Dr. Mvungi: Mwanafamilia aibua mapya kuhusu kifo chake

Dr. Mvungi: Mwanafamilia aibua mapya kuhusu kifo chake

Akili ndogo kizania et kauwawa na jk au serkal.

Serikali ikikutaka haina haja ya kutumia mapanga.

Utateleza tu choon na kuvnjika mkono kama babu s
 
Dr alwahi kucheza judo na karate so ucshangae jambaz mmoja kujeruhiwa
 
Akili ndogo kizania et kauwawa na jk au serkal.

Serikali ikikutaka haina haja ya kutumia mapanga.

Utateleza tu choon na kuvnjika mkono kama babu s


Unataka kutolea maelezo jambo kubwa sana kuliko uwezo wako mkuu,
;acha na kila mtu awaze kwa upeo wake ndio maana ya forum!!!!!!!!!

Unapoandika jione kama upo mkutanoni ambapo unaweza ulizwa swali na wahudhuriaji; je unaweza kuendesha mnakasha kwa kauli zako!!!!!!

Tafakari tu mkuu
 
Dr.Mvungi ameuliwa na hii G....nt full stop!
 
Dr Nvungi kauwawa sababu ya siasa(hilo ni given) na wauwaji wake ni wanasiasa wenzake na hao hao ndiyo watakaofanikisha mazishi yake pamoja na maombolezo yake:

jipeni mda ya huyu mtayasikia mapema sana maana watu waliotumiwa ni local people na sio wazoefu,kova knows it and he is playin with us

funguka zaidi mkuu,tunakuombea "mapepo ya mauti"(from Mwijulu) yasikutafute.
 
Police fanyeni uchunguzi kwa maelezo haya, hawa watu wanaonekana kabisa kuna kitu walifwata cio pesa.
 
Jakaya%20Kikwete(19).jpg

Rais Jakaya Kikwete, akimfariji mjane wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi, Anna, baada ya kwenda nyumbani kwake Mpiji Magohe, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam jana.(PICHA:OMAR FUNGO)

Familia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Sheria, Dk. Senkondo Mvungi (61), imesema watu waliosababisha kifo chake walipoingia ndani cha kwanza walitaka kompyuta mpakato (laptop) na nyaraka muhimu.

Mmoja wa wanafamilia hiyo (jina limehifadhiwa) akizungumza na NIPASHE nyumbani kwa marehemu Dk. Mvungi, eneo la Mpiji Magohe, alisema hadi sasa wako kwenye kiza kinene juu ya lengo la waliosababisha kifo cha ndugu yao.

Akielezea mazingira ya siku ya tukio, alisema watu hao walivunja mlango wa nyuma ambao unaingia jikoni na kumkutana kijana msaidizi wa Dk. Mvungi na kumkamata na kwenda naye hadi sebuleni.

“Walimkamata na kupanda naye hadi sebuleni, Dk. Mvungi alisikia purukushani na kuamua kutoka akiwa hana silaha yoyote, walipomwona walimfuata na kumng’angania huku wakisema wanataka laptop yake na nyakara muhimu,” alisema.

Alisema watu hao walikuwa wanne na hawakuficha sura zao na kwamba Dk. Mvungi hakukubaliana nao haraka na katika zogo hilo, mmoja wa watu hao alijeruhiwa kichwani na kuanza kuchuruzika damu.

“Baada ya mwenzao kutokwa na damu mmoja alisema hapa si salama akatoa panga na kumkata mara tatu Dk. Mvungi ambaye alianguka chini na walikwenda kwenye kabati na kutoa komyuta na nyaraka mbalimbali, bastola ya marehemu na kisha kumfuata mke wa marehemu wakitaka fedha wakachukua fedha kwenye kabati na kuondoka,” alisema.

Aidha, ndugu huyo alisema anashangazwa na taarifa za polisi kuonyesha mapanga na kigoda pekee, huku kompyuta haijulikani ilipo na watu hao tangu wanaingia walihitaji kompyuta na nyaraka muhimu.

“Ni vyema Polisi wakafanya uchunguzi wa kina kwani inaonekana lengo la watu hawa halikuwa fedha, walizichukua mwishoni kabisa baada ya kupata kompyuta na nyaraka hizo na kisha kutokomea,” alisema mwanafamilia huyo.

Alisema eneo hilo halina umeme wa Tanesco bali wanatumia umeme wa jua na kwa siku hiyo taa ya nyuma ilikuwa haiwaki.

