Dr Ashraf Marwan: Mkwe wa Rais wa Misri aliyegeuka kuwa Jasusi wa Mossad.

Dr Ashraf Marwan: Mkwe wa Rais wa Misri aliyegeuka kuwa Jasusi wa Mossad.

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
6,499
Reaction score
18,166
Kama ungebahatika kutembelea jiji la Cairo hususani siku ya tarehe moja mwezi wa saba mwaka 2007, ungegundua ni siku na mwezi ambapo hali ya hewa ilikuwa ni joto kali sana kiasi kwamba muda wote ungekuwa unatokwa na jasho.
stock-photo-cairo-egypt-january-busy-port-said-street-in-cairo-egypt-2157798551.jpg
Mitaa mingi ya mji wa cairo ikiwa ina msongamano ndivyo ilivyozidi kuchangia joto kuwa kali zaidi kwa siku hiyo. Madereva teksi nao wakiwa bize wanapambana kupenyeza huku na kule na teksi zao wakijaribu kutafuta wateja au wakipiga honi katika kuwashtua watu wawapishe wawawaishe abiria. Kila mtu akiwa kwenye pilikapilika za hapa na pale katika kujitafutia riziki.
a-busy-street-scene-in-cairo-egypt-ABFB63.jpg

Hakika siku hii ilikuwa bize sana.
Na pia katikati ya jiji hili la cairo pia ungebahatika kutembea siku hiyo, ungegundua pia soko maarufu la Khan-khalil Bazaar lililopo katikati ya jiji lilikuwa limefurika wanunuzi haswa na idadi kubwa ya kina mama waliovalia hijabu wakifanya manunuzi ya mahitaji ya nyumbani. Hata pia watalii nao ungewaona wakiwa wametapakaa kwenye soko hili maarufu wakitalii huku na kule katika kufahidi uzuri wa soko hili la zamani lililo katikati mwa jiji. Kwa kifupi mitaa mingi ya mji wa cairo siku hii ilikuwa bize haswa. Unaweza kupafananisha na mitaa ya kariakoo na viunga vyake unavyokuwa bize pale dsm .

Sasa basi pamoja na ubize wote na hekaheka ndani ya jiji hili la cairo siku hii hazikuzuia shughuli maalumu iliyokuwa ikiendelea kwenye msikiti mkubwa kabisa wa Omar bin Abdul Aziz ulioko katikati kabisa mwa jiji.
Msikiti huu mkubwa siku hiyo ulikuwa umefurika mamia ya waombolezaji. Wengi wa waombolezaji hawa walikuwa wanasiasa mashuhuri, maafisa wa ngazi za juu wa serikalini na wa kijeshi pamoja na wafanyabiashara wakubwa . Waombolezaji hawa walikuwa wamehudhuria katika msikiti huu kutoa heshima zao za mwisho kwa "mtu mzito sana aliyeaga dunia"ambaye kwao walimuona kama rafiki, mwanafamilia, kipenzi cha watu na pia kama patna wa kibiashara. Aliyekuwa akiagwa hakuwa mwingine bali ni mwendazake Dr. Ashraf Marwan.
10261034_0_0_1000_1486_0_x-large.jpg

Ni nani huyu mtu haswa?

Huyu bwana Marwan alifariki siku nne nyuma kabla yaani tarehe 27 june 2007 ,tena kifo chenye utata kidogo. Hii ni baada ya kusemekana alianguka kutoka kwenye nyumba ya ghorofa ambayo ni apartment yake iliyopo 5th floor aliyokuwa akiishi karibu na moja ya mtaa wa kifahari wa Carlton terraces karibu na makutano ya barabara ya Piccadilly Circus huko London uingereza.
168003-featured-image-1.jpg

