Dr. Kitila amkana Dr. Slaa

Dr. Kitila amkana Dr. Slaa

Dr Slaa anakiwanda cha uongo

Ni aibu kwa mtu aliyewahi kuwa mtumishi wa Mungu kusema uongo kwa taifa zima tena akizungukwa na wapika uongo wenzake

Mnyika anajidhalilisha kukaa na lile genge la wahuni wapika uongo

Mbowe na Dr Slaa mtuachie chama chetu na mumchukue na lema mwende nae

Fafanua mkuu waende nae wapi?
 
kwani alihojiwa na Dr. Slaa au kamati?
Dr. Slaa ni msemaji tu, halafu aliyekiripotiwa zitto kukiri kuufahamu ule waraka ni Samson Mwigamba, siyo Dr. Kitila Mkumbo.
It seems amechanganyikiwa sana.
Kisaikolojia anateseka sana.

Ndicho mlichokuwa mnataka, mnafurahi kumchanganya mwenzenu kisaikolojia. Kuchanganya watu kisaikolojia ni kazi ya wachawi... do the math!
 
kwa slaa hakuna cha kushangaa, maana hata alipoulizwa juu ya kuondoa kifungo cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya chadema alikana kuwa katiba yao haijawahi kuwa ni kifungo hicho tangia mwanzo. kwa kifupi umri umemtupa mkono na kumbukumbu zinapungua kila siku.

Kitila amruka Slaa

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo amesema kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa kuwa alikiri kwamba Zitto alikuwa akiujua waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, ni za kutunga.

Juzi, wakati akieleza uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kuwafukuza uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Dk Kitila, Dk Slaa alisema wakati akihojiwa na Kamati Kuu, Dk Kitila alisema Zitto alikuwa akiujua waraka huo.

"Siyo kweli. Hata siku moja sijawahi kukiri kwamba Zitto alikuwa akiufahamu waraka, kilichosemwa na Dk Slaa ni uongo."

Mwigamba afafanua

Mwigamba alisema hakuhojiwa na Kamati Kuu kwa sababu yeye ni Msabato na Siku ya Sabato, hairuhusiwi kufanya jambo lolote zaidi ya kumwomba Mungu. "Waliniita Ijumaa (Januari 3) ili nihojiwe lakini mpaka saa 12 jioni sikuwa nimehojiwa na niliwaeleza kuwa jua likizama sitakubali kuhojiwa kwa sababu itakuwa imeanza Siku ya Sabato," alisema.

Alisema kikao cha Kamati Kuu kiliendelea Januari 4, mwaka huu, pia hakuweza kwenda kuhojiwa kwa sababu ilikuwa Sabato, pia alikuwa kanisani, "Niliwaambia kuwa nipo tayari kuhojiwa Jumapili, hawakunijulisha kama wameridhia."
 
Dr Slaa anakiwanda cha uongo

Ni aibu kwa mtu aliyewahi kuwa mtumishi wa Mungu kusema uongo kwa taifa zima tena akizungukwa na wapika uongo wenzake

Mnyika anajidhalilisha kukaa na lile genge la wahuni wapika uongo

Mbowe na Dr Slaa mtuachie chama chetu na mumchukue na lema mwende nae

Kwa nini "unadhani" na kuamini kirahisi tu kuwa Dr Slaa ndiye mwongo na si huyu Dr Kitila Mkumbo?..Si ktk kikao cha CC - CHADEMA kila kitu kilikuwa recorded (visual & audial)?... Je, huyu Daktari Mkumbo akiwekewa sauti yake hapa ya mahojiano yake yote na CC ataikana na wewe kumwomba radhi Dr Slaa mtumishi wa Mungu,Rais ajaye na mwanasisa mahiri?

Hii hata mimi nimeisoma hii habari ktk gazeti la Mwananchi front page la leo; sikushangaa sana kwa sababu Denis Msacky ni miongoni mwa wahariri wa gazeti hilo na tunafahamu mahusiano ya huyu bwana na kina ZZK,Mwigamba na huyu Dr Mkumbo......Nahisi D. Msacky ndiye M2 ktk waraka ule!!
 
