Dr Magufuli awasha moto Dar - ofisi ya RC Lukuvi na Manager Tanroads kubomolewa!

Kwa nini CDM na sio upinzani in general? nyie mnaharibu sana mahali hapa mkiwa na mawazo ya U-CDM, kwa nini kulazimishana? vyama viko vingi na vina sera tofauti, kama hazipendi sera za CDM lazima awe CDM?? muwe mnajaribu kufikiria out of the box???

Ona sasa unamsifia akiwa CCM! sio utamsifia akiwa TLP pia??

Hayo ni maoni yake kwamba angependa jamaa awe CDM! We toa yako yaliyo nje ya box.. lakini uwe wazi box gani NCCR? PPTA? Jahazi asilia?
 
Kweli magufuli ni mchapakazi sana ila sijakubali apewe nafasi za juu hadi hapo atakapotubu ile dhambi kuu au ufisadi mkuu wa kuuza nyumba za serikali. Ufisadi huu unaendelea na utaendelea kuligharimu taifa fedha nyingi, Je mnajua ni viongozi wangapi wapya wanaishi mahotelini kwa kuwa hakuna nyumba za serikali wanazostahili? Ili kurekebisha jambo hili nyumba hizo zirudishwe serikalini na wahusika wafidiwe (hela nyingi pia)
 
sasas nyie mnataka mtu afanye nini? Akizembea mnasema mla rushwa. Kachachamaa kafanya kazi mnasema anatafuta njia . Nyie watu wa aina gani?

Wanataka viongozi kama hawa labda

MBUNGE wa Bumbuli, Januari Makamba, amezindua huduma ya mawasilino na wakazi wa jimbo lake ambao watakuwa wanatuma ujumbe mfupi katika simu zao na gharama za malipo zinakuwa chini yake. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamba alisema mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuharakisha maendeleo.

Alisema kwa kuzingatia hilo , wananchi wa Bumbuli lazima wawe miongoni mwa mamilioni ya Watanzania wanaopaswa kuwa na mawasiliano hayo, ili nao wapige hatua za haraka maendeleo."Nimefanya mazungumzo na kampuni za simu,lengo ni kuleta mawasiliano karibu ili wananchi wangu waweze kunufaika na mpango huo. Nitafanya semina elekezi ya viongozi ili waweze kuwahamasisha wananchi wa Jimbo la Bumbuli kuhusu mpango huo,"alisema Makamba.

Mbunge huyo wa Bumbuli aliandaa semina ya viongozi wa kata, viti wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kupangiana majukumu ya kutekeleza Ilaani ya CCM.Alisema kwa kipindi kirefu, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaendeleo na kwamba hadi sasa bado wako nyuma.

Alisema kwa msingi huo, kuna kila sababu za kubuni mikakati ya kujiletea maendeleo kwa haraka."Kwa miaka mingi sasa tumekabiliwa na tatizo la kutafuta maendeleo na bado hatujafanikiwa, lakini nadhani wakati umefika wa kutoka kwenye boksi na kufanya kazi kwa bidii ili tupate maendeleo,"alibainisha.Kwa mujibu wa Makamba, wajibu wake kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wa jimbo hilo, ambalo kabla ya uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, lilikuwa linawakilishwa bungeni na Wiliam Shellukindo ambaye alishindwa katika kura za maoni ndani ya CCM.

Mbunge huyo wa sasa, aliwataka wananchi kushirikiana na viongozio wao, ili iwe rahisi kutekeleza mikakati ya kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema, aliwataka viongozi wote walioko madarakani, kutekeleza ahadi zao kwa wakati.Hali kadhalika aliwahimiza watendaji wa vijiji, kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya fedha wanazochanga, ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Alisema kufanya hivyo, kutawafanya wananchi wawe na imani na viongozi hao.Wakati huo huo, baadhi ya wananchi walitoa malalamiko yao kwa uongozi wa Jimbo hilo kuwa, baadhi ya watendaji wa kijiji wamekuwa wakiwatoza fedha katika kupata huduma mbalimbali.Huduma hizo ni pamoja na kupigiwa mihuri, kuandikiwa barua na kadhalika.Kuhusu hilo, Mkuu wa Wilaya alionya viongozi wa vijiji kuacha mara moja kuwatoza wananchi gharama za mihuri au kuandikiwa barua.
 
Mh Dr Magufuli ameamuru ofisi ya RC Lukuvi na ya manager mkuu Tanroads - dar zimepewa siku 5 kubomolewa maana zinatajwa kujengwa ndani ya 'road reserves'. pia kagundua malipo feki ya fidia ambayo yangelipwa kwa watu zaidi ya 60, ambayo ni zaidi ya milion 600. salaale CCM na serikali yake! finish!
source: RFA reporters.

my take:
hili lijamaa halikutakiwa liwepo bado ktk chama hiki cha wezi. alitakiwa awe CDM ili kazi zake zikamilike ktk mikono safi.

Asingekuwa waziri!
 
Hapo hapo Magufuli, alipokomea Moringe endeleza. tafuta na ile kazi ya kolimba uimalizie. Mimi nakuona kama mzalendo, ndio binadamu hakosi kasoro lakini umekomaa. Kuhusu chama, aa, chama chochote ukiwa na dhamira nzuri unapeta.
 
Back
Top Bottom