Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,485
NImesoma magazeti na kuangalia luninga za nyumbani na mara kwa mara wameanza au wamepania kumtambulisha Kikwete kwa cheo cha Udaktari wa Heshima. Nikajiuiliza kama wanafanya hivyo kwa sababu yeye mwenyewe anataka wawe wanafanya hivyo au wanafanya hivyo kwa sababu wanapaswa kufanya hivyo? Siyo Kikwete tu bali wanafanya hivyo kwa Karume vile vile.
Nafahamu wote wawili wametunukiwa shahada hizo za heshima. Lakini ukizingatia kuwa wanakuwa kwenye habari mara kwa mara kuna umuhimu wa kuwaita hivyo kila wakati? Mbona Mkapa hawamuiti hivyo au Nyerere?
NI kwanini Wamarekani hawamtambulishi Obama kama Dr. Obama au Prof. Obama?
Labda inamsaidia kisiasa na kimtazamo mbele ya wananchi (maana ana shahada moja tu ya kusomea)..
Kama hilo ni kweli, kwanini wasiongezee na vyeo vya Luteni Mstaafu Dr. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki?
Mimi naamini kuna wakati ambapo angeweza kutumia cheo hicho cha kitaaluma kwa ujiko kama siku moja akiwa na ujasiri wa kwenda kuzungumza na wasomi wa chuo kikuu kimoja nchini basi hapo mnaweza kumtambulisha kama Dr. Kikwete. Maana siwezi kufikiria kwenye mikutano ya kimataifa wakimtambulisha kama Dr. Kikwete anajisikiaje mbele ya ma Dr. wenyewe?
Ila kama inamfanya ajisikie vizuri.. more power to him..