Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 4,820
- 8,886
Mdondoaji,
You're always against unfairness lakini naona kama hauko fair kwa Dr Shayo.Naamini unafahamu kuwa ASILI ya PhD ni kumpatia mwanataaluma uwezo wa kufundisha.Actually,hilo neno lenyewe PhD lina tafsiri ya moja kwa moja ya mwalimu wa filosofia (philosophiae doctor).Wakati inatarajiwa kuwa mhitimu wa PhD atabobea kwenye fani aliyoamua ku-specialise,bado anaweza kuwa na uwanja mpana kutegemea na fani husika hususan kwenye sayansi za jamii.Ni muhimu pia kufahamu kwamba fani aliyopitia mwanataaluma kabla ya kuhitimu PhD (kwa maana ya shahada ya kwanza na ya uzamili) inaweza kumsaidia mwanataaluma huyo kutanua upeo wa fani anayozamia.
Sasa kama Dr Shayo ana BA ya Economics,na MA ya Development Studies (ambapo kuna masuala ya Economics pia) na kisha akachukua PhD ambapo research interest yake ilikuwa kwenye Economics pia (pamoja na sustainability and environment in the construction sector) kuna tatizo gani kwa mwanataaluma wa aina hiyo kuchukua nafasi ya kufundisha Economics open university ambapo wengi wa wanafunzi wake watakuwa wanasomea shahada ya kwanza na ya pili?On top of that,Dr Shayo ana experience kama assistant programme development officer for local government reform program under the PMO.Sasa pengine kabla ya kuhoji kwanini ameteuliwa kuwa mhadhiri mwandamizi wa Uchumi ingekuwa busara kuuliza ni eneo gani la Economics atakuwa anafundisha.What if atakuwa mhadhiri wa Duoble Economics kwa Undegraduates au Managerial Economics (OBS602 Kwa Open University of Tanzania) kwa Postgraduates?Kwa kufahamu kozi zinazotolewa na taasisi hiyo angalia link hii http://www.out.ac.tz/directorate/postgraduate/masters/masters.htm na http://www.out.ac.tz/prospective/admission.html#C2
Lakini pengine kukupa mwanga katika nachoongelea hapa jaribu kutembelea tovuti hii www.jobs.ac.uk kisha angalia person specifications zinazobainishwa na baadhi ya vyuo vinavyotangaza nafasi za kazi za wahadhiri.
Ni muhimu pia kukumbuka kuwa wakati sifa muhimu ya kuwa mhadhiri ni USOMI katika fani husika,kuwa mhadhiri mwandamizi,profesa msaidizi au profesa kamili ni mambo yanayotegemea zaidi UZOEFU unaoambatana na usomi wa mwanataaluma katika fani husika.
Ni rahisi kumkosoa Dr Shayo aliyemudu kufikia hatua ya juu kitaaluma (naam,PhD sio rahisi kama kupiga soga) na kuandika machapisho kadhaa ya kitaaluma ilhali wengi wetu tunafahamu mgogoro unaoikabili Tanzania kama taifa linapokuja suala la uandishi wa machapisho ya kitaaluma (njia nyepesi ya kuthibitisha hilo,tafuta kijitopiki chochote kile kisha anza literature review inayotegemea vyanzo kutoka Tanzania).
Let's be fair!
Mlalahoi ingawa umetuita wenzio wavivu wa kutumia teknolojia, mimi sijaona ulipotoa majibu fasaha. Hata wewe umepiga around the bush. Leta hapa publication list ya Dr. Shayo..tuone amepublish wapi na nini! au tupe hiyo link. Hata kama "sijasoma sana" I know msomi when I see one.
What I know, ni kwamba mtu kuwa mhadhiri mwandamizi, its all about publications. Simple! (unless Tanzania we use different standards). Unaweza kuwa na degree moja, lakini ukawa ume-publish machapisho mengi. Which can elevate you to professorship. Kwa upande wa Dr. Shayo no body is questioning his education-atleast not me. I know he worked so hard to be where he is (irrespective of where he studied). Ninachopinga ni hii ya kutumia umaskini wetu watanzania kujustify any mediocrity coming from the so called wasomi. Eti kwa vile hatuna walimu/wahadhiri wa kutosha basi inabidi tukubali hata tukiletewa wahadhiri feki! Please, we are past that mkuu.
I remember one day, jamaa pale MZUMBE alitaka kuwa promoted kwenye level ya Associate Professor..wakati this person alikuwa...na four articles published in four jounals za Tanzania! Alikuwa hajawahi publish beyond the boaders of our country. Well, I cant argue more..but nilipata maswali mengi kuliko majibu na hatima ya wasomi wetu!
Masanja