Dr Kijazi: Kutakuwa na upungufu mkubwa wa mvua za mwisho wa mwaka, wakulima chukueni tahadhari!

Ni 'kutakuwa' au 'imeshaanza kuwa?'...sio kwamba hiki ni kipindi tulipaswa tayari kupata mvua?.

Na hizo tahadhari zingetajwa kabisa.

Bila ya shaka miongoni mwao ni ugeni kutoka huko Mbugani, hao Viumbe wenzetu kina Tembo na wenzao wakikosa malisho na maji hakika watakuja mjini tugawane kilichopo.
 
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Dr Kijazi amesema kutakuwepo na upungufu mkubwa wa mvua za mwisho wa mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo Wakulima wanapaswa kuchukua tahadhari.

Source: ITV habari
Dr Kijazi huwa hastaafu.....na yule wa tanapa pia au hawa huwa hawazeeki basi sawa
 
Tuchukue tahadhari gani sasa? Maana tumezoea kuchukua tahadhari kama mvua zitakuwa kubwa. Mafuriko nk.


1. Tuepuke kuingia gharama ya kuandaa mashamba ili hali mvua itakuwa ya mashaka.

2. Pia iwapo mvua zitanyesha chache basi tupande mbegu za muda mfupi.

3. Kuweka akiba ya chakula kilichopo tusikimalize ktk kucheza wali ngoma na harusi.
 
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Dr Kijazi amesema kutakuwepo na upungufu mkubwa wa mvua za mwisho wa mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo Wakulima wanapaswa kuchukua tahadhari.

Source: ITV habari

Kutegemea mvua za msimu kwa kilimo huu ni umasikini wa fikra...

Ipo mito mikubwa ambayo inatiririsha maji kwenda baharini na ktk maziwa... Kungekuwepo na mabwawa makubwa kwaajiri ya kutunza maji kwa kilimo na matumizi mengine...
 
Back
Top Bottom