Dr Harrison Mwakyembe atakuwa Waziri Bora wa Habari kuliko Nape Nnauye

Nape aliplay key role katika kuzuia bunge live, hii ni dhambi kubwa kwa umma na itamtafuna kisiasa.

Pili alipeleka muswada wa habari bungeni, ambao kwa upande mmoja una mapungufu makubwa ya kuzuia uhuru wa habari.

Lakini Tangu Nape awe Waziri wa michezo Taifa Stars ya Wakubwa imekuwa kichwa cha Mwendawazimu, Mwakyembe kaingia tu, tumeshinda gemu mbilu in a row!

Nape hajamsaidia Mwenyekiti wa Yanga katika madhila yake, I hope Mwakyembe atasaidia Manji awe huru!

Hata hivyo nampongeza Nape jinsi alivyosimamia suala la kuvamiwa Kituo kimoja cha Habari na Bashite!

Yanga hoyeeee !
Umefanya tathmini fupi lakini imeeleweka. Big Up Bro
 
Hivi yule Maulid Kitenge ana maslahi gani na Nape? Maana siku ile na wanahabari alikuwa kama mkoba wa Nape
 
Nape alikuwa ni janga la taifa kwa hivyo yeyote ambaye angekalia hicho kiti ni lazima angen'gaa tu.

Nape ni muasisi wa siasa za chuki na kikabila nchini. Kumbuka ndiye kiongozi wa juu wa kwanza kabisa kutamka kuwa hawezi kuhamia Chadema kwa sababu yeye siyo mchaga.

Nape ndiye waziri aliyetuletea sheria ya ovyo kabisa ya habari ambayo ubovu wake ni wa kiwango cha lami

Nape tena alisifia siasa za goli la mkono. Hata kama ni kweli liatumika, kulikuwa kuna haja gani kulitangaza kwa mbwembwe kiasi kile

Madudu ya Nape ni mengi mno na kilichompata ni stahili yake. Kwanza hata hiyo saga ya Clouds aliichukulia vile kwa sababu tu ya chuki binafsi aliyekuwa nayo kwa RC.
Tatizo la Nape ni kule kikosa utulivu tu, otherwise kwenye siasa ni mzuri tu. Uwaziri ni level nyingine kabisa mtu anapaswa kutulia katika kufanya maamuzi
 
Umekuja lini Tz?

Yaelekea hukuwepo Rais JPM alipotangaza kuachiwa kwa Ney.

Leo Nape amekuwa mtoto, alipokuwa akiwatangazia ,kuwatafutia na kuwapatia
"goli la mkono " alikuwa mzee?

Wakati akizuia matangazo ya Bunge mubashara alikuwaje?

JE HUYO MKOMAVU WAZIRI WAKO BORA ANAWEZA RUDISHA MATANGAZZ MUBASHARA YA BUNGE ????
Unaweza kuwa na busara kwa mambo mengi tu, lakini moja tu ukafanya utoto, ndicho kilichotokea kwa Nape
 
Tatizo la Nape ni kule kikosa utulivu tu, otherwise kwenye siasa ni mzuri tu. Uwaziri ni level nyingine kabisa mtu anapaswa kutulia katika kufanya maamuzi
Kama UTULIVU ni kigezo cha uwaziri basi huyo mzee hafai hata Unaibu WAZIRI.
Rejea kituko chake cha hivi karibuni kuhusu NDOA
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nape ameondoka na Mwakyembe ameingia. Kuna watu walikuwa na wasiwasi kuwa huenda Mwakyembe asifanikiwe kuvaa kiatu kilichoachwa na Nape. Hata hivyo kwa muda mfupi aliokalia kiti hicho, amekuwa na ufanisi mkubwa na weledi wa hali ya juu. Amerudisha nyoyo za waliokata tamaa na amepunguza joto lililotanda na mashambulizi dhidi ya Serikali.

