kitambiheshima
JF-Expert Member
- May 27, 2013
- 452
- 116
Ninakushauri ufuatilie nyendo za maafisa wako na utabaini haya ninayoyasema. Huku mikoani vijana wako ni wataalam wa "kuvuta mshiko". Wanachofanya ni kutishia watumishi wala rshwa na wakati mwingine kuwahakikishia "usalama" ili wawape chochote. Ofisi yako huku mikoani na wilayani, siyo ya mapambano dhidi bali ni mapambano ya kulinda rushwa. Maafisa wako huku, polisi wao, tra wao, mahakimu wao, traffic wao, usalama wao, mchwa wao n.k. Fanya ukaguzi wa kushtukiza wa kesi kwenye file zao, utabaini zile zenye dili ya pesa hazitumwi kwa dpp, zinapigwa danadana hukohuko watu wanamalizana juu kwa juu. Kama huamini fanya uchunguzi mzee. Ila tatizo hata wewe juzijuzi nimesoma kashfa yako humu kuwa ulichota vi "m" kadhaa vya ofisi kwaajili ya graduation ya mwanao u.s.a, sasa sijui kama hili utalifanyia kazi. Anyway ujumbe huo pokea.