Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nape ameondoka na Mwakyembe ameingia. Kuna watu walikuwa na wasiwasi kuwa huenda Mwakyembe asifanikiwe kuvaa kiatu kilichoachwa na Nape. Hata hivyo kwa muda mfupi aliokalia kiti hicho, amekuwa na ufanisi mkubwa na weledi wa hali ya juu. Amerudisha nyoyo za waliokata tamaa na amepunguza joto lililotanda na mashambulizi dhidi ya Serikali.
Mwakyembe ni shujaa. Alipoteuliwa kuwa Waziri wa Habari, ameanza kazi mara moja na kwa jinsi alivyoshughulikia suala la Nay wa Mitego kwa hakika limethibitisha kuwa jamaa ni mtu muhimu sana kwenye wizara hiyo. Tatizo la Nape ni umri wake. Bado ana utoto mwingi na hivyo kujikuta akiendekeza tamaa zake badala ya kufanya kazi. Aliwagawa wasanii badala ya kuwaunganisha. Amevigawa vyombo vya habari kwa kuvipendelea baadhi na kuviponda vingine.
Kwa ujumla Nape hakuwa kiongozi mtendaji. Aliendekeza majungu na fitina Wizarani. Afadhali ameondoka.
Karibu Dr Mwakyembe. Chapa kazi. Usimpendelee mtu na wala usimuonee mtu. Haijapita hata mwezi tayari Nape amebaki historia