MAJIRANI WANASEMAJE?
Baadhi ya majirani walisema kuwa kwenye eneo hilo imekuwa kawaida watu kuvamiwa na kujeruhiwa kutokana na ukweli kuwa hakuna kituo cha polisi na umeme.

“Umeme umeishia eneo la mbali sana na hatuna kituo cha polisi hadi eneo la Mbezi kwa Yusuph, hivi karibuni kuna familia mbili zilivamiwa na kuporwa fedha na kupigwa kwa ubapa wa panga…tunaiomba serikali kutufikiria tunahitaji kituo cha polisi,” alisema Hamida Ally, mkazi wa eneo hilo.

Aidha, alisema baadhi ya mafundi si waaminifu wanavujisha siri za familia wanazofanyia kazi za ujenzi hasa siku wanazolipwa fedha na kwamba kwa kuwa Dk. Mvungi alikuwa anaendelea na ujenzi wa uzio wa nyumba yake walijua ana kiwango kikubwa cha fedha.

SIMANZI NYUMBANI KWAKE

Hali ya simanzi imetanda nyumbani kwake huku viongozi wa serikali, vyama vya siasa, majirani na jamaa wakijumuika na familia ya Dk. Mvungi kuomboleza na kuwafariji.

Nyumba yake ina uzio unaoendelea kujengwa ambao haujafika nusu huku eneo kubwa likiwa wazi.

WARIOBA AWASALI

Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, aliwasilia majira ya saa 6:45 akiwa ameambatana na wajumbe wa Tume hiyo ambao walikwenda kutoa pole kwa wafiwa na mjane wa marehemu na kuweka saini kwenye kitabu cha maombolezo.

Viongozi wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana.

Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Naibu Waziri wake, Angela Kairuki.

Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, ndiye aliyesimama kwa niaba ya familia, chama na taasisi alizowahi kuzifanyia kazi Dk. Mvungi kuzungumzia taratibu za mazishi.

KIKWETE NA SALMA
Aidha, Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, waliwasili majira ya saa 7:35 mchana, ambaye alikwenda moja kwa moja kutoa pole kwa wafiwa na kusaini kitabu cha maombolezo.

Rais Kikwete alitoa pole kwa wajumbe wa Tume na majirani waliokuwapo na kuondoka.

Kwa mujibu wa Mbatia, Dk. Mvungi ameacha mjane Anna Mvungi na watoto Dk. Natujwa Mvungi, Injinia Doreen Mvungi, Nakundwa Mvungi.


Source: Nipashe

Maoni yangu:
Sijawahi kusikia majambazi kuingia ndani na kuanza kudai zipo wapi nyaraka kwanza na kisha laptop na pesa zifuate baadaye

Kua uyaone na ukishangaa ya musa utayaona ya filaun
 
Hawataweza kutunyamazisha watanzania wote. Ipo siku yote yatajulikana na Tanzania tuitakayo itapatikana tu....... Ulale mahali pema peponi Dk Mvungi!
 
funguka zaidi mkuu,tunakuombea "mapepo ya mauti"(from Mwijulu) yasikutafute.

Bora mtu augue na tuguze kisha naishindikane afe tuzike yaishe au bora mtu apate ajali ya gari au kuanguka ghafla kuliko kifo kilichomkumba mzee wetu.

mkuu sina lolote la siri na wala sijampoint mtu kuwa anahusika bali hawa wanaolinda sheria kugeuka wanasiasa ni kitu kibaya sana na mara nyingi mambo kama haya hujirudia hata ndani ya familia zao,kifupi ukitaka ulijue jeshi la police vzr gusa mtu wao
 
ni aibu kuwa ni viongozi aina ya kova,nchi ya ovyo sana hii.!!
 
Damu ya mtu wa watu ,kipenzi cha jumuiya haitokauka bure!!!!

Tangulia mzee wetu,watu wa silka na uzalendo wako wapo wengi umetufundisha kwa vitendo!!!!!Pumzika kwa amani mzee wetu uhai na weledi wako hukuutupa bali ulipanda mbegu itakayomea na utafurahi milele kwa kazi zako!!!!!!!!

Upate pumziko la amani mzee wetu!!!!
No doubt, the state is at steke.
 
Polisi wamekamata watu kadhaa, simu na bastola ya marehemu, wamekamata hadi mapanga yanayodaiwa kutumika isipokuwa laptop tu. Jambazi gani wa kutaka nyaraka na laptop?
kila nikiwaambia kaka mkuu ni kijino pembe mnakataa na kumtetea.
 
majambazi siku hizi wanaiba nyaraka kwanza! huitaji utaalamu kujua kuna sababu nyuma ya pazia
 
Back
Top Bottom