Dr. Magufuli amechafuka, hachaguliki


Brother nafikiri hata watu wenyewe nao akili zao ni za mazoea, personally hata kama ni mbumbu wankiasi gani, MR. PADLOCKS hana ubavu kuondoa mfumo wa CCM uliopo kwa sasa, labsa wafe wote.
Kwa akili yangu nitaendelea kuamini kuwa watanzania tumerogwa sijui na nani,labda mwalimu Nyerere
 
Mimi nilidhani Magufuli anachagulika lakini kwa sasa unasema hachaguliki!

Kwa hiyo wewe unadhani nani anachagulika?

Kuniambia fulani hachaguliki bila kunipa alternative ni sawa sawa na kutoa ushauri wa kijinga!

Kutokuwepo kwa alternative au mwingine anayechagulika, hakumfanyi Magufuli achagulike. Kwa maneno mengine, huhitaji kutoa alternative ili kupata uhalali wa kutoa hoja kuwa Magufuli hachaguliki. Hoja kuwa Magufuli hachaguliki inajitosheleza provided it is based on a sound premise. Uhalali wa kukosoa jambo hautokani na uwepo wa alternative. Kama jambo limekosewa, limekosewa tu bila kujali kuwa matokeo ya kukosewa huko yana mbadala au la. This is Learning How to Think and Argue 101.
 
Mbona mwenyekiti mboe wa cdmanachosema ndio wafuasi wote ndiooooooo
 
Magufuli ana kila sifa ya kuwa kiongozi bora. Tatizo ni hicho chama...... Hila na gilba ni nyingi kushinda nia njema.
 
CCM itapasuka vipande-vipande baada ya Kingunge kuongea tume ya maadili kuvunja kanuni bado Lowasa kuongea .
ushindi wa kishindo kwa #UKAWA unakuja
 
Hoja hapa ni Magufuli anachagulika au hachaguliki.

Huwezi kunieleza alichofanya ni sound premise bila kutoa solution.

Watanzania tuko njiani kwenda kupiga kura halafu unatuambia tunakwenda kumpigia kura mtu ambaye hachaguliki na ametuambia sababu inayomfanya Magufuli asichagulike.

Kwa hiyo nimemuuliza yeye anadhani nani anachagulika?.

Hili ni swali ambalo kwa mtu anayedai anajenga hoja yenye sound premise nadhani angelifahamu kabla ya kutuambia Magufuli hachaguliki.
 
Unajua huyu mzee Kingunge yeye siyo msafi na alikuwa na malengo mabaya na washirika wake. Hivyo kukosa wameharibikiwa
 
..ni kwasababu ya kashfa ya kuuza nyumba za serikali kwa bei ya hasara.

..mdhibiti na mkaguzi wa mahesabu ya serikali, prof.assad, umesema ule ulikuwa ni wizi wa wanasiasa.

..magufuli ameiingiza serikali na taifa hasara kubwa kuliko hasara iliyosababishwa na mramba na yona na kupelekea kufungwa miaka 3.

..magufuli hapaswi kujitetea kwamba ulikuwa uamuzi wa cabinet. Yeye binafsi alijitwalia nyumba. Ni wapi cabinet ilimuelekeza achukue nyumba kwa bei ya kizushi-zushi??

@Ngw'amapalala, Bukyanagandi
 
Last edited by a moderator:
 
Mimi nilidhani Magufuli anachagulika lakini kwa sasa unasema hachaguliki!

Kwa hiyo wewe unadhani nani anachagulika?

Kuniambia fulani hachaguliki bila kunipa alternative ni sawa sawa na kutoa ushauri wa kijinga!

Hii si mantiki sahii; mtu akikuambia barabara ile ina simba ni lazima akuoneshe barabara isiyo na simba ili uende unakotaka? Wakati mwingine mambo mengine inabidi wewe mwenyewe uyatafutie majibu.
 
Mkuu,
Hizo hoja za nyumba za serikali zimeishajibiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo, Frederick Sumaye.

Kwa maelezo zaidi, angalia hii video

[video]https://youtu.be/LofQGOS0bCM[/video]

Kuhusu yeye kuchukua nyumba, ingekuwa ni vizuri ukaleta documents hapa badala ya kuanza kujadili scuttlebutt lakini vile vile, kwani yeye hakuruhusiwa kisheria au kikanuni kununua nyumba zilizokuwa za serikali.
 