Nitaongea saa nane mungu wangu yupo pamoja na wanyonge sio wabana democrasia wasiotaka kupingwa kwenye madaraka wanayoshikilia
 
Nani kaisifia CCM?naichukia sana CCM na bila shaka nilianza kuichukia CCM ata kabla hujajua siasa ni nini LAKINI pamoja na chuki yangu hiyo lakini nautambua ukweli mchungu kuwa hii CCM Mbovu bado ni bora maradufu kuliko Chadema ya Mbowe na Slaa.Na uchaguzi wa kutoka kwenye "kibovu" kwenda kwenye "kibovu zaidi" sio uchaguzi wa mtu mwenye akili timamu.

Chadema ilikuwa na nafasi ya kujijenga kuwa tayari kutawala lakini ndio kwanza ipo busy kujidhatiti kwenye ubovu,tutaisaidiaje sasa?Tanzania itakuwa hovyo zaidi chini ya hii Chadema ya Mbowe/Slaa/Lema/Sugu/Msigwa kuliko ilivyo chini ya CCM ya Kikwete/Sitta/Membe/Mwakyembe/Magufuli.

Hujui hata unachokiandika hapa ni nini bias mkubwa wewe!Why CCM unawataja tu walio bora lkn CHADEMA unawataja unao ona wewe sio bora?Why usifananishe na CHADEMA ya Prof Safari;Prof Baregu,John Mnyika na wengineo!Why usiitaje CCM ya akina Lusinde,Prof Kapuya,Madabida,Rage na wengineo wa hovyohovyo?

CHADEMA ni chama bora mara 100 kulinganisha na CCM na uchaguzi ujao wa madiwani CCM imeisha poteza viti 2 hadi sasa Sombetini-Arusha na Bunda!

Mbuni hizi za zamani za divide and rule zilizoisambaratisha NCCR na TLP zimepitwa mno na wakati na kama CHADEMA ilivuka kizingiti kigumu cha kuwahusisha na ugaidi chini ya architect Zitto na Mwigulu itakufa vipi kwa hoja za kitoto kama hizi za Zitto?
 
Una uhakika kuwa Dr. Kitila alisema ukweli?

Kwenye press conference pale Serena, alikanusha, tatizo Slaa na Chadema kwa kutumia waraka Zitto hawamkamati kwa hivyo wanabwawaja mambo yasiyokuwa kwenye charge sheet.
 
mkuu nyie hamuaminiki. kuwapa detail zake yanaweza yakamkuta yaliyomkuta yona, yule chairman wa temeke.

Tunaomba namba ta kadi yako na tawi lako na jina la mwenyekiti wa tawi lako ndiyo tuthibitishe kuwa wewe kweli ni mwanachadema, vinginevyo wewe ndiyo tuachie chama chetu.
 
Mhadhiri wa Chuo kikuu na Mjumbe wa Kamati Kuu leo amekuwa sisimizi?
Gongo mbaya sana ndo nimeanza kuelewa.
Haya wewe Tembo unanafasi gani chadema na Tanzania?

kwa hiyo wewe unamuona Goliath kwa kuwa ni mhadhiri wa chuo kikuu? mbona una reason kitoto sana.
 
Dr Slaa anakiwanda cha uongo

Ni aibu kwa mtu aliyewahi kuwa mtumishi wa Mungu kusema uongo kwa taifa zima tena akizungukwa na wapika uongo wenzake

Mnyika anajidhalilisha kukaa na lile genge la wahuni wapika uongo

Mbowe na Dr Slaa mtuachie chama chetu na mumchukue na lema mwende nae

'' ...Mbowe na Dr Slaa mtuachie chama chetu..''

Chama chenu wewe na nani?! Hivi unaijua CHADEMA wewe?!
 
Huyu padri analaana uongo yeye,uzinzi yeye halafu eti awe Rais! Labda raisi wa JF.

Sent from my Tab-G777 using Tapatalk

uzinzi wake umeujuaje?au alishavuruga familia yenu wote,by the way wewe unae waita wenzako nasty names u msafi?
 
Nani kaisifia CCM?naichukia sana CCM na bila shaka nilianza kuichukia CCM ata kabla hujajua siasa ni nini LAKINI pamoja na chuki yangu hiyo lakini nautambua ukweli mchungu kuwa hii CCM Mbovu bado ni bora maradufu kuliko Chadema ya Mbowe na Slaa.Na uchaguzi wa kutoka kwenye "kibovu" kwenda kwenye "kibovu zaidi" sio uchaguzi wa mtu mwenye akili timamu.

