Cha ajabu afande Kova kama kawaida yake,katika mambo serious kama haya,yeye huwa analeta maigizo. Si mnakumbuka katika kikao chake cha kwanza na waandishi,alisema moja ya vitu walivyovikuta kwenye eneo la tukio, ni skafu ya Chadema! Hivi ni kwa nini JK hampigi chini huyu afande,na nafasi yake ampe mtu mwingine,ili amwache Kova aende akafanye kazi idara ya propaganda pale Lumumba,akiwa sambamba na Nape?!! Hivi kwa utendaji kazi wa Kova,tunatarajia kweli kuwapata wauaji "real" wa Mvungi? Si mnakumbuka wakati wa kutekwa kwa Dr Ulimboka,alipotuletea ile movie ya mkenya chizi? Si mnakumbuka pia wakati aliponyofolewa jicho Absolom Kibanda,afande Kova alijiapiza kuwa,hao majambazi waliohusika na tukio la Kibanda,watakamatwa wote,hivi leo ni zaidi ya miezi 6 tokea tukio hilo litokee,hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa!! Kwa hiyo hata katika tukio hili la Marehemu Mvungi,tutarajie kuziona movie zake za kawaida afande Kova!