Dr. Magufuli aongezewe washauri, anakwenda mrama

Ingawa sipo kwenye timu ya Kampeni ya mgombea wetu wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli,naujua uchungu wa chama hiki.Tumetoka nacho mbali na si rahisi kukiacha mkono. Nitamsaidia kwa kumkosoa na kuikosoa aina yake ya kampeni. Dr. Magufuli anakwenda mrama. Anayumba kikampeni. Anatoka kwenye mstari. Anatetereka. Aongezewe timu ya washauri mapema au waliopo wabadilishwe.

Aina ya kampeni ya kukosoa na kushangaa inashangaza sana. Anatumia muda mwingi kukosoa mambo ya kiserikali kana kwamba hakuwahi kuwemo humo. Anafanya hivyo kana kwamba anawachongea waliokuwa viongozi wake serikalini kuwa walikuwa vikwazo kwake ili asitekeleze majukumu yake. Amekuwa akishangaashangaa mambo mbalimbali yanavyofanyika kana kwamba yeye ni mgombea wa upinzani. Anakwenda mrama.

Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mhshmiwa alikua anashangaa pia kwann Tanzania ni ya tatu ktk uuzaji wa Tanzanite dunian .India inaongoza ya pili kenya. Wakat Tanzania ndio nchi pekee yanakopatikana haya madini. Very amazing
 
Ingawa sipo kwenye timu ya Kampeni ya mgombea wetu wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli,naujua uchungu wa chama hiki.Tumetoka nacho mbali na si rahisi kukiacha mkono. Nitamsaidia kwa kumkosoa na kuikosoa aina yake ya kampeni. Dr. Magufuli anakwenda mrama. Anayumba kikampeni. Anatoka kwenye mstari. Anatetereka. Aongezewe timu ya washauri mapema au waliopo wabadilishwe.

Aina ya kampeni ya kukosoa na kushangaa inashangaza sana. Anatumia muda mwingi kukosoa mambo ya kiserikali kana kwamba hakuwahi kuwemo humo. Anafanya hivyo kana kwamba anawachongea waliokuwa viongozi wake serikalini kuwa walikuwa vikwazo kwake ili asitekeleze majukumu yake. Amekuwa akishangaashangaa mambo mbalimbali yanavyofanyika kana kwamba yeye ni mgombea wa upinzani. Anakwenda mrama.

Ajirekebishe haraka. Asaidiwe kama inapasa. Iko wazi kuwa, Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mwanasiasa wa jukwaani kabla ya kuteuliwa kugombea Urais. Alishiriki, ukiacha kampeni zake binafsi za Ubunge, kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga tu. Bado mgeni jukwaani na juu ya vya kusema. KUSHANGAASHANGAA na KUKOSOAKOSOA kwake kutamponza na kukiponza chama. Na pia, ameonekana dhahiri kuwa hawezi kuwanadi wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Mzigo unamuelemea. Asaidiwe. Awekewe na mipaka ya ahadi za papo kwa papo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Wewe mzee ni ndumilakuwili,yaani una macho komchuzi.
 
Magufuli ANAMWAIBISHA SANA JAKAYA KIKWETE kwa kutaja waziwazi madhaifu wa mtangulizi wake. Anataja masuala mengi ambayo ni madhaifu makubwa ya JK.
 
KWELI ccm KITUKO NA HAWANA CHA KUWADANGANYA WATANZANIA MAANA UONGO UMEKWISHA NDO MAANA WAMEBAKI KUUWAITA WATZ MALOFA NA WAJINGA KWA KUWA WANAONA WANATUIBIA LAKINI BADO WANACHAGULIWA HIVYO MWAKA HUU TUUKATAE ULOFA, SI MUMEONA MBEYA ANATAMANI CHADEMA THUS
 
Back
Top Bottom