Chadema ilikuwa na nafasi ya kujijenga kuwa tayari kutawala
lakini ndio kwanza ipo busy kujidhatiti kwenye ubovu,tutaisaidiaje sasa?Tanzania itakuwa hovyo zaidi chini ya hii Chadema ya Mbowe/Slaa/Lema/Sugu/Msigwa kuliko ilivyo chini ya CCM ya Kikwete/Sitta/Membe/Mwakyembe/Magufuli.

Chini ya Ue-nyekiti wa ZITTO ZUBEIR KABWE na katibu mkuu akiwa DAVID KAFULILA nini mkuu??

Mimi nasema na kukataa kwa VERY BIG NO kwa sababu FREEMAN AIKAEL MBOWE (The National CHADEMA chairperson) and DR WILBROAD PETER SLAA (The national Party General Secretary) are still the right persons to take us where we are dreaming at!!. Ushahidi ni kuangalia CHAMA kilipokuwa about seven years ago, na kipo wapi sasa chini ya viongozi hawa. Hiki ndicho kipimo chao na si haya mengine ambazo ni propagations tu toka CCM wakisaidiwa na ninyi mliovaa ngozi za kondoo na kujifanya mlizijua siasa kabla wengine hatujaliwa kumbe ni madubu!!.....Na hii ndiyo hofu yenu na CCM "uwepo wa hawa jamaa kama viongozi wa chama hiki"..............Hii ni OPERSHENI YA MACCM WALIYOIPA JINA LA "TOKEMEZA DR SLAA na MBOWE CHADEMA TUWEKE WATU WETU" waendelee kutawala kiulaini tu, but nakuhakikishishia bro hii operesheni yao itawatokemeza wao CCM na mamluki yao yaliyo ndani ya CHADEMA kwani enzi zile wanatumia mbinu hii kudhoofisha CUF au NCCR mageuzi wengine tulikuwa bado tumelala,shule za kata za Lowassa zikatuamusha sasa tumeamuka tuko macho peee na ni kupambana mbele kwa mbele haogopwi mtu hapa,si CCM,polisi,katibu kata au siju Wassira au Nchemba Mwigulu yule jamaa - mbunge wa huku kwetu Iramba magharibi CCM (Singida) aliye kuja na mbinu ya kuingamiza chadema kwa "the so called ugaidi" akaangukia pua puu anavuja damu mpaka leo!!

MBOWE,DR SLAA,MSIGWA,TUNDU LISSU,SUGU,WENJE MNYIKA and all others fight,fight till the last drop of your blood keeping in mind that..............THE BIG ARMY on land,Air and ocean IS BEHIND YOU!!

Rejea historia ya vyama vya upinzani wewe tangu mwaka 1992 utaelewa ni nini CCM is capable of doing; but this time wamekwaa "kisiki cha mpingo" na si kila siku ni jumanne kama leo, na pia MUNGU SI IMANYARA mkuu!!
 
Sio kwamba wote wanaomtetea Zitto wako CCM!! Sema tu mmesha karirishwa kwamba mtu akipinga mawazo ya Mbowe na Slaa nyie mnasema anatumika CCM. Sis wengine tunamtetea Zitto b'se hatuoni kosa kubwa la Zitto kupelekea yeye kufukuzwa! Hawa viongoz wetu wa juu CDM wanamgogoro wao tu binafsi; Ilikua ni suala kutatua migogoro ya kwa njia ya mazungumzo, sio kupakaziana uongo na kufukuzana uanachama! Hawa CCM nao kumtetea Zitto ni kutaka kuchochea tu mgogoro ndan ya CDM, japo WANACHADEMA hatulitambui hilo, leo hii wampende Zitto kwa lipi? Tope la ufisad aliloipaka CCM litafutika lini?!! Ndugu wana CDM let us think beyond...!

