Huyu jamaa hana jipya, mimi ni mkazi wa Ngara na nimemjua huyu jamaa toka ameanza harakati zake kupitia CCM. Uchaguzi wa mwaka 2010 akiwa CCM alihonga sana vijana na kina mama pesa na simu ili ashinde kura za maoni, nakumbuka wakati huo alikuwa na project fulani aliyokuwa anaifanyia kupitia wafadhili aliitumia kama njia ya kujipigia debe lakini matokeo yake akashindwa na Ntukamazina. Baada ya kuanguka kwenye kura za CCM aliungana na wenzake walioanguka kama lugumya mheto kumpiga vita Ntukamazina ili jimbo lichukuliwe na NCCR, wakati huo mimi nilikuwa mmoja ya waliokuwa wakimnadi mgombea wa NCCR Sam Ruhuza kwa hiyo nilikuwa naona kila kitu walichokuwa wanafanya ku-sabotage kampeni ya chama chao. Aliebaki upande wa Ntukamazina alikuwa Alex Gashaza ambaye alimpigia kampeni jamaa hata wakati alipougua na kwenda kutibiwa India mwezi wa mwisho wa kampeni. Kilichotokea sasa hivi wananchi wengi wa Ngara wanamuona Alex Gashaza ndiye anafaa kuwa mrithi wa Ntunkamazina 2015 jamaa kaamua kukimbilia CHADEMA. Wasijione wamelamba dume, hilo ni galasa. Kama kweli wanalitaka hili jimbo CHADEMA nadhani watafute mtu anaeuzika kwa vijana na watu wa vijijini ambao ndio idadi kubwa ya wapiga kura, la sivyo CCM watatawala milele.