Huyu bwana ashraf katika siasa za pale Misri alikuwa amejijengea CV nzito sana.Kivipi ? Kwanza huyu bwana ashraf alikuwa amemuoa binti wa rais wa misri bwana Abdel nasser gamal, aliyeitwa Mona mwaka 1966.
marwan-marries-nasser-nasser-marwan-wedding.jpg


nasser-marwan-wedding (1).jpg

Kitendo cha huyu bwana ashraf kuoa kwenye familia ya rais kulimpa tiketi ya kuwa mmoja wa wanafamilia na kumfanya ajikute kwenye nafasi za uongozi wa juu katika taifa la Misri kama mshauri wa rais Abdel nasser na pia mshauri wa hayati Anwar sadat. Hii ilimfanya hata baada ya kustaafu kujikuta ametengeneza "connections" za kibiashara na wanasiasa pamoja na wafanyabiashara wakubwa kwenye nchi za kiarabu ambapo naye alijikuta akimiliki biashara kubwa kubwa na nzito zenye kumuingizia pesa ndefu. Huyu bwana ashraf alikuwa akiishi London tokea mwaka 1981 hadi mauti yalipomkuta.

Sasa basi , Mwili wa bwana ashraf ulipokelewa kwenye uwanja wa ndege wa cairo mapema siku hii ya tarehe 1 july.2007 ukilakiwa na waziri wa uchukuzi wa anga bwana Ahmed shafik pamoja na katibu mkuu ofisi ya rais wa misri Dr. Zakaria Azmi.(wakati huu rais akiwa Hosni Mubarak). Kisha kupelekwa kwenye msikiti wa Omar bin Abdul Aziz kwa ajili ya ibada ya swala maalumu ya kumuombea pumziko la amani kwa Allah.
relatives-and-friends-of-egyptian-billionaire-ashraf-marwan-read-the-holy-koran-around-his.jpg

gamal-and-ahmad-marwan-sons-of.jpg

Katika msikiti huu mtoto wa rais Hosni Mubarak aliyeitwa Gamal au jimmy Mubarak alikuwa bize kumliwaza mjane pamoja na watoto wa ashraf Marwan. Kwa kifupi familia ya Dr. Ashraf Marwan pamoja na familia ya hosni Mubarak walikuwa pia ni marafiki wakubwa kwa miaka mingi.

Katika siku hii rais Hosni Mubarak hakuweza kuhudhuria katika msiba wa wa bwana ashraf kwani alikuwa yupo nje ya nchi akihudhuria mkutano wa viongozi wa afrika huko accra Ghana lakini alitoa salamu zake kwa ashraf akimtaja kama "Mzalendo wa kweli katika taifa lake".Salamu hizi za hosni Mubarak kwa ashraf ziliwakilishwa na kusomwa rasmi msibani na jenerali Omar suleiman ambaye alikuwa ni mkuu wa idara yaujasusi wa misri.

Ibada ya kumuombea bwana Ashraf iliongozwa na Muhammad Sayyid Tantawy ambaye alikuwa ni imamu mkuu mstaafu wa Misri. Msiba huu ulikuwa umehudhuriwa na watu mashuhuri karibia nyanja zote ndani ya taifa la misri. Lakini jambo moja ambalo waombolezaji waliokuwepo walitambua katika ibada hii ya kumuombea bwana Ashraf, hawakuweza kuona mwanafamilia au mwakilishi yoyote aliyehudhuria msiba huu kutoka kwa familia ya Anwar Sadat, Rais aliyeuawa mwaka 1981 ingawaje zilikuwa familia rafiki(hii ni topic nyingine)

Sasa basi Katika msiba huu , yupo mtu mmoja au zaidi ya mtu mmoja ambao walikuwa wanaujua UKWELI MCHUNGU kuhusu mtu waliyekuwa wakitarajia kumzika yaani.ASHRAF MARWAN. Watu hawa walijua kilichokuwa kikiendelea hapo ni maigizo yaliyopangwa tu kuufunika ukweli ila kiuhalisia walijua wanayemzika hakuwa mzalendo bali MSALITI mkubwa kwa taifa la Misri. Yes Ni kweli alikuwa ni TRAITOR Haswa. Kivipi sasa bwana huyu aliyekuwa na connection hadi ikulu ya misri na pia alioa binti wa Rais ni msaliti tena? Na ni nani hao waliosalitiwa na huyu ashraf?Ipo hivi ...

