababu ndege zilinunuliwa taslimu huku hakuna dawa hosp
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom