Dr. Hosea aitikisa Ikulu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Hosea aitikisa Ikulu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 25, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Tanzania Daima la leo linatutaarifu ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Dr. Hosea ameitikisa Ikulu baada ya kubainika aliongea na Shushushu wa Marekani juu ya JK kuwa ni kikwazo cha vita dhidi ya rushwa kubwakubwa.............na ya kuwa JK amekuwa akizuia mafisadi kushitakiwa kwenye mahakama zetu..........kwa visingizio vya ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwafikisha mahakamani kazi ambayo ni ya DCI na DPP.......

  Gazeti hili limebaini ya kuwa JK amesononeshwa na madai hayo ya Dr. Hosea pamoja ya kuwa tayari amekwisha kuyapinga hadharani kuwa alinukuliwa vibaya...........

  Nionavyo mimi Dr. Hosea ataondolewa hivi karibuni kwa makosa ya kutathmini utendaji wa bosi wake na kwa kufanya hivyo alikosa imani na ni utovu wa nidhamu..................Hii tukiachilia mbali ukweli kuwa JK ni mtu wa visasi sana.....................
  Dk. Hosea aitikisa Ikulu  • Serikali yapatwa na kigugumizi kumchukulia hatua

  na Edward Kinabo


  [​IMG] TAARIFA kwamba Rais Jakaya Kikwete hataki vigogo wa serikali wanaotuhumiwa kwa rushwa wafikishwe mahakamani zimeelezwa kumpa mshtuko mkubwa na kuiweka Ikulu katika wakati mgumu wa kutojua nini cha kufanya kwa sasa.
  Mmoja wa watu walio karibu naye kikazi ameliambia Tanzania Daima kwamba tuhuma hizo ni nzito dhidi ya Rais Kikwete.
  Kwamba zilionekana kumshtuka, baada ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, kuripotiwa kutoa taarifa hizo kwa mwanadiplomasia mmoja wa Marekani aitwaye, Purnell Delly, walipokutana Julai 14 jijini Dar es Salaam mwaka 2007.
  Mtandao wa Wikileaks wa nchini Marekani ndio ulioibua taarifa hizo kuhusu uwezo na nia ya Rais Kikwete katika kushughulikia ufisadi, ukidai kuwa ndiye anayekwamisha kushtakiwa kwa baadhi ya vigogo serikalini wanaotuhumiwa kuhusika katika rushwa kubwa nchini.
  Taarifa hizo zilizochapishwa na gazeti la The Guardian la Uingereza na kurejewa na vyombo vya habari vya hapa nchini, zilinukuu taarifa za kibalozi za Marekani zikisema Dk. Hosea alimweleza mwanadiplomasia huyo kwamba ugumu wa kupambana na ufisadi Tanzania unaanzia Ikulu.
  "Unajua hizo habari zimemtangaza yeye (Rais Kikwete) na CCM kwamba hawana nia ya kupambana na rushwa, yaani maana yake wananchi wamekuwa wakidanganywa tu.
  "Sasa hizo ni tuhuma nzito sana kwa mkuu wa nchi …kama ni kweli au uongo siwezi kuzungumzia hilo lakini ni rahisi watu kuamini kwa sababu aliyetajwa ni Dk.
  Hosea…eeh eeh maana huyu aliteuliwa na mwenyewe. "Angesema mwingine labda tusingeamini lakini huyu…kwa kweli ni tuhuma nzito na mwenyewe (Rais Kikwete) zimemnyong'onyeza sana," alisema mtoa taarifa huyo.
  Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Ikulu jijini Dar es Salaam zinasema mpaka sasa bado wanatafakari kwa kina hatua za kuchukua ili kupata namna bora ya kusafisha jina la Rais Kikwete na kurejesha imani ya wananchi kwake kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.
  "Mpaka sasa sijajua hatua yoyote itakayoamuliwa kwa Dk. Hosea lakini najua suala lake bado wenyewe wanalitafakari kwa sababu ni wazi kwamba jina la rais limechafuka sana," alisema mtoa taarifa wetu mwingine.