Ngoja nikurudishe nyuma kidogo hadi miaka ya 1990s.


Kulikuwa na fununu zinatembea mtaani kwamba shirika la kijasusi la Israel la Mossad limepandikiza mtu ambaye ni double agent yaani pandikizi kwenye nafasi nyeti ndani ya taifa la misri hususani katika miaka ile Israel ikiingia kwenye mgogoro wa kivita na nchi za kiarabu mwaka 1973.

Sasa basi jambo hili lilibainika na kudhihirika
mwaka 1993 pale mkuu wa kitengo cha ujasusi jeshini wa Israel meja jenerali Eli Zeira alipochapisha makala ikielezea kwa kina kuhusu huyu mole au double agent.

Katika makala ya jenerali huyu, alibainisha huyu Mole au pandikizi aliyewekwa na Mossad alikuwa ni "double agent" ambaye pia anauza siri za kijeshi za Israel katika vita ya Yom Kippur, pale ambapo waaarabu walipoivamia Israel wakiwa katika sikukuu yao takatifu ya kiyahudi ambapo huyu bwana Zeira alikiri almanusura Israel wapoteze katika hii vita.

Kutokupoteza kwa Israeli kwenye hii vita ya Yom kippur ni huyuhuyu double agent kuwasanua mwishoni dakika za 90 Israel kuhusu next move ya jeshi la misri na na mipango yao hivyo ikabadili mkondo wa vita na Israeli ikashinda.Sasa baada ya muda kupita katika harakati za kumjua huyu double agent ni nani ilibainika alikuwa ana connection na familia za rais Abdel nasser na Anwar sadat. Baadhi ya waisraeli wachache waliokuwa wanamjua huyu double agent walimpa jina la Utani la "son in law" au "MKWE".

Kutokana na hizi fununu na uzushi kama zinamlenga bwana Ashraf Marwan, alipohojiwa na waandishi wa habari wa misri na kuulizwa kama yeye ni "Spy" Bwana ashraf alikanusha yote kumhusu yeye kuhusishwa na kuwa jasusi .

Mbali na kukana hizi shutuma, mwanahistoria raia wa Israeli aliyekuwa profesa wa historia kutoka chuo cha King's college cha London bwana Ahron Bergmann aliwadhibitishia waandishi wa habari wa misri kwamba Ashraf Marwan ni "spy".

Lakini mbali na hizi shutuma, bwana Ashraf aliendelea kukana katu yeye sio "spy" mbele ya vyombo vya habari. Sasa basi ilipofika june 7 mwaka 2007 kwenye mji wa Tel Aviv vikao vya kesi dhidi ya ashraf Marwan vilianza kunguruma mahakamani kuhusu tuhuma zinazomkabili. Sasa hapa huyu bwana Ashraf Marwan akahisi kamba ya kitanzi inazidi kumkaba koo. Lakini ghafla tu wiki tatu baadaye AKAFA tena kifo cha utata kabla ya kufika mahakamani.

Sasa tukirudi katika msikiti huu kunapofanyika ibada ya kuuaga mwili wa Ashraf Marwan, wachache kati ya waombolezaji waliohudhuria walijua nini haswa kinaendelea kuhusiana na kifo cha bwana huyu. Mmojawapo alikuwa ni huyu jenerali Muhammad suleiman aliyemwakilisha rais Hosni Mubarak. Jenerali huyu alijua nini haswa kimempata bwana Ashraf na ni nani alitoa "ORDER" haswa ya kumu "eliminate" bwana Ashraf kabla ya kupelekwa mahakamani.

