Dr. Harrison Mwakyembe unajua kinachofanyika Kivukoni??????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Harrison Mwakyembe unajua kinachofanyika Kivukoni???????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rich Dad, Jan 10, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa Dr Harrison Mwakyembe na wahamiaji wapya wa Kigamboni,

  Yafuatayo yalinikuta wakati nahamia kigamboni:-

  Nilipofika na gari aina ya Canter tani tatu sehemu ya Kulipia, ambayo mara nyingi wanakaa wadada wawili, na mmoja anauza ticket kwa upande ule magari yanapoingilia. Nilikutwa na mkasa wa ajabu pale nilipokwenda kulipia gari ili liweze kuingia. Yule dada alianza mbwembwe zake kwa kumuomba dereva kadi ya gari. Jamaa akamwambia sijatembea nayo ila uzito wa gari ni tani tatu, akamwambia hutavuka kama huna kadi ya gari. Mimi nikamwambia kwani tatizo nini? akanambia anataka kadi ya gari ili aweze kuangalia uzito wa gari. Nikamwambia kwani kuna mizani ya kupimia uzito? na hata ukipata kadi ya gari unawezeje kujua uzito wa gari pamoja na mizigo pasipo na mizani?
  Ndipo nilipoambia nitoe elfu tano, ambayo niliotoa...sikujua kinachoendelea na niliendelea kusubiri risiti. Ndipo yule dada akaniambia ondoka unasubiri nini? Nikamwambia nipe risiti. Akanikashifu na kuniambia kama hutaki kuvuka endelea kusubiri risiti. Nikamwambia naondoka lakini jua hiyo elfu tano itakutokea puani kama ndo tabia yenu.

  Tulipoondoka hatukuvuka hata kile kizuizi cha mwisho kuingia kwenye pantoni akaja askari mwingine akatuamuru tupaki gari pembeni. Nikamwambia kwani shida iko wapi wakati tumeshalipia?? Baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu ikabidi nimuombe yule askari msamaha bila kupenda ili aturuhusu kuvuka. Ndipo tulipobadilishiwa kibao kwanini mnavuka bila kuwa na risiti??. Niliwaeleza tumelipia Tsh.5000 na tulipoomba risiti tumejibiwa kashfa. Nikaambia nirudi nikachukue risiti, nikaelekea upande ule wa dirishani na sikufika hata dirishani ..nikakutana na askari mwingine amevalia kiraia akaniambia njoo uchukue risiti. Nilipomfikia akaichua ile risiti akaichana vipande viwili akanipa nusu na nusu akabakiwa nacho, akaniamuru niende nimpelekee askari yule aliezuia gari na nimueleze kuw nimeshalipia. Nikatii amri ya bwana mkubwa na niliponesha tukaruhusiwa kuondoka.

  MY TAKE:
  - Suala la kadi ya gari si kigezo cha kudhibiti magari yenye uzito uliozidi sehemu ambayo hakuna mizani ya kupimia uzito, unless kama kuna sheria kama hiyo.
  - Kushuka kwa mapato ya pale kivukoni huenda kunatokana na vitendo kama hivi vya rushwa vinavyofanywa na askari polisi kwa kushirikiana na ma-cashiers.
  - Kuna hatari ya kuja kuzamisha kivuko( Siombei) kama vitendo vya rushwa havitadhibitiwa mapema.

  Ushauri wangu:
  - Ili kudhibiti mapato pamoja na kumbukumbu ni wakati muafaka sasa kwa serikali kuanzisha mfumo wa kielekroniki ( Card Pre-paid system). Serikali itakusanya mapato yake kwa muda muafaka na itaweza kutunza kumbukumbu zake vizuri zaidi, ikilinganishwa na wakati huu ambao mtu anaweza aka temper na receipt books.
   
 2. k

  kisukari JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  hiyo ndio bongo,kila sehemu ndio hayo hayo.mimi kwenye atm zilitoka noti feki,siisahau siku hiyo
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hii unganisha na ile ya mwakyembe kufichua ufisadi wa kivukoni ili tutunze hii thread, kuna nyingine kama mbili ntaomba mkikubali tuunganishe sie wadau ili kieleweke
   
 4. K

  Kivia JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huu mfumo wa electronic p. Card ulifungwa na ulifanya kazi wiki moja wakauchakachua. Hata mashine bado zipo.
   
 5. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Umuhimu wa mizani pale hauhitaji kungoja miezi mingine tisa, pale mambo yanaharibika kwa kasi sana. Kingine ambacho huwa nakiona ni cha upuuzi kidogo pale, kuna watu wengi sana ambao sijui wanaumuhimu gani kwa kituo kile, Ukiacha wapiganaji wetu, wanaopita bure tena na magari yao. Ni ukiukaji wa taratibu uliokithiri.
   
 6. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama kuna mtu anaweza kusaidia kuziunganisha asaidie.
   
 7. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa kuliona hilo mkuu, mizani inatakiwa iwekwe haraka tena mno!!! unless pantoni linauwezo wa kupima uzito lililobeba automatically. Bila hivyo tusubiri maafa ambayo yangeweza kudhibitiwa mapema.
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hii kali kabisa. Bongo tambarare Duh.
   
Loading...