Dr. Mvungi: Mwanafamilia aibua mapya kuhusu kifo chake

Dr. Mvungi: Mwanafamilia aibua mapya kuhusu kifo chake

politiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Posts
2,376
Reaction score
1,519
Jakaya%20Kikwete(19).jpg

Rais Jakaya Kikwete, akimfariji mjane wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi, Anna, baada ya kwenda nyumbani kwake Mpiji Magohe, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam jana.(PICHA:OMAR FUNGO)

Familia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Sheria, Dk. Senkondo Mvungi (61), imesema watu waliosababisha kifo chake walipoingia ndani cha kwanza walitaka kompyuta mpakato (laptop) na nyaraka muhimu.

Mmoja wa wanafamilia hiyo (jina limehifadhiwa) akizungumza na NIPASHE nyumbani kwa marehemu Dk. Mvungi, eneo la Mpiji Magohe, alisema hadi sasa wako kwenye kiza kinene juu ya lengo la waliosababisha kifo cha ndugu yao.

Akielezea mazingira ya siku ya tukio, alisema watu hao walivunja mlango wa nyuma ambao unaingia jikoni na kumkutana kijana msaidizi wa Dk. Mvungi na kumkamata na kwenda naye hadi sebuleni.

“Walimkamata na kupanda naye hadi sebuleni, Dk. Mvungi alisikia purukushani na kuamua kutoka akiwa hana silaha yoyote, walipomwona walimfuata na kumng’angania huku wakisema wanataka laptop yake na nyakara muhimu,” alisema.

Alisema watu hao walikuwa wanne na hawakuficha sura zao na kwamba Dk. Mvungi hakukubaliana nao haraka na katika zogo hilo, mmoja wa watu hao alijeruhiwa kichwani na kuanza kuchuruzika damu.

“Baada ya mwenzao kutokwa na damu mmoja alisema hapa si salama akatoa panga na kumkata mara tatu Dk. Mvungi ambaye alianguka chini na walikwenda kwenye kabati na kutoa komyuta na nyaraka mbalimbali, bastola ya marehemu na kisha kumfuata mke wa marehemu wakitaka fedha wakachukua fedha kwenye kabati na kuondoka,” alisema.

Aidha, ndugu huyo alisema anashangazwa na taarifa za polisi kuonyesha mapanga na kigoda pekee, huku kompyuta haijulikani ilipo na watu hao tangu wanaingia walihitaji kompyuta na nyaraka muhimu.

“Ni vyema Polisi wakafanya uchunguzi wa kina kwani inaonekana lengo la watu hawa halikuwa fedha, walizichukua mwishoni kabisa baada ya kupata kompyuta na nyaraka hizo na kisha kutokomea,” alisema mwanafamilia huyo.

Alisema eneo hilo halina umeme wa Tanesco bali wanatumia umeme wa jua na kwa siku hiyo taa ya nyuma ilikuwa haiwaki.

MAJIRANI WANASEMAJE?
Baadhi ya majirani walisema kuwa kwenye eneo hilo imekuwa kawaida watu kuvamiwa na kujeruhiwa kutokana na ukweli kuwa hakuna kituo cha polisi na umeme.

“Umeme umeishia eneo la mbali sana na hatuna kituo cha polisi hadi eneo la Mbezi kwa Yusuph, hivi karibuni kuna familia mbili zilivamiwa na kuporwa fedha na kupigwa kwa ubapa wa panga…tunaiomba serikali kutufikiria tunahitaji kituo cha polisi,” alisema Hamida Ally, mkazi wa eneo hilo.

Aidha, alisema baadhi ya mafundi si waaminifu wanavujisha siri za familia wanazofanyia kazi za ujenzi hasa siku wanazolipwa fedha na kwamba kwa kuwa Dk. Mvungi alikuwa anaendelea na ujenzi wa uzio wa nyumba yake walijua ana kiwango kikubwa cha fedha.

SIMANZI NYUMBANI KWAKE

Hali ya simanzi imetanda nyumbani kwake huku viongozi wa serikali, vyama vya siasa, majirani na jamaa wakijumuika na familia ya Dk. Mvungi kuomboleza na kuwafariji.

Nyumba yake ina uzio unaoendelea kujengwa ambao haujafika nusu huku eneo kubwa likiwa wazi.

