Dr. Magufuli aongezewe washauri, anakwenda mrama

Ook wapendwa.tuwe wakweli nini kinamfanya ashangae weakness za serikali??mfano.suala la dawa hospitalini.ni kweli hakuna madawa na vifaa tiba na msd wanaidai serikali mpaka leo.pia suala la damu salama ambayo haipo kwenye zonal centres nayo madaktar na manesi wameinywa??? Think twice who the cap fits?????
Ndiyo wameinywa ndo maana anashangaa unakunywaje damu????
 
Ingawa sipo kwenye timu ya Kampeni ya mgombea wetu wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli,naujua uchungu wa chama hiki.Tumetoka nacho mbali na si rahisi kukiacha mkono. Nitamsaidia kwa kumkosoa na kuikosoa aina yake ya kampeni. Dr. Magufuli anakwenda mrama. Anayumba kikampeni. Anatoka kwenye mstari. Anatetereka. Aongezewe timu ya washauri mapema au waliopo wabadilishwe.

Aina ya kampeni ya kukosoa na kushangaa inashangaza sana. Anatumia muda mwingi kukosoa mambo ya kiserikali kana kwamba hakuwahi kuwemo humo. Anafanya hivyo kana kwamba anawachongea waliokuwa viongozi wake serikalini kuwa walikuwa vikwazo kwake ili asitekeleze majukumu yake. Amekuwa akishangaashangaa mambo mbalimbali yanavyofanyika kana kwamba yeye ni mgombea wa upinzani. Anakwenda mrama.

Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Jana amerejelea makosa aliyoyafanya Igunga kwa kutoa maagizo kwa Tanroad! Sijui mshauri wake akumweleza kuwa akishakuwa mgombea siyo waziri tena na hata akiwa wazirimaagizo ya namna hiyo ni dhairi hongo kwa ajili ya kupata kura!
 
Ingawa sipo kwenye timu ya Kampeni ya mgombea wetu wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli,naujua uchungu wa chama hiki.Tumetoka nacho mbali na si rahisi kukiacha mkono. Nitamsaidia kwa kumkosoa na kuikosoa aina yake ya kampeni. Dr. Magufuli anakwenda mrama. Anayumba kikampeni. Anatoka kwenye mstari. Anatetereka. Aongezewe timu ya washauri mapema au waliopo wabadilishwe.

Aina ya kampeni ya kukosoa na kushangaa inashangaza sana. Anatumia muda mwingi kukosoa mambo ya kiserikali kana kwamba hakuwahi kuwemo humo. Anafanya hivyo kana kwamba anawachongea waliokuwa viongozi wake serikalini kuwa walikuwa vikwazo kwake ili asitekeleze majukumu yake. Amekuwa akishangaashangaa mambo mbalimbali yanavyofanyika kana kwamba yeye ni mgombea wa upinzani. Anakwenda mrama.

Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Huyu hafai kabisa kuwa kiongozi mkuu bali anafaa kuwa manager tu.
Mwandikie waraka mkubwa wake
 
Mwache arahisishe kampeni za UKAWA maana anawasaidia kuwaeleza watanzania matatizo ya serikali ya CCM. Kazi iliyobaki ni kufanya reference ya maneno yake na kuwaambia msimchague maana anawadanganya ni wale wale akina mzee tupa tupa

Ingawa sipo kwenye timu ya Kampeni ya mgombea wetu wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli,naujua uchungu wa chama hiki.Tumetoka nacho mbali na si rahisi kukiacha mkono. Nitamsaidia kwa kumkosoa na kuikosoa aina yake ya kampeni. Dr. Magufuli anakwenda mrama. Anayumba kikampeni. Anatoka kwenye mstari. Anatetereka. Aongezewe timu ya washauri mapema au waliopo wabadilishwe.

Aina ya kampeni ya kukosoa na kushangaa inashangaza sana. Anatumia muda mwingi kukosoa mambo ya kiserikali kana kwamba hakuwahi kuwemo humo. Anafanya hivyo kana kwamba anawachongea waliokuwa viongozi wake serikalini kuwa walikuwa vikwazo kwake ili asitekeleze majukumu yake. Amekuwa akishangaashangaa mambo mbalimbali yanavyofanyika kana kwamba yeye ni mgombea wa upinzani. Anakwenda mrama.

Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hayuko nje ya mikakati ya CCM. Hiyo ndio mkakati mpya ulioasisiwa na mwenyekiti wa kamati ya ushindi ni lazima ambaye pia ni katibu mkuu wa chama, ndugu Kinana. Kwa takribani mwaka na zaidi sasa Kinana amekuwa akizunguka nchi nzima (akiambatana na vuvuzela la chama) na kuwahadaa wananchi kwa 'kupinga na kukemea' utawala wa ccm majukwaani na kuonesha jinsi serikali ya ccm ilivyoshindwa kudeliver!! Tunaweza kusema ni staili ya kujipaka kinyesi chako alimradi 'wapumbavu na malofa' wakupe kura zao. Baada ya hapo unasepa na kufuta kinyesi hicho kwa kuoga, tena maji ya dawasco ambayo malofa hawayapati, na kujipulizia utuli, na kuwaacha wakisubiri 'maisha bora' hadi baada ya miaka mitano utakaporejea na kujipaka kinyesi tena na kuwahadaa. Mzunguko wa hadaa unaendelea. Daktari Makufuri anafanya jambo sahihi kwa mujibu wa mikakati ya ushindi ni lazima. Hiyo ina baraka za kamati ya kampeni.
 
