Uadilifu chanzo cha wizi wa mitihani na udanganyifu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,913
Taifa lenye watu wengi wasio na uadilifu ni kawaida sana kuwepo kwa wizi wa mitihani ama udanganyifu kwenye mitihani. Uadilifu ni zaidi ya mtu kutokuiba ama kusema uongo, uadilifu pia ni pamoja na mtu kujali maslahi ya wengi pale anapokuwa na cheo kwa niaba ya Umma.

watu waadilifu wataweka mifumo rahisi na yenye ubora kwa ajili ya watu kufanya mitihani na kusahihishiwa mitihani yao. watu waadilifu ni wale wanaojua kwamba mitihani inatakiwa iwe kipimo cha uelewa na siyo kipimo cha uwezo wa kukariri.

Ili mitihani iwe kipimo cha uelewa ni lazima watu waadilifu waweke mifumo inayofanya watoa elimu (Waalimu/wahadhiri) watimize wajibu wao wa kufundisha na kuhakikisha asilimia kubwa ya wanaofundishwa wanaelewa. Watu waaadilifu hawajivunii asilimia kubwa ya watu kufeli mitihani yao kuliko kufaulu.

Leo ni kawaida kabisa baadhi ya watahiniwa kuhonga, kuingia na majibu kwenye vyumba vya mitihani, kununua mitihani, kughushi vyeti, kutumia majina yasiyo yao na kadhalika na kadhalika. Wanaposhikwa ndipo jamii hushikwa na butwaa kama vile haijui kuna watu kama hao kwenye jamii yetu.
 
Nada kama hii ni ngumu kuchangiwa ila leta inayohusu kula mbususu kimasihara utaona matokeo. Nchi za Afrika kila mwananchi anaangalia tumbo lake na akipata upenyo ni mwendo wa kujilimbikizia kwa njia yoyote na hata mfumo wetu wa ajira unachangia wizi wa mitihani sababu kinachoangaliwa ni ufauli katika vyeti na hata kama Kuna usaili wa vitendo bado pelepeche ni nyingi.Mlisema tutafika tumechoka nataka niseme hakuna atakayefika tutazunguka na mwisho tutakufa na kuzikwa kibudu na juu ya makaburi watoto wetu wataweka mashine za kubet na vijiwe vya ndumu.
 
Back
Top Bottom