Kuna nadharia iliibuliwa na kudai kwamba huenda Lengo la kumzima bwana Ashraf lilikuwa ni kuutenga utawala na uongozi wa misri dhidi ya Kashfa na aibu kutokana bwana Ashraf kutuhumiwa na kufunguliwa kesi mahakamani kuwa aliwahi kuwa jasusi wa Israeli kitu ambacho wamisri hawakukiamini . Hii ni kutokana na jina alilolijenga ndani ya nchi ya misri . Kwanza ni mkwe wa rais,mshauri wa rais na pia rafiki wa karibu wa Hosni mubarak n.k iweje awe jasusi tena wa MOSSAD?
Nadharia ya pili iliibuka kwamba Mossad wenyewe ndio waliamua kum " eliminate" baada ya kumtumia ashraf katika kuvujisha siri za utawala wa misri na mipango yake ya kijeshi kipindi akiwa London miaka ile ya mwishoni mwa 60 na 70 .

Nadharia nyingine inadai kwamba baada ya huyu bwana ashraf. Marwan kuwa na connection kubwa za kibiashara , maadui zake wa kibiashara ndio waliamua kumzima , pengine kutokana na kufanyiana dhulma haswa kwenye mgao wa pesa , kwakuwa ilisemekana huyu bwana aliwahi kuhusika kwenye biashara za silaha miaka ile ya 90 kati yake na Rwanda wakati ikipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na Uganda licha ya yeye kuwahi kumiliki hisa zake kwenye klabu ya Chelsea miaka hiyo .

Haijawahi julikana haswa ni nani kati ya hao watatu kati ya Israel,misri na wafanyabiashara wenzake ndio walioamua kumzima.

Lakini mwaka 2010 kwenye chapisho la gazeti la The standard ,mjane wa ashraf Marwan alitoa shutuma akidai kwamba mumewe alikuwa akifuatiliwa na majasusi wa Mossad na ndio huenda waliomuua🧐🧐🧐🧐.

london-mona-abdel-nasser-attends-the-book-launch-of-rowan-somervilles-latest-book-the-end-of.jpg


Screenshot_20260201-112716~2.jpg

Screenshot_20260201-112937~2.jpg

Lakini kwenye ulimwemgu wa ujasusi Kuna Nukuu moja inasema hivi "As with all Spy stories, the lines between Truth, lies, facts and fiction are never quite what they seems'

Anyway dunia ina mengi Hususani ya huku Afrika 😎😎
 
Caleb na Joshua ndo Mossad wa kwanza. Walijipenyeza hadi kwenye kuta za Jericho. Hawa watu wa MUNGU WA KWELI ni noma. Nawaambiaga watu hata Ayatollah mwenyewe ni Mossad hawaamin. Aliwauza General Suleiman, Ebrahim raisi, Ismail Hanniyeh na Hassan Nassrallah. Putin pia Mossad. Rais wa Syria Sharaa ni Mossad, Sisi wa Misri Mossad, MBS wa Saudia Mossad, Erdoğan wa Turkey Mossad na Al thani wa Qatar mossad tena aliwauza viongozi wa Hamas.

Ni hawa tu miarabu mitarajiwa niggers mieusii zenye sijdah kuubwa kama chapati ndio siyo mosad.

adriz de mbusii
 
***** kila ntu ni Mossad hata litrump ni liyahudi tu
Caleb na Joshua ndo Mossad wa kwanza. Walijipenyeza hadi kwenye kuta za Jericho. Hawa watu wa MUNGU WA JWELI ni noma. Nawaambiaga watu hata Ayatollah mwenyewe ni Mossad hawaamin. Aliwauza General Suleiman, Ismail Hanniyeh na Hassan Nassrallah. Putin pia Mossad. Rais wa Syria Mossad, sisi wa Misri Mossad, MBS wa Saudia Mossad, Erdoğan wa Turkey Mossad na Al thani wa Qatar mossad tena aliwauza viongozi wa Hamas.

Ni hawa tu miarabu watarajiwa niggers mieusii zenye sijdah kuubwa kama chapati ndio siyo mosad.
 
Back
Top Bottom