Naona CCM wameamua kutumia nguvu za giza kuizima UKAWA, hii mvua inatoka wapi tena? Ndio wale waganga toka Sumbawanga? Wameshashindwa
 
Ingawa sipo kwenye timu ya Kampeni ya mgombea wetu wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli,naujua uchungu wa chama hiki.Tumetoka nacho mbali na si rahisi kukiacha mkono. Nitamsaidia kwa kumkosoa na kuikosoa aina yake ya kampeni. Dr. Magufuli anakwenda mrama. Anayumba kikampeni. Anatoka kwenye mstari. Anatetereka. Aongezewe timu ya washauri mapema au waliopo wabadilishwe.

Aina ya kampeni ya kukosoa na kushangaa inashangaza sana. Anatumia muda mwingi kukosoa mambo ya kiserikali kana kwamba hakuwahi kuwemo humo. Anafanya hivyo kana kwamba anawachongea waliokuwa viongozi wake serikalini kuwa walikuwa vikwazo kwake ili asitekeleze majukumu yake. Amekuwa akishangaashangaa mambo mbalimbali yanavyofanyika kana kwamba yeye ni mgombea wa upinzani. Anakwenda mrama.

Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Wa kwanza kwenda mrama alikuwa mzee Mkapa. Na kwa sasa kampen lazima aende Mrama kwa kuwa ni lazima aseme mabaya ya Serikali au mapungufu ya kiongoz aliyoko madarakani, jambo hilo nalo ni tatizo pia!
 
Wana ccm wenyewe weshaanza malalamiko, atii Huyu jamaa hatusaidii kwenye kampeni wabunge na madiwani. Mpoo?? Mwenyewe hauziki wataka akuuze weye?? Mabadiliko yapo nje ya ccm si vinginevyo. Mtanzania wa leo, hamchagui Lowasa, anachagua upinzani ili tu yatokee mabadiliko ya aina yeyote ile ila si ccm tena. Miaka 54+ imewatosha. Hatumtaki Lowasa, tunataka mabadiliko. Hata akitoka Lowasa leo, tutachagua jiwe au punda si ccm. Tumechokaaaaaa
 
Umeusemea moyo wangu wewe awe Lowassa awe nyani hata nyau ntachagua kuliko kuichagua ccm tena hapanaaaaaa tumechoka kuburuzwaaaa in bawacha's voice jana...
 
Huyo ndiye Rais angetakiwa, Tanzania ya sasa haitaki Rais mwanasiasa bali mtendaji.
 
kwanini hamuandiki tena chagua ccm? Mnaogopa nini?

Mbona nyie hamuandiki wala kuongelea CHADEMA?, Hata Mbowe sasa anaimba wimbo wa LOWASA, MABADILIKO NA LOWASA, si CHADEMA Tena!, CHADEMA IMEPOTEA HATA KWENYE VYOMBO VYA HABARI. CHAMA KIMEFUTIKA TAYARI, JIBU MTAPATA BAADA YA TAREHE 25/10/2015
 
hahahahahaha mzee tupakule mbona hutaki Mgagufuli aseme ukweli? mwacheni atusaidie kuiondoa ccm madarakani wananchi wanamuelewa magufuli!
 
mzee VUTA-NKUVUTE tatizo la wagombea wote wamekosa watu wakuwaandikia speech wamekuwa nanaongea vi2 vya kawaida sana badala ya kuongerea sela na mikakati wamejikita kwenye kutoa ahadi bahati nzuri wamewakuta watanzania wengi huwa wanasikiliza speech rakini hawazichambui kujua porojo na ukweli tatizo jingne ccm jaman toka mmekifunga chuo chenu cha siasa kigamboni mmekuwa mnatoa watu ambao c wakutegemea ktk kujieleza na kutoa hoja zenye mashiko na kuzcmamia hoja zao tatizo la magufuli ndo la lowassa wamejikuta wanatopeza tym kuimba mchaka mchaka kaz hyo wawaachie wakina diamond na frola mbasha wao watupe nondo dah na bahati mbaya wote ni product of ccm jamani wambieni sifa ya mwanasiasa ni uwezo wake wa kucheza na watu na kucheza na hoja na kuztetea na kuzcmamia ccm inaandaa watawala c wanasiasa ndo maana mnajikuta wanatumia ela nying kulipa usafil na wasanii ili kujaza watu wangekuwa na watu wanaojua kuongea kama tundu lisu kulikuwa hakuna haja ya kuweka wasanii na watu wangejaa 2 mikutanoni
 
Last edited by a moderator:
Magufuli amechanganyikiwa , huyo ni Rais wa mabarabara tu. yeye anakazana na sitawaangusha kana kwamba haelewi ccm ilishawaangusha Watanzania kitambo sasa, ni afadhali angekuja na sera ya atatuinuaje. Kwa tafsiri nyingine hiyo sitawaangusha itakuwa ni ujumbe kwa watu wa kitengo waliomuweka pale.
 
Au inawezekana ndiyo kubadilishiwa lugha kama kwa wale wajenzi wa babeli ya kale? Maana huku anasema ataendeleza pale watangulizi wake walipoishia. Akigeuka upande mwingine anashangaa jinsi hali ya huduma kwa jamii ilivyo mbaya, akimeza mate anasema mnitume na sitawaangusha....

Nadhani tunahitaji mtu anayejituma. Huyu wa kusubiria kutumwa atatulaza njaa!
 
Back
Top Bottom