Dr. Magufuli aongezewe washauri, anakwenda mrama

Dr. Magufuli aongezewe washauri, anakwenda mrama

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Ingawa sipo kwenye timu ya Kampeni ya mgombea wetu wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli,naujua uchungu wa chama hiki.Tumetoka nacho mbali na si rahisi kukiacha mkono. Nitamsaidia kwa kumkosoa na kuikosoa aina yake ya kampeni. Dr. Magufuli anakwenda mrama. Anayumba kikampeni. Anatoka kwenye mstari. Anatetereka. Aongezewe timu ya washauri mapema au waliopo wabadilishwe.

Aina ya kampeni ya kukosoa na kushangaa inashangaza sana. Anatumia muda mwingi kukosoa mambo ya kiserikali kana kwamba hakuwahi kuwemo humo. Anafanya hivyo kana kwamba anawachongea waliokuwa viongozi wake serikalini kuwa walikuwa vikwazo kwake ili asitekeleze majukumu yake. Amekuwa akishangaashangaa mambo mbalimbali yanavyofanyika kana kwamba yeye ni mgombea wa upinzani. Anakwenda mrama.

Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Japo nimeshindwa kusoma yote, ila nakumbuka juzi ulikuja na thredi, na ndani yake ulisema we uko kwenye team ya kampeni.
 
Magufuli ana timu mahiri sana ya kampeni ikiongozwa na Kinana na akina January.....
Tatizo sio magufuli kukosoa au kushangaa bali ni UKAKASI WA MATENDO YA SERIKALI YA CCM inayojaribu tena kuwaghilibu wapiga kura. Magufuli UONGO hawezii kwa hiyo anatemaa MAKAVUUU LIVE....
 
Ook wapendwa.tuwe wakweli nini kinamfanya ashangae weakness za serikali??mfano.suala la dawa hospitalini.ni kweli hakuna madawa na vifaa tiba na msd wanaidai serikali mpaka leo.pia suala la damu salama ambayo haipo kwenye zonal centres nayo madaktar na manesi wameinywa??? Think twice who the cap fits?????
 
Kwenye bango lake amesema "CHAGUA MAGUFULI" full stop!! CCM haitambui!
Kwingine kapiga piiipozzz power naomba kura zenu!!
Slogan ya "wanataka mabadiliko" anayotumia. Kifupi hana mzuka na CCM! Pia kumbuka kuwa pale Jangwani alisema "Chagueni wabunge watakaoibana serikali yake"(kama atashinda) means siyo maccm!! Ni mgombea binafsi na anawakubali sana wapinzani!!
 
Back
Top Bottom