Dr Kigwangala aikemea CCM na kuikubali UKAWA

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,566
Reaction score
28,729
Dr Kigwangala ameitahadharisha CCM kuwa makini na nguvu za UKAWA kufuatia kuinyanganya CCM 20% ya viti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi punde. Dr Kigwa aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha UZALENDO kinachorushwa na ITV.

Kigwangala alisema wananchi wa leo sio wale wa miaka 5 au 10 iliyopita. Ametumia nafasi hii kumuonya Rais Kikwete atekeleze maazimio yote ya bunge dhidi ya mafisadi wa ESCROW bila kusita kwani asipofanya hivyo anazidi kukididimiza chama wakati yeye muda wake unakaribia kuisha. "Rais asipotekeleza maazimio ya bunge anazidi kukiweka chama chetu katika wakati mgumu", alisema.

Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe amewaomba watu wa CCM kuacha kufanya siasa kwa mazoea na kwa kutumia hila na ujanjanja. Ameenda mbali zaidi kwa kuwataka CCM waache kuwakumbatia mafisadi kwani kufanya hivyo wanaweka rehani uhai wa chama.

Source: ITV

MAONI YANGU
Nampongeza Kigwa kwa kusema ukweli, tofauti na wanaCCM wengine wanaoubeza Muungano wa UKAWA.

:israel:
 
wapi LB7 akina Faizafoxy,lizaboni,simiyu yetu et all...!!!
Dr.Kigwa you have nailed...Wanahitajika watu realistic kama huyu ndani ya ccm
 
Kumbe anajua siasa za CCM ni za kiujanjajanja?
Wananchi wasipokomaa kwenye chaguzi huwa wanabadilisha kura.
 
Samahani mkuu, huyu jamaa ndio nani?. ingekuwa fresha kama ungetuambia ni nani na anamchango gani katika nchi hii
 
TV ya mengi mleta mada kijana wa mengi hatuwezi kupata habari nzuri hata kidogo.
 
he's matured enough....ame komaa kisiasa.
 
mimi nikiona mtu anasifia ukawa naanza kutilia mashaka akili yake siyo bure.
 
hapo kwenye mwanasiasa mkongwe ndipo Nina wasi wasi nao..unaonaje pakisomeka hivi..mwanasiasa kijana anae chipuka
 

Na sio 20% UKAWA wana 36% yaani ccm wana 64% tu kwa mujibu wa TAMISEMI, na hapo hujatoa walizoshinda kwa mapingazi. Ccm ni wazi inang'oka 2015.
 
TV ya mengi mleta mada kijana wa mengi hatuwezi kupata habari nzuri hata kidogo.

Kwa maoni yako habari nzuri inatoka wapi?
Ipi kwako ni habari nzuri?
 
Kama sio mizengwe na makundi ya wenye noti huyu ndiye mtu pekee wa ccm anayeweza kunitoa nyumbani kwenda kupiga kura wengine woote ni kama kuurudisha utawala wa sasa. Mda wa mtandao umeisha ,tukiuendeleza nchi yetu haitakalika.
 

Mtu aliyekaa darasani akaelimika lazima ajipambanue na waliohudhuria darasani kama Nape Nauye, Assumpter Mshama na Livingstone Lusinde.

cc: Dr, Prof. Hon JK, Mary Nagu, Lukuvi, Wassira etc..
 
hizo % za maccm nizakujifariji tu ccm ni mahututi anytime Natakiwa marehemu
 
Toa maoni nasio kuchangia utumbo sasa ww ulitaka achangie uzembe na utumbo was Ccm?
 

Yan jamaa kachangia vizuri sana kwa uzalendo na kwa uchambuzi bila kuegemea upande wowote hakika nampongeza sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…