  Alipoulizwa kwa nini Dk. Hosea achukuliwe hatua wakati ameshakanusha kutoa kauli hizo dhidi ya rais, alisema: "Ni kwa sababu maelezo yake ya kukanusha hayana nguvu….yeye amekataa kwamba alisema rais hataki vigogo washtakiwe……badala yake akadai kwamba alichomwambia yule Mmarekani ni kwamba Rais Kikwete hawezi kuruhusu vigogo na watuhumiwa wengine wa ufisadi washtakiwe bila ushahidi kwa sababu serikali inaweza kupata hasara.
  "Sasa unaweza kuona waziwazi kuwa hayo maelezo yake ya kukanusha ni ya kutengeneza tu kwa sababu yule Mmarekani sio mbumbumbu wa sheria kiasi hicho hadi ampe maelezo hayo. Ni ukweli ulio wazi kwamba huwezi kumshtaki mtu bila ushahidi – hilo huwezi kuwa na haja ya kumueleza mtu.
  "Yaliyofichuliwa na Wikileaks ndio ukweli wenyewe wa aliyoyasema. Na hawa majasusi wa Marekani pengine nyie hamuwajui vizuri, ni watu wanaofanya kazi zao kwa umakini wa hali ya juu. …na hapa nchini wapo wengi tu."
  Mkurugenzi wa Mawasialiano Ikulu, Salva Rweyemamu alipoulizwa na chombo kimoja cha habari kuhusiana na tuhuma hizo nzito dhidi ya rais, alijibu kuwa Ikulu haina cha kueleza.
  Hiyo ilikuwa ni siku chache tu zilizopita mara baada ya kuripotiwa kwa habari hizo zinazomhusu Dk. Hosea.
  Aidha, Tanzania Daima ilipompigia simu Rweyemamu jana ili kujua kama ana lolote la kusema kuhusiana na tuhuma hizo dhidi ya rais, simu yake ilikuwa haipatikani.
  Hata alipotumiwa ujumbe uliomtaka kueleza hatua gani Ikulu itachukua baada ya Dk. Hosea kuripotiwa kumtaja rais kwamba hataki vigogo mafisadi washtakiwe, ujumbe huo haukujibiwa hadi tunakwenda mitamboni.
  Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema taarifa zilizoibuliwa na Wikileaks kuhusu kauli zilizotolewa na Dk.
  Hosea kwa mwanadiplomasia huyo wa Marekani, ni ushahidi tosha kwamba Rais Kikwete na CCM hawana nia yoyote ya dhati ya kukomesha rushwa na ufisadi nchini.
  Akitoa salamu zake za Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Profesa Lipumba alisema upo ushahidi wa kutosha unaoonyesha jinsi serikali pamoja na watendaji wake husika akiwemo mkurugenzi huyo wa TAKUKURU, wanavyowatetea mafisadi na kuwasafisha.
  "Taarifa ya balozi huyu wa Marekani ni kwamba alielezwa na Dk. Hosea kuwa Rais Kikwete hana nia thabiti ya kuwafikisha mahakamani vigogo wa ufisadi walio karibu yake. Ushahidi mwingine ni ule aliowahi kuutoa Rais Kikwete mwenyewe ambapo alikemea watu wanaotaka Mkapa ashtakiwe kwa kuhusishwa na ufisadi wamuache rais huyo mstaafu apumzike Akiendeleza kile alichokiita ushahidi wa Rais Kikwete na CCM kuwalinda mafisadi na wala rushwa wakubwa, Profesa Lipumba alisema: "Pamoja na shirika la upelelezi wa makosa ya jinai la SFO la Uingereza kutoa ushahidi wa rushwa aliyopewa Saileth Vithlan ya dola milioni 12.4 na ushahidi wa kibenki kwamba alitumia dola milioni moja katika akaunti zinazomilikiwa na mwanasheria mkuu wa serikali katika kipindi cha awamu ya tatu, mpaka leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nilishasema humu, Dr Hosea na Sitta wanahitaji sala zetu kwani serikali hii si ya kuambiwa ukweli wasikushike uchawi. JK mwenyewe mara kibao kanukuliwa na vyombo vya habari akisema vita dhidi ya mafisadi ni hatari mno na kwamba inahitaji tahadhari mkubwa mno.

