Ubovu wa Elimu ya Tanzania

wililo

Member
Apr 25, 2015
78
27
Habari ndugu zangu!
Leo naomba kuongelea kidogo ubovu wa elimu ya TANZANIA hasa elimu msingi na sekondari.

Elimu yetu ya msingi na sekondari imekuwa na changamoto nyingi ambazo zimepelekea elimu hii isiwe chombo Cha ukombozi Kwa mwananchi. Changamoto hizo ni kama ifuatavyo:

1.Lugha ya kufundishia na kujifunza. Kwa elimu msingi wanatumia lugha ya kiswahili na mwanafunzi anapofika elimu ya sekondari anabadilishiwa lugha na kutumia kingereza lugha ya kigeni, jambo hili limefanya wanafunzi wengi wasome Kwa kukariri kuliko kuelewa Kwa sababu anapswa ajifunze lugha kwanza ndipo aanze kujifunza masomo. Hivyo mwanafunzi anakuwa na kazi mbili Kwanza ajifunze lugha ya kigeni ndani ya wiki 12 ndipo aanze masomo rasmi jambo si rahisi kulingana na muda wa kujifunza lugha kuwa finyu.

2. Mada zinazofundishwa haziendani na uhalisia wa mazingira yetu. Mambo mengi anayofundishwa mwanafunzi hayamfanyi aweze kukabiliana na changamoto zilizomo kwenye mazingira anamoishi, Kwani mambo mengi yamechukuliwa kutoka kwenye mazingira ya kigeni. Hususani masomo ya sayansi ambayo waandishi wengi wa vitabu ni kutoka mataifa ya kigeni.

3. Utitiri wa masomo. Mwanafunzi amekuwa akibebeshwa mzigo wa masomo ambayo kulingana na uwezo wa kiakili hawezi kuyamudu na hayawezi kumsaidia . mf. Elimumsingi anasoma masomo Saba Hadi nane, sekondari masomo Saba Hadi 12 ingekuwa vema mwanafunzi asome kulingana na uwezo wa akili na upendeleo wake!

4. Masomo kufundishwa Kwa nadharia. Vitu vingi vinavyofundishwa kwenye shule za msingi na sekondari ni nadharia na sio Kwa vitendo au kuona japo linalopunguza uelewa na umahili katika mada husika.

5. Kutaka kuacha historia Kwa viongozi. Mfumo wa elimu umekuwa ukiharibiwa na watawala wasiokuwa na ujuzi na suala la ufundisha, kumekuwa na mabadiliko ya mara Kwa mara kwenye mfumo wa elimu bila kujali adhari Kwa taifa hasa pale kiongozi mwenye dhamana anapotaka aache historia bila kuangalia faida ya mabadiliko hayo Kwa taifa. Mf. Kuunganisha fisikia na kemia, kuunganisha historia na jiografia, kuanzisha kalenda ya ufundishaji kama Misa, mikataba ya ufaulishaji kama mwalimu ndiye mwanafunzi.

6. Muda wa kukaa shule. Mwanafunzi anapoteza muda mwingi sana katika suala la kutafuta elimu jambo ambalo linachelewesha maendeleo Kwa familia na taifa.Mf. elimumsingi miaka 8, sekondari miaka 4, kidato Cha Tano na sita miaka 2 na chuo miaka 3 hadi 6. Mfumo huu ni wakikoloni ambao hauna tija Kwa taifa linalotaka kuendelea.

7. Upatikanaji wa vifaa vya kujifunza na kufundishia. Mitihani inayotungwa haiangalii mwanafunzi amesomea kwenye mazingira gani mtoto aliyepo kwenye mazingira bora na yule aliyepo kwenye mazingira hafifu wote wanapimwa sawa lakini pia shule zenye vifaa vyote vya kujifunzia na kufundishia zinapimwa sawa.

Mwisho. Kama taifa inatupasa kuwa na mfumo wa elimu wenye shabaha ya kukidhi mahitaji ya Taifa Kwa ujumla bila viongozi wetu kutafuta umarufu kwenye mambo ya msingi.
 
Fanya comparison plz unataka tuwe na mfumo wa elimu kama wa nchi gani? Je hiyo nchi imefanikisha? Kutaja unazo ziita chagamoto bila kutoa mbadala hujafanya lolote.
 
Hakuna mtu alizungumzia shida ya elimu ya Tanzania akaacha kuzungumzia lugha ya kingereza na kushauri kingereza kitumike katika masomo yote kuanzia chekechea

Ila kitu Cha kushangaza hao ambao wamepewa jukumu la kushughulika na mabadiriko ya mfumo wa elimu hili tatizo la lugha hawalioni

Cha kushangaza zaidi Kuna mmoja katika hiyo tume nimesikia anesema eti mwanafunzi akiingia secondary apewe mwaka mmoja wa kujifumza lugha ya kingereza Sasa shida yote hiyo ya Nini wakati morabaini wa hi shida ni kutumia kingereza kuanzia chekechea

Hi nchi waliosoma na wasiosoma wote ni vilaza tu
 
Back
Top Bottom