Hili jambo linanikera hata mimi. Sijawahi kuwa mwanachama wa ccm wala CDM, bali napenda sana mabadiliko. Simjui Zitto, wala Mbowe wala yoyote. Na isitoshe siishi Tanzania na sitegemei ccm ili kuishi,nashangazwa sana na ukionyesha mtizamo tofauti unapewa chama hapohapo kuwa CCM, khaaa! Binafsi naichukia sana ccm na nikipewa uanachama hata wa jukwaani huwa inanikera. Wana CDM heshimuni mawazo ya wengine si kweli kwamba sote ni ccm. Nalisema hili kwa dhati kabisa ya moyo wangu. Hao ccm wanaomsapoti zitto bila shaka wana ajenda yao. Ila binafsi sina agenda yyte ila napenda kuona demokrasia ya kweli CDM isiwe copy & paste ya CCM
 
Kwa harakaharaka kundi linalomwona zitto kama msarit asilimia 90 lazima watokee kanda ya kaskazin na hata ukifuatia kwa makin elimu Zao ni std 7 mpaka kidato 6 kama hukubalian na mm una matatizo
 
Lazima tuende hivihivi,tupambane hivihivi kwa mfumo wa kidemokrasia huuhuu uliopo sasa hata kama ni wa kukopi na kupesti toka CCM,lakini lazima tuende pamoja na tukiupata ushindi, we create our own democracy!!. Hiyo demokrasia unayoidhania wewe kwa sasa haipo mkuu,labda CHADEMA ife kwanza ndo tuanze kuitafuta!!

Na kuitwa CHADEMA/BAVICHA au CCM/LUMUMBA/LB7 isikukere,isikutishe bhanaa coz whether you like or not ktk mfumo wa kisiasa tulionao ni lazima utakuwa ktk upande ulioshindwa au kushinda!,. Vita ndo imepamba moto twendeni tusonge mbele,lazima CCM iondoke,pambana ujuavyo wewe kama unahitaji mabadiliko ya kweli ktk nchi hii,waambie wanakijiji/wanafunzi/wanamtaa wenzako sasa ni wakati wa mabadiliko...THE CHANGES WE ARE TALKING HERE IS KUINDOA CCM NA MFUMO WAKE WOTE KTK RAMANI YA USO WA VYAMA VYA SIASA!!...... USHINDI U KARIBU!!
 
Hawa watu wanataka nini CDM? Wameshafukuzwa kelele za nini sasa,wapeleke taarifa kwa aliyewatuma kuwa ishu imefeli........tumechoka na mipayuko.
 
Kwa harakaharaka kundi linalomwona zitto kama msarit asilimia 90 lazima watokee kanda ya kaskazin na hata ukifuatia kwa makin elimu Zao ni std 7 mpaka kidato 6 kama hukubalian na mm una matatizo

Atakayekubaliana na wewe Buku7 ana matatizo, Tena makubwa kwelikweli!
 
Kitila amruka Slaa

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo amesema kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa kuwa alikiri kwamba Zitto alikuwa akiujua waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, ni za kutunga.

Juzi, wakati akieleza uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kuwafukuza uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Dk Kitila, Dk Slaa alisema wakati akihojiwa na Kamati Kuu, Dk Kitila alisema Zitto alikuwa akiujua waraka huo.

"Siyo kweli. Hata siku moja sijawahi kukiri kwamba Zitto alikuwa akiufahamu waraka, kilichosemwa na Dk Slaa ni uongo."

Mwigamba afafanua

Mwigamba alisema hakuhojiwa na Kamati Kuu kwa sababu yeye ni Msabato na Siku ya Sabato, hairuhusiwi kufanya jambo lolote zaidi ya kumwomba Mungu. "Waliniita Ijumaa (Januari 3) ili nihojiwe lakini mpaka saa 12 jioni sikuwa nimehojiwa na niliwaeleza kuwa jua likizama sitakubali kuhojiwa kwa sababu itakuwa imeanza Siku ya Sabato," alisema.