WARIOBA AWASALI

Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, aliwasilia majira ya saa 6:45 akiwa ameambatana na wajumbe wa Tume hiyo ambao walikwenda kutoa pole kwa wafiwa na mjane wa marehemu na kuweka saini kwenye kitabu cha maombolezo.

Viongozi wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana.

Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Naibu Waziri wake, Angela Kairuki.

Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, ndiye aliyesimama kwa niaba ya familia, chama na taasisi alizowahi kuzifanyia kazi Dk. Mvungi kuzungumzia taratibu za mazishi.

KIKWETE NA SALMA
Aidha, Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, waliwasili majira ya saa 7:35 mchana, ambaye alikwenda moja kwa moja kutoa pole kwa wafiwa na kusaini kitabu cha maombolezo.

Rais Kikwete alitoa pole kwa wajumbe wa Tume na majirani waliokuwapo na kuondoka.

Kwa mujibu wa Mbatia, Dk. Mvungi ameacha mjane Anna Mvungi na watoto Dk. Natujwa Mvungi, Injinia Doreen Mvungi, Nakundwa Mvungi.


Source: Nipashe

Maoni yangu:
Sijawahi kusikia majambazi kuingia ndani na kuanza kudai zipo wapi nyaraka kwanza na kisha laptop na pesa zifuate baadaye
 
kilichonishangaza zaidi ni hao waoitwa majambazi kudai nyaraka kwanza na kutoficha sura zao inamaana wamekuja kuua hao kitu ambacho jambazi huwa anafanya kila analoweza kukiepuka kwa kuepuka kesi ya mada.
 
Polisi wamekamata watu kadhaa, simu na bastola ya marehemu, wamekamata hadi mapanga yanayodaiwa kutumika isipokuwa laptop tu. Jambazi gani wa kutaka nyaraka na laptop?
 
Police haijazungumzia kuwatafuta MASTERMIND wa tukio hilo.

Hao waliokamatwa wametumwa tu. Waliowatuma ndio watafutwe.
 
Ilikuweje Mmoja wao kujeruhiwa na kutoka Damu ???
 
aisee inatia huruma,na kweli alikuwa muadilifu miaka yote hiyo,hata ukuta alikuwa hajamaliza kuzungushia ghorofa lake,wakati mukandala liukuta kwenye hekalu lake ni la kufa mtu.RIP Dr Mvungi
 
Police haijazungumzia kuwatafuta MASTERMIND wa tukio hilo.

Hao waliokamatwa wametumwa tu. Waliowatuma ndio watafutwe.
Walitumwa na nani? Nani ambaye anataka laptop ya Mvungi na kwa sababu gani? Je waliowatuma walikuwa wanataka kuona nini katika laptop hiyo? Je ni mambo yanayohusu Katiba mpya? Ikiwa ni hivyo, Je hawa waliowatuma wanaweza kuwa marafiki au au maadui zake? Ama tusiwaite maadui bali wapinzani wa msimamo wake! Bila shaka hawani wapinzani wa msimamo wake kwani kama kama wangekuwa marafiki au watu wa msimamo wake wangeenda kujadili naye na kupata mtizamo wake! Je msimamo wa Mvungi ulikuwa ni nini kuhusu katiba mpya? Wajumbe wa tume wanaweza kujua kuwa msimamo wake ulikuwa unaweka kundi gani katika wakati mgumu? Nani ambao wangeweza kuwa wapinzani wake? Je msimamo wake ulikuwa unahatarisha masilahi ya kundi hili kiasi cha kuhisi hatari?............
 
These people are so stupid mtu mwennye akili timamu ufanye kazi za muhimu usiwe na back up?? Ukiwa CCM akili inatoweka full
 
Kuna haja gani ya sisi kuwa na mchakato wa katiba ili hali watu wenye mawazo sawa na Dr Mvungi watauwawa na hao wanaoitwa majambazi? Kheri yake yeye anayeweza kuua ama kutoa maelekezo ya nani auwawe kwa faida ya wachahe, maana yeye ataishi milele!
 
nimeishiwa nguvu ghafla.
kama yasemwayo ni kweli na ile laptop kwanini isipatikane?
kama kuna ukweli hao hao waliowahi kwa mbwembwe kutoa pole wakijua kilichonyuma ya pazia inakera
 
Cha ajabu afande Kova kama kawaida yake,katika mambo serious kama haya,yeye huwa analeta maigizo.

