DR CONGO: Padri mwengine auawa kwa kupigwa risasi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
_100760882_c7915ece-2f7c-4218-9ca7-ea0d5021fc56.jpg
​

Kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.

Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimearifu kuwa Padri Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini na ndipo wakati mtu mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.

Tukio hilo lilijiri wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.

Taarifa zinadai kuwa muuaji huyo ni kutoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji

Chanzo: BBC Swahili
 
Dictator Kabila katika jitihada zake za kutaka kuwafunga midomo makasisi..
 
Iskute ni subortage ya kumng'oa kutoka kwa maadui zake
 
Dini na serikali vitu viwili tofauti,tatizo viongozi wa ya kikristo huko DRC kazi yao si kuubiri wao ni kukosoa serikali,ndiyo kazi hiyo? Hayo ndio malipo take.
 
Kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.

Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimearifu kuwa Padri Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini na ndipo wakati mtu mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.

Tukio hilo lilijiri wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.

Taarifa zinadai kuwa muuaji huyo ni kutoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji

Chanzo: BBC Swahili
hata mkiua mapadri wote bearing in ur mind kanisa la kitume katoliki halitakaa kimya daima.
 
Dini na serikali vitu viwili tofauti,tatizo viongozi wa ya kikristo huko DRC kazi yao si kuubiri wao ni kukosoa serikali,ndiyo kazi hiyo? Hayo ndio malipo take.
siasa ni maisha huwezi kutenganisha maisha na siasa.mapadri wanawajibu wa kukemea yote yanayotokea kwenye nchi.
 
Wanazidisha mkuu mpaka wanachochea maandamano! Aisee hiyo Kali,hapa Home Sizonje amewapiga mkwara ukawa VP hapo
 
Congo noumer, ndiyo maana wanapiga kiwi viatu wakiwa wamevaa wanakwambia muda wowote anakimbia na hawajengi wananunua magari mazuri wanasema hawawezi kukimbia na Nyumba.
 
Dini na serikali vitu viwili tofauti,tatizo viongozi wa ya kikristo huko DRC kazi yao si kuubiri wao ni kukosoa serikali,ndiyo kazi hiyo? Hayo ndio malipo take.
Kwanza kuandika kwenyewe shida tu, The evil triumph when men of God are silence. ( maovu hushamili watu wema wanapokaa kimya)
 
Back
Top Bottom