Dr. Mwaka, tunaomba majibu hapa tafadhali

Dr. Mwaka, tunaomba majibu hapa tafadhali

Mie ni mhanga wa madawa yake fake huyu mganga njaa,nimeacha Tsh180,000/= zangu pale kwenye ka-clinic kake uchwara pale Ilala Bungoni na kuninywesha madawa yake machungu zaidi ya siki yasiyoonyesha yalikotengenezwa..miezi mitatu nakunywa dawa hata nafuu hamna..
 
Movie inaendelea
 
Attachments

  • 1450294591683.jpg
    1450294591683.jpg
    24 KB · Views: 832
Muoneeni huruma wakuu mana shule tatizo pale, ila kama kweli anatibu na watu wanapona sio vibaya serikali kuangalia namna ya kumsahuri afanya kazi zake kwa usahihi bila ujanjaujanja

Nina mtu wa karibu alifanikiwa kupata mtoto kwa tiba ya (Dr.) Mwaka
 
Mie ni mhanga wa madawa yake fake huyu mganga njaa,nimeacha Tsh180,000/= zangu pale kwenye ka-clinic kake uchwara pale Ilala Bungoni na kuninywesha madawa yake machungu zaidi siki yasiyoonyesha yalikotengenezwa..miezi mitatu nakunywa dawa hata nafuu hamna..

pole sana.... sasa usidanganywe tena
 
ISLETS unajua mtu ukiumwa unaweweseka...hii hali ilinitokea nikawa namwanini kila niliyesikia ana dawa kasoro witchdoctor tu,maumivu makali na vitu kama hivyo ndo mana Mwaka alinikamata..ila namshukuru Mungu nilijapona kwa Tsh4,000/= kwa dawa hizi hizi za kienyeji.Mwaka anaharibu sifa za wauza dawa za kienyeji kwa utapeli wake.
 
Last edited by a moderator:
Kitendo cha yeye kumkimbia kiongozi wa nchi ambaye ana dhamana ya afya za WATANZANIA.....ni tukio la aibu kwa mtu aliyejozolea sifa na umaarufu kama yeye kutokana na matokeo ya kazi zake......ni kitendo kinachomfanya kila mwenye akili timamu kufikiria mara mbili mbili kuwa kama walikuwa sahihi kufuata tiba kwake......
Tukio la kutembelewa na waziri au hata naibu waziri ni ambacho kingemuongezea umaarufu na sifa maradufu miongoni mwa jamii ya walalahoi......hata wale waliokuwa na shaka naye kuhusu tiba zake....wataanza kuwa na imani nae....
 
Shida kweli kweli , kama nawaona wakina Mbwiga na Shafii wanavyonuna ujio wa Kigwangala.Mwaka ujao no ndondo cup.
 
ISLETS unajua mtu ukiumwa unaweweseka...hii hali ilinitokea nikawa namwanini kila niliyesikia ana dawa kasoro witchdoctor tu,maumivu makali na vitu kama hivyo ndo mana Mwaka alinikamata..ila namshukuru Mungu nilijapona kwa Tsh4,000/= kwa dawa hizi hizi za kienyeji.Mwaka anaharibu sifa za wauza dawa za kienyeji kwa utapeli wake.

nikweli usemacho, mtu ukiumwa kila ushauri unausikiliza.
Mwaka kanisikitisha sana.
Uwe na mazoea wa kuonana na wataalamu madaktari bingwa ikiwa unatatizo serious, hawa kinaMwaka nchi hii wapo wengi sana kila kona kuna Herbal clinic sasa inabidi serikali ifanye kweli
 
Surely mkuu..hili nalo neno.
 
kuna dawa ya hospitali inaitwa clomifene inasaidia utoaji wa yai kwa mwanamke. kuna uwezekano mkubwa mwaka alikuwa anachanganyia wagonjwa wake.

Laah sikutegemea hayo kwa (Dr.) Mwaka,
 
kuna dawa ya hospitali inaitwa clomifene inasaidia utoaji wa yai kwa mwanamke. kuna uwezekano mkubwa mwaka alikuwa anachanganyia wagonjwa wake.

Duh! Hiyo dawa ni ya asili pia?
 
Serikali iwekeze ktk Afya ili kuepuka Matapeli. Lakini pia tusipuuze tiba m'badala, kwani upo ushahidi ktk baadhi ya maradhi imeonyesha mafanikio.
Mfano mdogo ni upande wa uungaji mifupa, tiba asili imekuwa ikiwasaidia wengi. Muhimu ni kupitia upya utaratibu mzima wa tiba hii Asilia. Serikali itoe Elimu kwa watoaji huduma hii na kuweka muongozo ili kuepusha madhara.
 
Kitendo cha yeye kumkimbia kiongozi wa nchi ambaye ana dhamana ya afya za WATANZANIA.....ni tukio la aibu kwa mtu aliyejozolea sifa na umaarufu kama yeye kutokana na matokeo ya kazi zake......ni kitendo kinachomfanya kila mwenye akili timamu kufikiria mara mbili mbili kuwa kama walikuwa sahihi kufuata tiba kwake......
Tukio la kutembelewa na waziri au hata naibu waziri ni ambacho kingemuongezea umaarufu na sifa maradufu miongoni mwa jamii ya walalahoi......hata wale waliokuwa na shaka naye kuhusu tiba zake....wataanza kuwa na imani nae....