  Sasa hebu jiweke katika vyatu vya huyu mtumishi wa chini yake (Dr Hosea) ambaye angependa kuona anafanikiwa na jukumu ambalo Wa-Tanzania tumempa kupiga vita rushwa.

  Sasa hata wewe unapokuta ya kwamba wanaotajwatajwa katika mambo ya rushwa ni maswahiba wakubwa wa bosi wako kiasi kwamba wao wakifika ikulu hupita ndani moja kwa moja.

  Kwa hali hiyo hata wewe utapata wapi jeuri ya kuwashtaki watu ambao hata bosi wako mwenyewe keshasema mwenyewe kwenye vyombo vya habari kwamba ni hatari mno na kwamba wala hawawezekani??? Isitoshe, Rais wetu huyo huyo amesikika akiwasifika watu tunaowatuhumu kwa UFISADI kwamba ni majemadari kweli kweli na watu mashuhuri sana katika maendeleo ya jamii yetu.

  Kama kweli JK naye alikua anasumbuliwa na UFISADI wa baadhi ya watuhumiwa wetu, sehemu nzuri zaidi pa kuwatupilia nje tena mbali kabisa ni kuwazuia watu kama hawa wasipitishwe na chama chao kugombea nafasi ya uongozi yoyote lakini yeye alienda mbali zaidi na kufikia hata hatua ya kuwapigia chapuo ili wakachaguliwe kuongoza.

  Sasa kwa lugha ya mwili wa Mhe rais wetu katika hatua hizi zote inatoa ujumbe wowote unaopingana na hayo madai Wikileaks?? Tunawaangalieni kwa mbali huku uraiani. Mauaji na visasi visianzie mambo ambayo wala si siri kwa umma wa Tanzania.

  Dr Hosea asiwe kisingizio wala mbuzi wa shughuli katika masuala ya UFISADI unaotisha nchini mwetu.
   
 3. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hoseah himself is a Fisadi and friend of Fisadis
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Hosea yeye ni ndumila kuwili........na JK nimfahamuvyo mimi ni lazima atamshughulikia tu..........................hivi karibuni...................na hoja zitajengwa...........kama siyo umri umefika......................basi mkataba umekwisha............au tunataka Takukuru iwe huru...............................................kwa kuwa na viongozi waliopitishwa na Bunge.............................something will be cooked to fry him alive................and the time has just begun ticking......................
   
 5. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Jk ndio fisadi mkuu, hoseah mtumwa wake!
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  natamani zipatikane weekleaks kama 10 hivi itakuwa poa sana
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180  Hosea is nothing, and I don't think if we are doing right to discuss this stupid person.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bora amuondoe na akambakishie uhai wake.

  Na mara baada ya hapo, kiongozi wa TAKUKURU ajaye nafasi yake itangazwe magazetini na PriceWatersCoopers wakawafanyie interview ya kufa mtu kisha majina sita yatakayo bakishwa kwenye mchakato yapelekwe Bungeni Dodoma ili nao wakawachuje na kubakisha majina matatu ambayo ndio yatakayopelekwa kwa rais kuteua mmoja tu kati yao kushika wadhifa huo nyeti. Kusiwepo na mambo ya u-KADA wala urafiki katika hili.

  Mara baada ya uteuzi, rais atangaze kumachia mikono huru mtu huyo afanye kazi jinsi taaluma yake inavyomelekeza.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wala usipate taabu katika hili, hizi unazoona kwa sasa ni vya mtoto tu ... ngoma bado iko njiani na watu tutapotea na milango na kuishia kutokea dirishani.

  Vuta pumsi kaka.
   
 10. K

  KAMARADE Member

  #10
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ni visasi gani ambavyo JK amewafanyia watu? Mnaweza kutupa mifano hai ili tuweze kuelewa.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndg Karamande wewe, wale viongozi wenye hekima ya Pope John Paul wa pili kupigwa risasi na mtu kisha akaja akamtoa huyo mtu jela na kukaandaliwa chakula wakala wote meza moja, kwa huku bara letu iliojaa giza hili, hata MAONI TU kutofautiana basi tayari wewe haki yako ni kifo cha kiana.

