basa
JF-Expert Member
- Mar 21, 2012
- 252
- 383
tarehe 12 dec 2012, zaidi ya miezi miwili tangu mwaka wa masomo uanze,wanafunzi mwaka wa pili tuliokata tamaa na kuzoea kupiga pasi(lampard) ndefu tumeingiziwa boom pia na wanafunzi baadhi mwaka wa tatu waliofield wameingiziwa pesa zao, inhali wenzetu vyuo vingine wanazaidi ya wiki mbili tangu waingiziwe awamu ya piil, lakini kinachoumiza zaidi hata pesa yenyewe ilingizwa baada ya tishio la wanafunzi lilopelekea tatizo letu kumfikia waziri wa elimu na baada ya saa chache tukaingiziwa pesa ,lakini nyuma ya panzia kunamchezo mchafu unachezwa na baadhi ya maofisa wandamizi wa bodi kwani walitusainisha pesa kupitia afisa mikopo wa chuo toka tar 05/12 wakijua tunasiku chache kwenda likizo, cha ajabu zaidi ya wiki ikakatika mpaka hiyo jaana mara baada ya tatizo hilo kufikishwa kwa waziri ndo pesa ikaingizwa... inhali dada zetu wamejiuza, watu wameishi kwa kula mihogo na maji ya kuchemshwa kwa zaidi ya miezi miwili na hata wengine wameshindwa kufanya usajiri mpaka hivi sasa.., Baada ya kikao cha kuweka chinikizo wanafunzi tumeazimia kwa pamoja, Mosi tupewe ripoti ambayo itaeleza chanzo cha tatizo hilo, Pili wale wote waliohusika na wakasababisha hili suala liwe hili wanachukuliwa hatua na wanawajibishwa na ifanywe transparent , Tatu na mwisho ndugu waziri tunaomba ulipatie ufumbuzi wa kudumu tatizo hili kwa chuo cha mzumbe kwani limeshakuwa sugu na kujiludia kila mwaka