Dr. Eve Hawa Sinare atangaza Kuhama CCM

Dr. Eve Hawa Sinare atangaza Kuhama CCM

Hana madhara....did you know her before hilo tangazo???

Yes. She finished her pHd at Konstanz University Germany. And she is an inteligent woman! I could imagine of her being an asset for any Tanzaian jumuia fighting for Mabadiliko.
 
Yes. She finished her pHd at Konstanz University Germany. And she is an inteligent woman! I could imagine of her being an asset for any Tanzaian jumuia fighting for Mabadiliko.

I see, umefanya ur homework vizuri mkuu....
Pengine niulize hivi, katika muktadha wa siasa za nchi na ccm, alikuwa ni nani huyu Dr???
 
Ni moja ya ma technocrat wazuri kabisa.

Kama kumbukumbu zangu ni sahihi jina hili la ukoo wao walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa chama changu pendwa kilichopendwa na mafisadi nyakati hizi; wakaingia kwenye mtandao na baada ya kupiga deal za kutosha sijui wanarudi tena nyumbani kuendeleza usanii?

Ukiwa msomi wa hivi ni bora ungebakia kuwa ngumbaru, any way let them be!
 
Misukule yote huongea hivyo ila Uongozi ndani ya chadema sahau utaishia kufanywa chambo tu kama misukule wenzako waliolemazwa baada ya kushawishiwa na KLM elite kuandamana na kubeba spika tu za matangazo!

Pumba tupu ccm wao ndo wanatoa uongoz? Rizone na mama yake wanacheo gani ndani ya ccm? Mtoto wa kombani anagombea kule kawekwa na maccm baada ya mama yake kufarik hilo hulion sitta na malecela wote wamesimamisha wake na watoto hayo huoni? Baadae waje kuwa mawazir kama walivyo watoto wa mwinyi amka wewe gamba watu wanajitambua
 
I see, umefanya ur homework vizuri mkuu....
Pengine niulize hivi, katika muktadha wa siasa za nchi na ccm, alikuwa ni nani huyu Dr???

Mkuu inawezekana labda wewe ni kada wa chama chetu au siyo? Mkuu tafadhari think more innovative!!! Mabadiliko hayaitaji mtu kutoka ktk chama chetu ambaye alikuwa na mavyeo ya kupachikwa as if hakuna wengine. Dr she might get an open space to play her role as an innovator! Siyo kushikiria mawazo ya miaka 50 iliyopita.
 
Mkuu inawezekana labda wewe ni kada wa chama chetu au siyo? Mkuu tafadhari think more innovative!!! Mabadiliko hayaitaji mtu kutoka ktk chama chetu ambaye alikuwa na mavyeo ya kupachikwa as if hakuna wengine. Dr she might get an open space to play her role as an innovator! Siyo kushikiria mawazo ya miaka 50 iliyopita.

Mkuu, kwanza niseme mm si kada wa kile chama chetu kama mama Sinare.

Pili, sina personal vendetta na Dr kukihama chama alichokitumikia ujana wake wote na kuamua kutojishughulisha na siasa uzeeni.

Mimi kama mtanzania wa kawaida kabisa ambaye navuja jasho kutumikia makaburu nna haki ya kuhoji motives behind ya hiki kinachoitwa "kuchoshwa na siasa za ccm" courtesy of Mzee Kingunge na wengine mfano Dr Sinare, Balozi Mwapachu etc......

Mkuu sisi watu wa kawaida, kazi yetu ni kutuhumu in the same way tulifanya kwa Mh EL akiwa chama chetu kabla ya kukatwa na kuhamia "mabadiliko"...unakumbuka tulimpa jina maarufu, "fisadi mkuu"...Kwa mantiki hiyo ndiyo maana nikasema, mama hana madhara, yeye amekubali tu kutumika kwa manufaa ya mafisadi wa jana ambao leo ni makamanda kama ambavyo wengine wanasema Dr Slaaa alitumika kwa manufaa ya magamba...similarly ni kwa balozi Mwapachu na wengineo
 
MMGM2455.jpg


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Eve Hawa Sinare

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Eve Hawa Sinare, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho.
Dk. Sinare amesema amefikia uamuzi huo kutokana na CCM kushindwa kutatua matatizo ya vijana na umaskini kwa kutoa huduma bora ya afya, elimu, maji na umeme hata wakishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Dk. Sinare alitangaza hayo juzi jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari.

"Kuanzia leo (juzi, nimejitoa CCM," akisisitiza huku akisema licha ya kujitoa katika chama hicho tawala, bado hajaamua kujiunga na chama kingine chochote cha siasa.

Hata hivyo, Dk. Sinare alisema anaunga mkono mabadiliko ya kweli ndani ya nchi.

Uamuzi wa Dk. Sinare kujitoa CCM unakuja siku chache baada ya aliyekuwa kada wa chama hicho, Balozi Juma Mwapachu, kutangaza kujiengua katika chama hicho na akitanguliwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyetangaza kujitoa CCM, Oktoba 4, mwaka huu.

Dk. Sinare ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kahawa, Mwenyekiti wa kuchunguza matatizo ya vyuo vikuu na Mjumbe wa Bodi ya Mashirika ya Umma ambaye hivi sasa ni Wakili wa kujitegemea, alisema kwa miaka 53 madarakani, elimu nchini ni duni huku viongozi wakichukulia uongozi ni ajira ya kujitajirisha kuliko kuangalia matatizo ya Watanzania.

Alisema kuwa hivi sasa vijana wengi hawana ajira zenye tija wakati viongozi wanajilimbikizia mali na kujilipa mamilioni ya fedha kwenda kuhonga na kununua kura kila inapofika kipindi cha uchaguzi.

Dk. Sinare alisema Serikali ya CCM imewakosea wananchi, kwani kwa miaka yote ilipokuwa madarakani, huduma za afya zimekuwa duni huku viongozi bila woga wakisafiri kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu ya gharama kubwa na hospitali zikikosa dawa.

Alisema huo ni mfumo mbaya uliowekwa na CCM kuwanufaisha viongozi huku wananchi wakiteseka kwa kukosa huduma bora na uongozi kutoka kwao.

Aliongeza kuwa vyombo vya usalama, Polisi na muundo mzima wa serikali pamoja na mashirika ya umma, yamekuwa yakitumika kukampenia chama tawala.

Aidha, alisema chini ya uongozi wa CCM, kila Mbunge hulipwa mafao makubwa na yasiyo na ulazima pindi Bunge linapovunjwa.

Alisisitiza kuwa mambo yote mabaya yaliyofanywa na CCM na kuifanya nchi kuwa katika hali mbaya, yanahitajika mabadiliko ili kuokoa ufujaji wa fedha za umma ziende kuwahudumia Watanzania.

Chanzo:
NIPASHE


 
msomi naye kaingia mkenge kambi lwasa hyo anafikiri akishinda atapew xheo pole mama ukawa hawaingii ikulu kamweeeeee
 
Back
Top Bottom