Dr. Kitila amkana Dr. Slaa

Dr. Kitila amkana Dr. Slaa

Siku moja utajua kuwa kwa Dr Slaa uongo ni sehemu ya maisha yake ya kila siku.Zamani na mie nilikuwa kama wewe,siku moja utakuja kufahamu hili.

Uongo wa Dr Slaa ndiyo unesababisha UMEME upande kwa 78%?

Tuvulana tujinga tunapiga kimaisha lkn bado tu wapo kuisifia CCM!Matatizo haya tuliyo nayo ya watoto wetu kusomea madarasa ya nyasi hajaletwa na Mungu!
 
kwani alihojiwa na Dr. Slaa au kamati?
Dr. Slaa ni msemaji tu, halafu aliyekiripotiwa zitto kukiri kuufahamu ule waraka ni Samson Mwigamba, siyo Dr. Kitila Mkumbo.
It seems amechanganyikiwa sana.
Kisaikolojia anateseka sana.

Wewe ndio umejichanganya...Ni Dr Slaa ndiye aliyeongea na Umma kuwa Dr Kitila amekiri ndani ya kikao kuwa Zitto alikuwa anataarifiwa juu ya waraka ule.

Kumbuka:Mwigamba hakuhojiwa na kamati kuu kwa sababu ya kamati kuu kung'ang'ania kumhoji wakati wa Sabato kinyume na imani yake.
 
Uongo wa Dr Slaa ndiyo unesababisha UMEME upande kwa 78%?

Tuvulana tujinga tunapiga kimaisha lkn bado tu wapo kuisifia CCM!Matatizo haya tuliyo nayo ya watoto wetu kusomea madarasa ya nyasi hajaletwa na Mungu!

Nani kaisifia CCM?naichukia sana CCM na bila shaka nilianza kuichukia CCM ata kabla hujajua siasa ni nini LAKINI pamoja na chuki yangu hiyo lakini nautambua ukweli mchungu kuwa hii CCM Mbovu bado ni bora maradufu kuliko Chadema ya Mbowe na Slaa.Na uchaguzi wa kutoka kwenye "kibovu" kwenda kwenye "kibovu zaidi" sio uchaguzi wa mtu mwenye akili timamu.

Chadema ilikuwa na nafasi ya kujijenga kuwa tayari kutawala lakini ndio kwanza ipo busy kujidhatiti kwenye ubovu,tutaisaidiaje sasa?Tanzania itakuwa hovyo zaidi chini ya hii Chadema ya Mbowe/Slaa/Lema/Sugu/Msigwa kuliko ilivyo chini ya CCM ya Kikwete/Sitta/Membe/Mwakyembe/Magufuli.
 
Kitila amruka Slaa

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo amesema kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa kuwa alikiri kwamba Zitto alikuwa akiujua waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, ni za kutunga.

Juzi, wakati akieleza uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kuwafukuza uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Dk Kitila, Dk Slaa alisema wakati akihojiwa na Kamati Kuu, Dk Kitila alisema Zitto alikuwa akiujua waraka huo.

“Siyo kweli. Hata siku moja sijawahi kukiri kwamba Zitto alikuwa akiufahamu waraka, kilichosemwa na Dk Slaa ni uongo.”

Mwigamba afafanua

Mwigamba alisema hakuhojiwa na Kamati Kuu kwa sababu yeye ni Msabato na Siku ya Sabato, hairuhusiwi kufanya jambo lolote zaidi ya kumwomba Mungu. “Waliniita Ijumaa (Januari 3) ili nihojiwe lakini mpaka saa 12 jioni sikuwa nimehojiwa na niliwaeleza kuwa jua likizama sitakubali kuhojiwa kwa sababu itakuwa imeanza Siku ya Sabato,” alisema.

Alisema kikao cha Kamati Kuu kiliendelea Januari 4, mwaka huu, pia hakuweza kwenda kuhojiwa kwa sababu ilikuwa Sabato, pia alikuwa kanisani, “Niliwaambia kuwa nipo tayari kuhojiwa Jumapili, hawakunijulisha kama wameridhia.”
Kama habari hizi ni kweli basi Dr.Slaa na Kamati kuu ya Chadema mna matatizo makubwa, na mjipime wenyewe kabla ya mwaka 2015 kama mnafaa kuitwa wanademokrasia na wana maendeleo
 
1. Hakuna institution itayoendelea kwa kuentertain mawazo yanayofanana tu. Hapa nakubaliana naye
2. Zitto akienda chama kingine will gain momentum and CHADEMA will fall. Anatoa mfano wa mrema miving to TLP from NCCR Mageuzi. Hapa naona kama anaota vile.
NB. He seems to struggle to regain psychological relief.
Kwenye Chai asubuhi hii hapa Utawala UDSM

Chai wakati mi course work haisomi kabisa, joho lileee
 
lini aliwahi kuwa mkweli!???.................wote wanafiki nafiki tu.------- zao!!
 
