Dr. Bagonza: Mkandamizaji wako wa jana hawezi kuwa mkombozi wako wa leo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,208
103,782
UASI NA UZALENDO VINAPAKANA HIVI?​

Tujadili:

Kila nyuma ya mwanamme aliyefanikiwa, kuna mwanamke mwenye nguvu.

Kila nyuma ya mwanamke anayeasi, kuna mwanamme mwenye nguvu.

Kila nyuma ya mwanamke mwenye hekima, kuna Mungu.

Kila nyuma ya mwanamme mwenye hekima, kuna kusubiri.

Mkandamizaji wako wa jana hawezi kuwa mkombozi wako wa leo.

Mkandamizaji anapomhitaji sana mkandamizwaji ujue kuna utakatishaji wa mavuno.

Tuanue matanga.
 
"Kila nyuma ya mwanamke anaeasi kuna nguvu ya mwanaume"

Swali linakuja huyo mwanaume mwenye nguvu yupo ndani ya chama chao au nje?

Anyway, jibu la swali hilo tutalipata kwenye mstari wake huu;

"Kila nyuma ya mwanaume mwenye hekima kuna kusubiri"

Naamini mkutano wa Chadema na waandishi wa habari utatoa jibu.
 
Ukimuamini mwanamke utalea watoto si wako. Chadema, mmeshaletewa mimba tayari.
 
Kwa muktadha huu huu wa Dr. Bagonza pia tuendelee kujiuliza; Robert Amsterdam, wakoloni wetu wa zamani Ujerumani na Brussels makao makuu ya EU anakotoka King Leopold aliua raia wa Congo DR 10mil; hawa ndio watetezi wa TAL na haki za binadamu.

Wakoloni kwa miaka 75 na zaidi ya kuzitawala nchi za Afrika na uvunjifu wa haki za binadamu; leo wanapowatuma akina Amsterdam, ni kwa wema upi toka kwa wazungu
 
Kwa muktadha huu huu wa Dr. Bagonza pia tuendelee kujiuliza; Robert Amsterdam, wakoloni wetu wa zamani Ujerumani na Brussels makao makuu ya EU anakotoka King Leopold aliua raia wa Congo DR 10mil; hawa ndio watetezi wa TAL na haki za binadamu...
Barikiwa zaidi. Umenena mema yasiyothaminiwa na waafrika wengi. Alikuita kila aina ya jina baya na ni juzijuzi tu, miaka 60 hadi 80. Leo unamwita mtetezi.

Akili ya lisu inatia kinyaa. Nimeamini adui wa mwafrika ni mwafrika mwenyewe.
 
UASI NA UZALENDO VINAPAKANA HIVI?​

Tujadili:

Kila nyuma ya mwanamme aliyefanikiwa, kuna mwanamke mwenye nguvu.

Kila nyuma ya mwanamke anayeasi, kuna mwanamme mwenye nguvu.

Kila nyuma ya mwanamke mwenye hekima, kuna Mungu.

Kila nyuma ya mwanamme mwenye hekima, kuna kusubiri.

Mkandamizaji wako wa jana hawezi kuwa mkombozi wako wa leo.

Mkandamizaji anapomhitaji sana mkandamizwaji ujue kuna utakatishaji wa mavuno.

Tuanue matanga.
Ubeti wa mwisho umebeba Ujumbe mzito:mkandamizaji anapomuhitaji sana mkandamizwaji ujue .........
 
Back
Top Bottom