Si mnakumbuka katika kikao chake cha kwanza na waandishi,alisema moja ya vitu walivyovikuta kwenye eneo la tukio, ni skafu ya Chadema!

Hivi ni kwa nini JK hampigi chini huyu afande,na nafasi yake ampe mtu mwingine,ili amwache Kova aende akafanye kazi idara ya propaganda pale Lumumba,akiwa sambamba na Nape?!!

Hivi kwa utendaji kazi wa Kova,tunatarajia kweli kuwapata wauaji "real" wa Mvungi?

Si mnakumbuka wakati wa kutekwa kwa Dr Ulimboka,alipotuletea ile movie ya mkenya chizi?

Si mnakumbuka pia wakati aliponyofolewa jicho Absolom Kibanda,afande Kova alijiapiza kuwa,hao majambazi waliohusika na tukio la Kibanda,watakamatwa wote,hivi leo ni zaidi ya miezi 6 tokea tukio hilo litokee,hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa!!

Kwa hiyo hata katika tukio hili la Marehemu Mvungi,tutarajie kuziona movie zake za kawaida afande Kova!
 
Cha ajabu afande Kova kama kawaida yake,katika mambo serious kama haya,yeye huwa analeta maigizo.

Si mnakumbuka katika kikao chake cha kwanza na waandishi,alisema moja ya vitu walivyovikuta kwenye eneo la tukio, ni skafu ya Chadema!

Hivi ni kwa nini JK hampigi chini huyu afande,na nafasi yake ampe mtu mwingine,ili amwache Kova aende akafanye kazi idara ya propaganda pale Lumumba,akiwa sambamba na Nape?!!

Hivi kwa utendaji kazi wa Kova,tunatarajia kweli kuwapata wauaji "real" wa Mvungi?

Si mnakumbuka wakati wa kutekwa kwa Dr Ulimboka,alipotuletea ile movie ya mkenya chizi?

Si mnakumbuka pia wakati aliponyofolewa jicho Absolom Kibanda,afande Kova alijiapiza kuwa,hao majambazi waliohusika na tukio la Kibanda,watakamatwa wote,hivi leo ni zaidi ya miezi 6 tokea tukio hilo litokee,hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa!!

Kwa hiyo hata katika tukio hili la Marehemu Mvungi,tutarajie kuziona movie zake za kawaida afande Kova!

director kover
 
Dr Nvungi kauwawa sababu ya siasa(hilo ni given) na wauwaji wake ni wanasiasa wenzake na hao hao ndiyo watakaofanikisha mazishi yake pamoja na maombolezo yake:

jipeni mda ya huyu mtayasikia mapema sana maana watu waliotumiwa ni local people na sio wazoefu,kova knows it and he is playin with us
 
kilichonishangaza zaidi ni hao waoitwa majambazi kudai nyaraka kwanza na kutoficha sura zao inamaana wamekuja kuua hao kitu ambacho jambazi huwa anafanya kila analoweza kukiepuka kwa kuepuka kesi ya mada.

Mkuu wakati Mzee Warioba anatoa salam za mwisho alisema kazi ya mwisho ambayo Dr. Mvungi aliifanya ilikuwa utafiti wa jambo nyeti kwenye katiba ambalo lilikuwa na utata na ripoti ya utafiti huo aliikabidhi siku ya Ijumaa jioni.connect the dot...............
 
Ilikuweje Mmoja wao kujeruhiwa na kutoka Damu ???

Mvungili alikuwa mtaalamu wa karati na judo, alikuwa anakaa maeneo hatarishi sana hakuna umeme wala jituo cha polisi!
 
Damu ya mtu wa watu ,kipenzi cha jumuiya haitokauka bure!!!!

Tangulia mzee wetu,watu wa silka na uzalendo wako wapo wengi umetufundisha kwa vitendo!!!!!Pumzika kwa amani mzee wetu uhai na weledi wako hukuutupa bali ulipanda mbegu itakayomea na utafurahi milele kwa kazi zako!!!!!!!!

Upate pumziko la amani mzee wetu!!!!
 
Back
Top Bottom