Ona unavyojichanganya,kama Nyerere alikuwa safi huku akiitumia CCM hiyohiyo na unasema CCM ya Nyerere ilikuwa safi basi maana yake tatizo sio mfumo,hili ndilo tatizo la kukariri bila kuelewa ndio maana mnajichanganya kama hivi.
 
Hii si mantiki sahii; mtu akikuambia barabara ile ina simba ni lazima akuoneshe barabara isiyo na simba ili uende unakotaka? Wakati mwingine mambo mengine inabidi wewe mwenyewe uyatafutie majibu.
Mtu akikuambia barabara ile unayotaka kupita ina simba, na wewe hufahamu barabara nyingine zaidi ya hiyo na una akili timamu, lazima utamuuliza kama anafahamu barabara nyingine ambayo haina hatari.

Mimi nimeuliza kama anafahamu barabara nyingine isiyo na hatari anieleze.

Hili ni swali la kawaida katika mazungumzo.
 
Ona unavyojichanganya,kama Nyerere alikuwa safi huku akiitumia CCM hiyohiyo na unasema CCM ya Nyerere ilikuwa safi basi maana yake tatizo sio mfumo,hili ndilo tatizo la kukariri bila kuelewa ndio maana mnajichanganya kama hivi.


Wewe ndiye unajichanganya mkuu. Tatizo la CCM sio mtu bali ni mfumo. Hata huyu Kikwete mwaka 2005 wakati anaingia madarakani alituaminisha kuwa atahakikisha kila Mtanzania anapata maisha bora. Miaka kumi inakaribia kuisha maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyoahidiwa na Rais Kikwete mwaka 2005, yamebaki ni kitendawili na sasa jamaa anaondoka kwa aibu kubwa. Tulichoshuhudia ndani ya miaka yake takribani 10 ni UFISADI, Rushwa, Wizi na Ubadhirifu wa mali za umma.

Baadhi ya skandali zilizotikisa kipindi cha utawala wake ni pmj na EPA, IPTL, Kagoda, Tangold, Meremeta, Richmond na Escrow, kutaja kwa uchache. Hapo sijaongelea matukio ya ubadhirifu katika halmashauri nyingi nchini.Ni kipindi ambacho tumeshuhudia tembo wakipukutika kutokana na ujangiri uliokithiri. Vitendo vya ujambazi na ugaidi km kuvamiwa vituo vya Polisi hatukuwahi kuvishuhudia huko nyuma. Sasa ukiangalia matukio kama haya tatizo lake sio Kikwete, bali ni mfumo mbovu na sera zilizoshindwa za CCM.

Lazima tuseme ukweli hata kama ni mchungu. Mwl.Nyerere hakuacha CCM ya wezi, majizi, walaghai na mafisadi kama nyinyi. Huu ndio umadhubuti unaousema mkuu? Nawashauri muache kutapeli Wananchi kwa kauli za Nyerere bila kuangalia muktadha wake. CCM ya leo imejaa majizi, matepeli na walaghai. Huu sio umadhubuti, bali ni ulegelege. Kama alivyowahi kusema Nyerere mwenyewe, chama legelege huzaa serikali legelege. Na siku zenu zinahesabika wahuni nyie. Tafakari
 
VUTA-NKUVUTE

Endelaeeni kusema tu KINGUNGE SIYO MUNGU TUNASUBIRI SIKU YA KUAPISHWA TU MAGUFULI NI RAIS TAYARI HAKUNA WA KUMZUIA ISIPOKUWA MUNGU TU. BAADA YA KUSHINDWA SUNGURA ALISEMA SIZITAKI MBICHI HIZI KWA HIYO HATUSHANGAI KUSIKIA MASHAIRI HAYO.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Kwani huyu Nyerere alikuwa kwenye mfumo gani ambao ni tofauti na huu unaodai kwa sasa haufai?

Nielimishe!
 
Usijitie ujuha kiasi hicho cha kujifanya hujui tofauti kubwa iliyopo wakati Mwalimu alipokuwa kiongozi wa Tanzania na hawa wahuni, wezi, wapokea rushwa n.k. Unadhani jina la Baba wa Taifa lilidondoka toka mbinguni? Unadhani kwanini Watanzania walio wengi bado wanampenda sana na kumuenzi pamoja na kuwa aling'atuka miaka 30 iliyopita?

Mkuu,
Kwani huyu Nyerere alikuwa kwenye mfumo gani ambao ni tofauti na huu unaodai kwa sasa haufai?

Nielimishe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…