Amina Thomas
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 272
- 130
Nilipata bahati ya kuangalia kipindi cha uswazi kinachorushwa na channel 5. Wiki ya juzi waliahidi kwamba ktk kipindi kifuatacho wataonesha dokta Manyaunyau akitafuta 'nyoka' ambaye wananchi wa eneo hilo walidai kua anagonga na ku ua watu. Sikupata bahati ya kujua jina la sehemu hiyo ila ni hapa hapa dar. Hivyo jumapili ya juzi nikasubiri kwa hamu kuona jinsi huyo mganga anavyomtoa nyoka. Kwa kupitia runinga, niliona umati mkubwa wa watu ukifuatilia utoaji wa nyoka. Dokta huyo kila mara huanza kwa kuchinja paka na kunywa damu yake kwa kumfyonza kwa mdomo. So disgusting! Akaanza kumsaka nyoka na hatimaye kumtoa nyoka huyo toka kwenye shimo. Hata kama mazingaombwe, nilitegemea kuona at least nyoka wa ukweli. Dokta aliibuka na uchafu ndani ya sijui rambo au nini. Ila ni dude fulani. Hivi serikali inaruhusu mambo kama haya ktk karne hii? Maana jamaa anadai amepata ruhusa toka serikali ya mitaa. Next week amedai atakua na kazi ya kusaka wachawi hapo mtaani. Nilivyoona mimi ni kama kundi la wahuni ambao wanawa brain wash watu. Nina hofu watu hao wanaweza kuleta uchonganishi mkubwa baina ya wakazi wa eneo hilo, na pia anaweza kusababisha maradhi mapya duniani kama vile swine flu.