Mwakyembe ni shujaa. Alipoteuliwa kuwa Waziri wa Habari, ameanza kazi mara moja na kwa jinsi alivyoshughulikia suala la Nay wa Mitego kwa hakika limethibitisha kuwa jamaa ni mtu muhimu sana kwenye wizara hiyo. Tatizo la Nape ni umri wake. Bado ana utoto mwingi na hivyo kujikuta akiendekeza tamaa zake badala ya kufanya kazi. Aliwagawa wasanii badala ya kuwaunganisha. Amevigawa vyombo vya habari kwa kuvipendelea baadhi na kuviponda vingine.

Kwa ujumla Nape hakuwa kiongozi mtendaji. Aliendekeza majungu na fitina Wizarani. Afadhali ameondoka.

Karibu Dr Mwakyembe. Chapa kazi. Usimpendelee mtu na wala usimuonee mtu. Haijapita hata mwezi tayari Nape amebaki historia
Kwa kusifia kwenu kila nyie Mbweha na Nyumbu wa Lumumba kitu hiyo Nafasi hata angepewa Msukuma ama Kibajaj bado ungesema hivyo hivyo
 
Kwa majungu, chuki, fitna na kujipendekeza kaka unatisha, we ni chiboko, mola niepushe na huu ugonjwa wa kulamba watu miguu,
Hana tofauti sana na DAB a boy from kolomije niliwahi kuona picha yake akimfunga viatu lizboy from msoga, NI tabia ya mtu tuu
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nape ameondoka na Mwakyembe ameingia. Kuna watu walikuwa na wasiwasi kuwa huenda Mwakyembe asifanikiwe kuvaa kiatu kilichoachwa na Nape. Hata hivyo kwa muda mfupi aliokalia kiti hicho, amekuwa na ufanisi mkubwa na weledi wa hali ya juu. Amerudisha nyoyo za waliokata tamaa na amepunguza joto lililotanda na mashambulizi dhidi ya Serikali.

Mwakyembe ni shujaa. Alipoteuliwa kuwa Waziri wa Habari, ameanza kazi mara moja na kwa jinsi alivyoshughulikia suala la Nay wa Mitego kwa hakika limethibitisha kuwa jamaa ni mtu muhimu sana kwenye wizara hiyo. Tatizo la Nape ni umri wake. Bado ana utoto mwingi na hivyo kujikuta akiendekeza tamaa zake badala ya kufanya kazi. Aliwagawa wasanii badala ya kuwaunganisha. Amevigawa vyombo vya habari kwa kuvipendelea baadhi na kuviponda vingine.

Kwa ujumla Nape hakuwa kiongozi mtendaji. Aliendekeza majungu na fitina Wizarani. Afadhali ameondoka.

Karibu Dr Mwakyembe. Chapa kazi. Usimpendelee mtu na wala usimuonee mtu. Haijapita hata mwezi tayari Nape amebaki historia
Tatizo la Mheshimiwa Mwakyembe ni kwamba huwa msimamo wake juu ya masuala muhimu huwa haueleweki!. Vitu vingi alivyokuwa anaviamini enzi za ujana wake haviamini tena. Intellectually amekuwa "a born again apologist". Mifano miwili inadhihirisha haya. Haamini katika Serikali Tatu kama suluhisho la matatizo ya Muungano (Thesis ya PhD yake inasema hivyo). Pili juzi tu ameipinga Ripoti ya Uvamizi wa kituo cha TV cha Clouds kwa kuwa Mheshimiwa Makonda hakupewa nafasi kujitetea wakati Tume yake ya kuchunguza suala la Richmond ilimhukumu Mheshimiwa Edward Lowasa bila hata kumualika. Katika ulimwengu wa siasa na Uongozi "the Devil you know about is far better than the Angel you do not know".
 
Kuendelea kupata vichekesho kama hivi kutoka kwa lizaboni tafadhali bonyeza alama ya # utatozwa tsh 30/= tu kwa siku
 
Jamaa phd yake haina specialisation kila wizara anapangiwa mara sheria,africa mashariki,uchukuzi na sasa habari yaani jamaa amekuwa shamba a bibi
Muda si mrefu atapelekwa kilimo na mifugo
 
Huyu mwakembe ni sifuri kaisa juzi anasema kamati haikuwa na maoni ya upande wa makonda anasahau kwenye kamati ya richmondi yy akiwa mwenyekiti walimuhukumu lowassa pasipo kupata maoni yake
 
Back
Top Bottom