Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

mwobho

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
808
Reaction score
352
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti' mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.


Source:
Raia Mwema
 
Aliyoandika. Dr.Kitila Mkumbo kwenye gazeti la Raia mwema.
********************
.Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.

Tumeikataa CCM kwasababu inakumbatia makosa kwa kuogopa watu eti watayumbisha nchi. Lazima tujifunze kutoa adhabu na kupokea adhabu lazima tuanze na ZZK ili kutengeneza std zinazokubalika. NCCR haikuwa taasisi ilikuwa ni viongozi wenye uchu mkubwa sana wa madaraka na fedha, usalama wa taifa nk. Mazingira yamebadilika sana hatuwezi kuacha kuadhibiana kwa kuogopa kivuli cha NCCR. Dr ingebidi kwanza useme wazi je kwenye sakata lenu kwa vyovyote vile mlivunja katiba ya chama na kama mlivunja adhabu yake ilikuwa nini kwa mujibu wa katiba?

Lazima tuzifuate sheria zetu tulizokubaliana nazo. Sioni upofu wa wanachama ila naona tamaa ya tuliowaamini.
 
So Kitila Mkumbo you need mbadala wa CDM na CCM, kwa hiyo mlitaka muangamize CDM ili muelekee kwa huyo mbala. Acheni uhuni bhana.

Wakati wa uchaguzi 2010 kampeni zinaendelea. Zitto alikuwa busy kutangaza atagombea Urais 2015. Was it right timing? Acheni uhuni na kuaminisha wananchi ujinga.

Ndio Zitto alitaka kugombea Uenyekiti wa CDM, Kitila nakwambia kwamba, huyo Zitto wako angepata Uenyekiti leo CDM isingekuwepo.

Endelea kutuletea porojo zako unadhani wote ni mabwege.......
 
Kwenye andiko hili la Mh Dr. Kitila nimeona kuna sehemu mbili au tatu kama kajichanganya

1.Anaposema uteuzi ni kwa wateule tu

na sio kama utaratibu ulivyo wa kujaza fomu na kurudisha

Swali katika waraka huo ambao waliuandaa je walipiga kura wenyewe wa nne kwa maana dr kitila,zitto,mwigamba na huyo mm2 na zito akashinda?au waliamua tu kumteua au alijiteua zito mwenyewe?


2.Chama hakijengi mfumo wa kushabikiwa ila viongozi wametengenexa mfumo wa kushabikiwa wao,viongozi

Je hapo haoni kama zitto nae amehusika kutengeneza mfumo huo mbona na yeye alikuwa na watu wanaomuunga mkono yeye kama yeye?

3.Hivi dr katiba yetu ya leo na hii rasimu ikipita umri wa MGOMEA URAIS UTAKUA NA NIKUANZIA MIAKA MINGAPI

JE zitto mungu akitujalia uhai atakua amefikisha umri halisi wa kupigiwa kura kama rais????

4.Hivi NCCR MAGEUZI NA CHADEMA mwaka 2010 waliopeperusha bendera ya kugombea urais walikuwa wenyeviti wa VYAMA VYAO????????


SHUKRANI MLETA UZI NA DR KITILA.
 
So Kitila Mkumbo you need mbadala wa CDM na CCM, kwa hiyo mlitaka muangamize CDM ili muelekee kwa huyo mbala. Acheni uhuni bhana.

Wakati wa uchaguzi 2010 kampeni zinaendelea. Zitto alikuwa busy kutangaza atagombea Urais 2015. Was it right timing? Acheni uhuni na kuaminisha wananchi ujinga.

Ndio Zitto alitaka kugombea Uenyekiti wa CDM, Kitila nakwambia kwamba, huyo Zitto wako angepata Uenyekiti leo CDM isingekuwepo.

Endelea kutuletea porojo zako unadhani wote ni mabwege.......
Kitu cha pekee ninachoamini ni kuwa Kitila hamjui Zitto wala hajui dhamira ya moyoni mwa Zitto. Ameburuzwa tu na bahati mbaya amekubali kuburuzika
 
Mkuu Mlengo wa Kati, hebu kuwa mstaraabu basi hata kidogo, mbona ngono ni jambo la kawaida sana. Hebu tumia robo tu ya akili yako kisha uje hapa utuambia criteria ya kwanza kwa Viti maalumu na UDC vinapatikanaje!!!!

Kama ni ngono hata wewe ulizaliwa baada ya ngono kuwa imefanyika.

Acha ujjinga wewe,yaani sababu kipenzi chenu kimaenasa mtegoni ndio iwe kawaida!!!!!

Jingazzz saaaaanaaa
 
Aliyoandika. Dr.Kitila Mkumbo kwenye gazeti la Raia mwema.
********************
Tunahitaji mbadala wa CCM, CHADEMA
Kitila Mkumbo
Itaendelea wiki ijayo..

Mbadala wa CDM? Kwa hiyo mabadiliko 2013 ilikuwa ni kuleta mbadala wa CDM? Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri nia ni kuleta chama kingine cha siasa ili kiwe mbadala ! Kama ni hivyo viongozi na wanachama wote wa CDM wanahaki zote kuwaita wasali, wahaini kwani nia yenu ilikuwa kuuwa CDM na kuanzisha mbadala. Je huoni mlikuwa hamuwatendei haki wale waliokubaliana na CDM, sera, taratibu , katiba, nk. Ni vyema mkaanzisha mbadala mkaendesha kwa vile mnavyoona inafaa ndio maana ZZK anatakiwa atoke mwenyewe kama anafikiri kama unavyofikiri asisubiri tsunami kwani lazima imbebe.
 
Tumeikataa CCM kwasababu inakumbatia makosa kwa kuogopa watu eti watayumbisha nchi. Lazima tujifunze kutoa adhabu na kupokea adhabu lazima tuanze na ZZK ili kutengeneza std zinazokubalika. NCCR haikuwa taasisi ilikuwa ni viongozi wenye uchu mkubwa sana wa madaraka na fedha, usalama wa taifa nk. Mazingira yamebadilika sana hatuwezi kuacha kuadhibiana kwa kuogopa kivuli cha NCCR. Dr ingebidi kwanza useme wazi je kwenye sakata lenu kwa vyovyote vile mlivunja katiba ya chama na kama mlivunja adhabu yake ilikuwa nini kwa mujibu wa katiba?

Lazima tuzifuate sheria zetu tulizokubaliana nazo. Sioni upofu wa wanachama ila naona tamaa ya tuliowaamini.

Alikuwa amekaa kimya nikadhani amekubali kosa na anaelekea kuomba radhi kumbe bado anajiona ana haki!!!!!
 
Mbadala wa CCM ni CHADEMA, na CHADEMA haijawa na mbadala bado na ili awepo inabidi kusota kwanza nje, Kitila anza kuchakalika, ila siku zote katika harakati zako fahamu chama cha kufukuzana ni kizuri kuliko chama cha kulindana.
 
Back
Top Bottom