Dr Kessy: Mitihani ya Tanzania inapima uwezo wa mwanafunzi kukariri siyo kuelewa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Akichangia mjadala katika kipindi cha Kipima Joto Dr Kessy anasema tatizo kubwa au changamoto kubwa tuliyonayo Watanzania ni pale Mitihani yetu ya taifa inapopima uwezo wa mwanafunzi wa kukariri na siyo uelewa wake.

Hali hii imepelekea taifa kupata Wasomi wa Vyeti na siyo wataalamu na watafiti, amesema.

Chanzo: ITV
 
Ni rahisi sana ondoa mambo ya kufanya mitihani ya kushindana elimu sio ushindani kama mbio ni kuwaelemisha watoto kinadharia na matendo zaidi na wacha waongelee topic tofauti na kuchangia utajuwa uwezo wa uelewa na kufikiri kwa watoto badala ya kuwapa pressure soma sana uwe number moja mwisho wa siku anakariri tu usiku na mchana anakuwa number moja baada ya hapo hakuna kitu. elimu lazima iwe katika uelewa zaidi maana mtoto akiongea tu unajuwa huyu kapevuka anajuwa mazingira yaliyo mzunguka ila sisi hata watoto wa KG unataka washindane unajenda stress kwa watoto isiyo ya lazima. Paper za kukariri hata kasuku ana kariri. Na kama mitihani basi wasiandike kama walivyosoma kwenye vitabu ila waandike kwa maneno yao kuonesha uelewa wao sio muhimu apatie grammar lakini kujuwa huyu kaelewa anachotaka kuandika majibu yasifanane.
 
Huyu dr.kessy ,hata yy alikuwa mzuri kwa kukariri ndo maana Leo anaitwa Dr.kessy !! we mtu umeikuta kitu iko hivi...log(axb)=loga + log b. Sasa hapa unataka uelewe nn!!!,unaambiwa hiyo ipogo hivo hivo,na ukijifanya mbishi Sasa wewe usikalili hivyo uone ,kama huja sapu!!
 
We jiulize wanafaulu kwenda secondary vizuri wakifika huko ndo inajulikana hawajui kusoma na kuandika na Serikali ipo kimya waziri wa elimu wala hilo halimshtui!

Sasa njoo waliomaliza form 4 au chuo kikuu yaani kama hao wa chuo kikuu ndo AIBU lakini taifa halishtuki wala kujiuliza .
Mi naamini ni mkakati wa serikali raia wasitoke kwenye UJINGA
Ref. Waziri wa mambo ya ndani upande kuajiri askari ndo kituko!
 
Akichangia mjadala katika kipindi cha Kipima Joto Dr Kessy anasema tatizo kubwa au changamoto kubwa tuliyonayo Watanzania ni pale Mitihani yetu ya taifa inapopima uwezo wa mwanafunzi wa kukariri na siyo uelewa wake.

Hali hii imepelekea taifa kupata Wasomi wa Vyeti na siyo wataalamu na watafiti, amesema.

Chanzo: ITV
Fact. Students should be encoraged to undestand concepts rather than memorizing unlogically.
 
Ninachoelewa mimi siku hizi waalimu wanafundisha jinsi/namna ya kufaulu mitihani siyo kuelewa unachofundishwa
Sidhani sema baadhi ya masomo

Wanaoenda kusoma udaktari au engineering swala la kukariri halipo .Masomo ya sayansi Hakuna ubabaishaji Ni ama unaelewa au huelewi full stop

Ndio maana unaona majengo yanajengwa na mainjinia wa kitanzania, hospital zina madaktari bingwa wa kitanzania nk

Lakini kwenye masomo ya arts nakubaliana wanakariri kariri tu akiwemo yeye mwenyewe Dk Kessy
 
Back
Top Bottom