Alisema kikao cha Kamati Kuu kiliendelea Januari 4, mwaka huu, pia hakuweza kwenda kuhojiwa kwa sababu ilikuwa Sabato, pia alikuwa kanisani, "Niliwaambia kuwa nipo tayari kuhojiwa Jumapili, hawakunijulisha kama wameridhia."
Hapa tunapaswa kukiri wote kama wana familia ya CHADEMA kuwa tumeshindwa wote ktk vita hii......nitafafanua. Ktk kila ugomvi wa kifamilia Baba mwenye busara inapotokea watoto wake wameumizana ni lazima nae aumie siyo tu kimwili bali hata kihisia kuwa ameshindwa kuitunza familia yake vizuri mpaka watoto wakafika hatua ya kuumizana. Kuchukua majukumu ya kibaba ni lazima mzazi mwenye hekima ajilaumu mwenyewe kwa kutoweza kugawanya keki ya familia ktk uwiano sawa hadi ugomvi ukazuka. Kugombana maana ni kushindania kidogo kilichoonekana. Je, inawawezekana kuwa kuna kikubwa kilifichwa kidogo kikagombaniwa mimi na wewe hatujui. Lkn kama wazazi tunapaswa kuwa waadilifu ili hata hicho kidogo kilichopatikana basi kigawanwe ktk misingi ya haki bila mizengwe na hiyo ndiyo itatuweka kwenye safe side. Otherwise leo ni Zitto, Kitila Mkumbo na Mwigamba lkn kesho anaweza kuwa Lema, Mnyika na mtu mwingine. Tujifunze kuwa watu wa kutosheka. Kutosheka haina maana kuwa tutakuwa tayari matajiri la hasha! Tujifunze kwa majirani zetu Zaire ya zamani na Mabutu wao. Tumkumkumke Hayati Baba wa Taifa, pamoja na umasikini aliokuwa nao lkn akawa mtu wa kutosheka. Akafikia wakati anataka kujengewa nyumba na jeshi letu anauliza nyumba hiyo yote mimi ni Tembo? Je, Nyerere hakujua kuwa ana familia kubwa iliyopaswa kurithi mali zake? Hapana alijua yote hayo lakini kwa kuwa alikuwa mtu wa kiasi basi alifanikiwa kujitawala nafsi yake na ndiyo maana linapokuja suala la uadilifu sisi vijana na wazee wa nchi tunapojiangalia tunajiona hatujitoshi kwa Nyerere na Kawawa tukiwataja kwa uchache bila kusahau jembe la kazi Sokoine. Hatupaswi kujilinganisha lkn linapokuja suala la nani atuongoze katika nchi namlinganisha na Sokoine na ndugu yetu mmoja ambaye kila kukicha yuko makanisani na misikitini akitoa misaada kama kwamba alishaambiwa tunataka rais wa misaada au rais wa makanisa au misikiti. Hivi huko makanisani hakuna vyeo vinavyo endana na maeneo hayo? Hivi Mapadri, Maaskofu na Mapapa si vyeo vya makanisa jamani? Kwa nn huyu anayepita huko mara kwa mara asigombee hivyo vyeo huko na misikitini hali kadhalika?
Kwa jinsi anavyowajua Watanzania najua alisha fanya utafiti wake akagundua kuwa ili uwaibie Watanzania kwa urahisi basi jifanye mtu wa dini tu. Hatujaona mpaka wahaeshimiwa wasio washemiwa siku hizi wanamilki makanisa makubwa lkn kinachoendelea huko ni Mungu mwenyewe anajua?
Mwisho nimalize kwa kuwasihi wanaCHADEMA wote kuwa kama tulikuwa wanachama 100 sasa idadi yetu imepungua. Maana yake ni kwamba ikitokea mtu anataka kutupatia msaada wowote kwa masharti kuwa ni lazima tuwe 100 basi huo msaada tumeukosa. Kwa hiyo si kitu cha kufurahia kuwapoteza wanachama hata kama ni mmoja bali wote tunapaswa kujihoji kwa ujumla wetu kuwa tumekosea wapi na nn kimetusibu wakati huu tunaoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Mwisho kabisa napenda kumshukuru Mh. Wasira kwa busara zake za kiutu uzima kuwakumbusha CHADEMA kuwa itakufa kabla ya 2014. Tunakushukuru Mh. maana angalau tunaweza kupata muda wa kujipanga japo nafikiri hayo uliyatoa si kwamba unatupenda la hasha ni kwa sababu ulishindwa kudhibiti domo lako na kupenda sifa kwenu Magamba. Ulifanya hivyo ili kujiboost maana inawezekana jina lako halikuwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu so ukatafuta pa kutokea usijue kuwa unatoa siri za chama chenu cha Magamba a.k.a CHUKUA CHAKO MAPEMA NA TAMBAA.
Napita tu jamani mm mwenyewe mgeni. Nahaurumia kucha na meno yangu!!!!!!!!!!!! MAGAMBA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!
 
Back
Top Bottom