Uko sahihi kabisa....amenishangaza kwa kukimbia.
 
Mie nilitibiwa ugonjwa wa pumu na watu hawa hawa wa mitishamba ambapo hospitalini walishndwa kunitibia badala yake walikuwa wananipatia za kutuliza tu

Msome vzr Dr...@ Njiwa unaweza kwenda saw a nahuu mjadala
 
Dr. Preta! Mwaka amefanya makosa katika utambulisho wake..

1) Angejinasibisha ni mtaalamu wa Tiba Mbadala kama Mkuu Mzizi Mkavu wa JF

2)Mwaka picha nyingi ninazoziona kwenye mitandao na matangazo amening`iniza stethoscope shingoni... sidhani kama anajua hata kuitumia ? Heart sounds takes years of practice kuzi master ndio maana medicine ni miaka 5 mpaka 6

3)Anapicha nyingine amebeba kitabu cha Obstetrics and Gynecology yeye ni mtaalamu wa tiba mbadala hicho kitabu ni cha nini ? amefika mbali na kujinasibisha ni Mtaalamu wa magonjwa ya kina mama ... jamani! kuwa gynecologist lazima uende Medical school miaka 5 mpaka 6 , ufanye mwaka mmoja wa internship then urudi shule ku specialise miaka 4 tena... mwaka yeye amefanya training ya mwaka mmoja na red-cross china anajiita gynecologist ????

4) Pelvic Exam, kufanya uchuguzi sehemu za siri za kina mama na dada zetu "ONLY A QUALIFIED PHYSICIAN NDIO ANARUHUSIWA JUST INCASE IKATOKEA SEVERE BLEED , A PHYSICIAN WILL KNOW HOW TO INTERVENE " Sidhani Mwaka kama anaweza kushona hata kidonda..

5) Unapofanya pelvic exam kuna some modern equipment's zinatumika again only certified physician ndio anaruhusiwa kuvitumia ... mfano kama mwana mama ana matatizo ya kizazi kumbe she has Carcinoma of the cervix, most of CAX ukigusa tu zina bleed ,, je mwaka ana blood bank pale clinic yake ?!! JE IKATOKEA MGONJWA AMEFARIKI WAKATI MWAKA AKIFANYA PELVIC EXAM UNAJUA ITAKUWA NI MURDER CASE ?! SABABU MWAKA HE WAS NOT TRAINED KUTOA HIYO HUDUMA.

MWISHO

Mimi sina neno na Mwaka! ila tu arudi kwenye misingi yao ya tiba mbadala na asifanye utatibu kama wanavofanya madactari wa modern medicine including kufanya Pelvic exam...

Kuna watu wanacomplain mbona kikombe cha babu watu walitumia ... well babu hakuvaa stethscope , babu hakujiita gynecologist, babu tiba yake ilikuwa ni kiimani zaidi...

hata sisi waislam tuna wataalamu wetu wa tiba za kissuna huwasikii wakijitangaza ni ma gynecologist wala kufanya uchunguzi wa kizazi kama mahospitalini wanavofanya...

Mwaka amshukuru sana Mh.Dr. H. kingwa! sababu ingefika siku mgonjwa akafariki basi mahakamani angehukumiwa kama muuaji sababu si tabibu aliyekuwa trained kufanya yale anayo yafanya ...

Hayo yaliwezekana wakati wa Utawala wa Kikwete na yalifanyika zaidi ya Hayo na kama uchunguzi hautafanyika yataendelea kufanyika.
Huku Kwetu Waganga wa Kienyeji wanalaza Wagonjwa na wanazalisha
Kumbuka ya Loliondo hata Mangufuli alienda kunywa Kikombe
Watu walitolewa Hospitalini akiwemo Edward Hosea wakaenda Loliondo na hilo ni tusi kubwa kuliko kuchunguza Uke
Jambo la Msingi akina Mwaka ni Washirikina na wanakimbilia Kwenye Uke kwa Sababu za Ngono Tu!!
 
Poleni sana ambao wamke wenu wamechunguliwa huko dantauni na Dr. Mwaka bingwa wa Miziziology! Tembele ba wewe shemeji yetu alichunguliwa? Isije ikawa hizi hasira ni kutokana na hayo? Huyu jamaa Mimi nilikuwa nahoji sana kuhusu ELIMU yake maana nilikuwa simfahamu, kilichonifanya nianze kumsikia ni kipindi cha michezo cha clouds kuhusu ndondo cup! Lakini pia matangazo yake kwenye runinga akiwa amepiga white coat na kitu kinaninginia (kwa lafudhi ya Kihaya) shingoni. Sasa najiuliza hawa wamama wanaotoa ushuhuda nao ni fake? Serikali ilikuwa wapi muda wote huo? Kigwa si alikuwa mbunge? Haya alikuwa hayajui? Je, mke wake hajaenda kupata tiba hapo ili apate mtoto? Hizi hasira siyo bure!
 
Back
Top Bottom