Hata aruke nauli mía, Zitto ndiye aliratibu oasis yote. Let us wait time will tell.
 
Hata aruke mara mía, Zitto ndiye muasisi wa issue yote, tungoje time will tell
 
Mfa maji haishi kutapatapa ...naona wanahangaika tu hawa watu
 
mtu wa kufuata mkumbo wakati mwingine hakumbuki alichosema mpaka muda upite na mkumbuke yeye alikuwa mfuasi wa masalia na wasaliti si ajabu mwizi kukataa wizi wake na msaliti kukana kauli zake ndivyo walivyo
 
Sio kwamba wote wanaomtetea Zitto wako CCM!! Sema tu mmesha karirishwa kwamba mtu akipinga mawazo ya Mbowe na Slaa nyie mnasema anatumika CCM. Sis wengine tunamtetea Zitto b'se hatuoni kosa kubwa la Zitto kupelekea yeye kufukuzwa! Hawa viongoz wetu wa juu CDM wanamgogoro wao tu binafsi; Ilikua ni suala kutatua migogoro ya kwa njia ya mazungumzo, sio kupakaziana uongo na kufukuzana uanachama! Hawa CCM nao kumtetea Zitto ni kutaka kuchochea tu mgogoro ndan ya CDM, japo WANACHADEMA hatulitambui hilo, leo hii wampende Zitto kwa lipi? Tope la ufisad aliloipaka CCM litafutika lini?!! Ndugu wana CDM let us think beyond...!

Zito alionyesha wazi nia ya kutaka kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni, kosa la kwanza, alikusudia wazi wazi kugombea Uenyekiti, la pili, na aliumbua vyama vyote vya Siasa kwa niaba ya wananchi, vilivyo amua kufanya 'ruzuku' ni pocket money !
 
Dr.Kitila, nakushauri ukame kimya kwa muda ili uweze kujitafakari na uweze kutengeneza mwelekeo wako, kwani unapojaribu kusema uongo ni hatari siku Cd zilizotekodiwa kwenye kikao zikiwa kwa hadharani utapoteza hata ile credibility ndogo uliyobakia nayo v hata wanafunzi wako watakupuuza ........
Mahojiano yake yalirekodiwa na anajua hivyo, sasa kupotosha haitakusaidia kwa hatua za sasa .
 
Hawa wahaini watateseka sana na kinachofuata wataanza kuokota makopo.
 
Things will never be the same again kwa CHADEMA. Huo ndio ukweli. Kila tukio hasi linalotokea nhuacha athari nyuma yake.
 
Ndo tatizo lenu mzinzi munamuona kama malaika, nawewe lazima uwe Shirima au Masawe.

1. Bosi wako Zitto ana miaka 37 hajaoa, amezaa mtoto nje ya ndoa- Yeye sio Mzinzi
2. Bosi wako Zitto amekuwa Naibu Katibu mkuu chademe kwa miaka zaidi ya 7- Yeye ni Njau, Massawe au Urassa

Wewe UNACHUKI na CHADEMA, Lazima utakuwa ni MHA.
Wewe una mke mmoja, hujawahi kutoka nje ya ndoa wala hujawahi kusalitiwa-WEWE SIO MZINZI.

Asante
 
Binafsi hainiingii akilini, waraka uandaliwe kwa ajili ya zitto kuwa mwenyekiti halafu yeye(zitto) asiambiwe! Huu ni uwongo wa mchana kweupe!
 
Kitila amruka Slaa

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo amesema kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa kuwa alikiri kwamba Zitto alikuwa akiujua waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, ni za kutunga.

Juzi, wakati akieleza uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kuwafukuza uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Dk Kitila, Dk Slaa alisema wakati akihojiwa na Kamati Kuu, Dk Kitila alisema Zitto alikuwa akiujua waraka huo.

“Siyo kweli. Hata siku moja sijawahi kukiri kwamba Zitto alikuwa akiufahamu waraka, kilichosemwa na Dk Slaa ni uongo.”

Mwigamba afafanua

Mwigamba alisema hakuhojiwa na Kamati Kuu kwa sababu yeye ni Msabato na Siku ya Sabato, hairuhusiwi kufanya jambo lolote zaidi ya kumwomba Mungu. “Waliniita Ijumaa (Januari 3) ili nihojiwe lakini mpaka saa 12 jioni sikuwa nimehojiwa na niliwaeleza kuwa jua likizama sitakubali kuhojiwa kwa sababu itakuwa imeanza Siku ya Sabato,” alisema.

Alisema kikao cha Kamati Kuu kiliendelea Januari 4, mwaka huu, pia hakuweza kwenda kuhojiwa kwa sababu ilikuwa Sabato, pia alikuwa kanisani, “Niliwaambia kuwa nipo tayari kuhojiwa Jumapili, hawakunijulisha kama wameridhia.”

Ili miili isilalale msalabani siku ya SABATO walimuomba Pilato miguu yake ivunjwe
 
Back
Top Bottom