  Listi hiyo unayoitaka wewe ni sharti niwe na uhakika kwamba umeshapata supu ya nguvu usije ukadondoka chini bure!!1
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hosea hivi sasa anajua kitumbua kimeingia mchanga na mkwere anamlia timing tu; hivyo nae anajitayalisha kukimbia ili akauungane na familia yake huko marekani!! Wajinga ndio waliwao!
   
 13. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  ukitaka kufikisha message yako ccm,ongea halafu sema ulinukuliwa vibaya,...na kwa vile ccm wanajua exactly hosea alisema...he is a goner just like that...i never liked hosea since the richmond/dowans saga,..so well...hell
   
 14. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280

  labda sijui vizuri lakini nafikiri PWC ni accounting firm!wamfanyie interview mkurugenzi wa TAKUKURU kwani anatafutwa mhasibu mkuu wa serikali au CAG!!mi nadhani hawtakiwi watu wenye CPA'S na ACCA takukuru
   
 15. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  i support u 1000% absolutely he is a fisadi.
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi kwa kauli ya Dr.hosea kuwa Jk ni kikwazo ktk kesi za rushwa, ndio kusema yeye Hosea ni mtu safi ila anaharibiwa na Jk au?
  Mi sijamwelewa Hosea kabisa.
   
 17. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  The BOSS of PCCB is not the RPC. He already know too much for comfort. My bet is that removing him will be a suicide for the current government and will be retained lest he spill the beans. He will be spared until such a time when it will be safe to depose him OR Kill him.
   
 18. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, mimi nahisi wewe unajitahidi kumjenga na kumtetea huyu Hosea fisadi mkubwa kwa kutaka kum empty Kikwete ili amuache mahali alipo!!! Hosea si ndiye huyu huyu aliye msafisha fisadi Chenge juzi juzi? Hivi aliambiwa au kulazimishwa na Kikwete ili kumsafisha chenge? I will be very glad akifungashiwa virago vyake, tena siyo kesho afungashiwe leo, kama hakutimuliwa jana!! Hosea ameigeuza TAKUKURU kuwa kitu tofauti na madhumuni ya kuanzishwa kwake.

  Hosea hana cha kujitetea kwetu hata kwa hao Wamarekani maana hakuna la maana alilokwisha fanya la kufanya tumuonee huruma! kama kweli alizuiwa kumkamata Mkapa na Mwinyi, je alizuiwa pia kumkamata Tannil Somaiya? Chenge? Manji? Mkono?Subash? Lowasa na Rostam?

  Hawa wote ni wasanii wanafanya mchezo wa kuigiza. Kikwete akiwa kwenye kona zake anasema kuwa anaangushwa na maafisa wa takukuru na wale wa ofisi ya upelelezi na mwanasheria mkuu lakini hachukui hatua dhidi ya hao wanaomwangusha akianzia kwa wakuu wa taasisi hizo. Then hosea naye anakuja anasema nimezuiliwa kufanya kazi zangu, Mkurugenzi wa upelelezi na Mwanasheria Mkuu nao wanasema hatujawezeshwa kufanya upelelezi au hakuna ushahidi wa kutosha wa kupeleka mahakamani!! ....... na Sinema inaendelelea hivyo hivyo na nchi inaendelea kuliwa tu
   
 19. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nenda segerea utapata majibu!!! usipopata kwa wengine mutafute babu Seya atakwakwambia!
   
 20. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usio pingika kwamba Kikwete ndiye kikwazo cha mafisadi kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, kwa kutoa sababu za kitoto kwamba huwezi kumpeleka mtu mahakamani mpaka ithibitishwe kwamba ana hatia.Hata kama mtandao wa WikiLeaks usinge m-quote Hosea haya tunayajua.Compelling evidence is everywhere.Kinachonikera hapa ni kwamba Hosea anamtupia lawama mwenzie ili aonekana kwamba yeye hana matatizo,mwenye matatizo ni Kikwete.Hizi ni tabia za kitoto.Kwanza yeye mwenyewe ana usafi gani mpaka awe tayari kushughulia mafisadi?Ni mapapa yale yale tu.Ana tuhuma chungu nzima.Finally hapa hakuna wa kumchukulia mwenzie hatua,wote wana hatia,wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
   
Loading...