Dr.Edward Hoseah ataka kuletewa ushahidi mezani,kuhusu rushwa

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Hii ni kauli aliyoitoa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari leo. Dr.Edward Hoseah amesema ushiriki wa jamii ya Watanzania katika vita dhidi ya rushwa umekuwa mdogo..."watu wanalalamika tu ooh yule mtoa rushwa,yule fisadi,maneno matupu hayatusaidii "......Hivyo ndivyo alivyosema Mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania......source:star tv...........MY TAKE................Kama taasisi kama TAKUKURU yenye wataalamu wanaolipwa kwa ajili ya kuzuia na kupambana na rushwa hawawezi kuifanya kazi hiyo basi wanalipwa kwa kazi gani? Watu wasioweza kutafuta ushahidi EPA,RICHMOND,MEREMETA,KAGODA na rushwa katika uwekezaji wa ardhi badala yake wanataka wananchi wanaodhurika kwa rushwa na kulalamika wawapelekee ushahidi? Kweli TAKUKURU ni toothless dog kwani ni vizuri wananchi kuripoti kuhusu rushwa lakini siyo kutoa ushahidi kwani hawana utaalamu wa kutosha.Kwa mwendo huu,kuna matumaini ya kutokomeza rushwa Tanzania?
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
46,552
2,000
Sasa yeye kazi yake ni ipi kama anataka tumpelekee ushahidi??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,096
2,000
Wasting of our time kuijadili Takukuru, Wiki leaks walituambia yote kuhusu hii taasisi sasa mnamhoji nini tena cha ziada?
 
DSM

Member
Oct 25, 2012
35
0
Waziri wake Mkuchika nae anakurupuka eti wenye majina wa watz wenye akaunti nje wampelekee. hivi mzee wa vijisenti si alikiri kabisa kwamba yeye anavijisenti mbona hawajamfanya chochote. waache usanii wao
 
Africa_Spring

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
428
0
Yupo sahihi coz watu wanasematu lakini ushahidi hawatoi sasa mnataka asemeje. Tumesikia ya uswiss kila siku kucha kutwa
kutaja hakuna, tajeni majina, na pia mnapo sema chaguzi zimegubikwa na rushwa watajeni basi, Au ndo kama ya Sumaye,,,,
 
Mr. Mwalu

JF-Expert Member
Feb 4, 2010
1,058
1,500
yupo sahihi coz watu wanasematu lakini ushahidi hawatoi sasa mnataka asemeje. Tumesikia ya uswiss kila siku kucha kutwa
kutaja hakuna, tajeni majina, na pia mnapo sema chaguzi zimegubikwa na rushwa watajeni basi, au ndo kama ya sumaye,,,,
mangula mwenyewa kaistukia kwamba haina dili anadai ukikamatwa wala rushwa hatosubiri taku ..ru, p'se changanya na zako!
 
Mpwechekule

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
221
0
Yupo sahihi kwani serikali yetu ina jukumu la kulinda mafisadi, hivyo anataka mtu ajitokeze kusema ili ashughulikiwe iwe fundisho kwa wengine, ile taasisi ya majambazi inayokula jasho letu kulinda majambazi sugu na masilahi ya viongozi mafisadi kwa kifupi ni kikundi cha kihalifu kama mafia n,k.
 
Monyiaichi

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
1,826
1,250
hata hivyo haiwezekani kuwa hajawahi pelekewa. atuambie alizopewa ushahidi amewahi kuzitolea uamuzi gani zaidi ya kupindishapindisha. kama hukumu ya Mungu ipo sijui wengine wataikwepaje?!
 
Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,559
2,000
Hii ni kauli aliyoitoa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari leo. Dr.Edward Hoseah amesema ushiriki wa jamii ya Watanzania katika vita dhidi ya rushwa umekuwa mdogo..."watu wanalalamika tu ooh yule mtoa rushwa,yule fisadi,maneno matupu hayatusaidii "......Hivyo ndivyo alivyosema Mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania......source:star tv...........MY TAKE................Kama taasisi kama TAKUKURU yenye wataalamu wanaolipwa kwa ajili ya kuzuia na kupambana na rushwa hawawezi kuifanya kazi hiyo basi wanalipwa kwa kazi gani? Watu wasioweza kutafuta ushahidi EPA,RICHMOND,MEREMETA,KAGODA na rushwa katika uwekezaji wa ardhi badala yake wanataka wananchi wanaodhurika kwa rushwa na kulalamika wawapelekee ushahidi? Kweli TAKUKURU ni toothless dog kwani ni vizuri wananchi kuripoti kuhusu rushwa lakini siyo kutoa ushahidi kwani hawana utaalamu wa kutosha.Kwa mwendo huu,kuna matumaini ya kutokomeza rushwa Tanzania?
kwani vile vidagaa wanavyvikamataga wanapelekewa na nani?
 
kivyako

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
14,280
2,000
takukuru wenyewe uwa wana visa vya kuzugia km kuwakamata wanaotoa rushwa za bukubuku ktk chaguzi za chama tawala, nahisi uwezo wao unaishia hapo, msitake wapasuke vifua kwa kuwabebesha mambo mazito km ya richmond etc Bravo Dr. Hosea.
 
Nyalutubwi

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
573
225
Yupo sahihi coz watu wanasematu lakini ushahidi hawatoi sasa mnataka asemeje. Tumesikia ya uswiss kila siku kucha kutwa
kutaja hakuna, tajeni majina, na pia mnapo sema chaguzi zimegubikwa na rushwa watajeni basi, Au ndo kama ya Sumaye,,,,
Wewe ni Mtanzania na unalipa kodi?.Wajibu wa raia katika Serikali yeyote duniani ni kulipa kodi Serikalini ikionekana kodi hiyo inaibiwa si kazi ya raia hao kuidhibitishia serikali wezi wanaoiba kodi hiyo.Ni jukumu la Serikali iliyoko madarakani kuonyesha na kuthibitishia wananchi walipa kodi kwamba kodi zao ziko salama.
Hata ukienda kwenye Msingi wa utawala bora si jukumu la msingi Raia kuzuia wezi wa mali za umma na jukumu hili ni la akina Edward Hosea na Waziri Mkuchika na ndilo linalowapa uhalari wa kulipwa Mishahara na marupurupu mengine kutoka hazina ya nchi..
 
Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,327
2,000
Meno ya takukuru yapo mikononi mwa wananchi,peleni ushaidi jamani ili kuyanoa meno yapate kuuma vizuri nyama mgumu ya ufisadi.
 
Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Mimi siungi mkono kauli ya Dr.Edward Hosea wala sijawahi kumsifia ila JF ni jukwaa huru hivyo tuna nafasi ya kujadili utendaji wa kila siku wa taasisi za umma. Ni kweli utendaji ni mbovu kiasi cha watu kuibatiza jina la TAASISI YA KULINDA NA KUENDELEZA RUSHWA (TAKUKURU) nchini Tanzania.Lakini kuna Watanzania wengi wasioijua taasisi kwani haijajipambua kiutendaji.Tatizo la rushwa bado ni ufa unaolitafuna taifa,je tukate tamaa ya kutaka mageuzi katika taasisi hii? Basi ni nini kifanyike ama tunadhani kitafanyika ila TAKUKURU iwe ni kimbilio la wanyonge?
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,151
2,000
hawezi kitu mzee, ni mmoja wao. simnakumbuka alivyowatetea Richmond (dowans), kuwa hakuna dalili za rushwa wala ufisadi.
 
Top Bottom